Wenyeji wa Melbourne Wawakaribisha Wakimbikizi wa Syria kwa Mikono Miwili—na Panzi

Welcome to Eltham

Karibuni Eltham – picha ya ukurasa wa Facebook wa Welcome to Eltham

Wenyeji kutoka mtaa wa mji wa Eltham wanawakaribisha wakimbizi wa Syria ambao wanatarajiwa kuanza kuishi kwenye makazi yao hivi karibuni kwa chakula cha panzi waliokaangwa nyumbani.

Wa-Syria mia moja na ishirini wanatarajiwa kupewa mahali pa kuishi kwenye jengo lisilotumika la kulelea wazee. Ushirikiano wao umefika mpaka mtaani na hata kwenye mitandao ya kijamii —ukurasa wao wa Facebook, Welcome to Eltham, una zaidi ya watu 7,000 wanaoufuatilia.

Kikundi hicho kinatumia panzi kama alama yao na waliwatumia kupamba mji ili kupambana na chuki dhidi ya wahamiaji: “Panzi wetu wanatukumbusha kuwa hata kitendo kidogo kinaweza kuwa na matokeo makubwa.”

Mkazi mmoja, mwigizaji na mwimbaji Drew Weston, alizungumzia hisia hizi kama ifuatavyo:

Nina furaha kuwa kijana wa mji wa Eltham leo. Karibuni Eltham

Video hii inaelezea kampeni hiyo:

Karibu watu 9,000 wametia saini wito huo kwenye Mtandao wa Hatua kwa lengo la kuwakaribisha wakimbizi kwa mikono miwili:

Kuna wakimbizi wa Syria wapatao milioni 11 duniani kote. Eltham imeombwa kusaidia kwa wakimbilizi 120.

Tuna nafasi mjini kwetu na mioyoni mwetu kuwaonyesha huruma na kuelewa hali yenu.

Jiunge na Kairbu Eltham na uweke ahadi ya kusema: wakimbizi wanakaribishwa.

Wakimbizi ni sehemu ya kundi maalum la wa-Syria na wa-Iran 12,000 walioahidiwa mwaka 2015 na serikali ya Tony Abbott nchini Australia baada ya shinikizo la umma.

Mwitikio mzuri wa wakazi wa Eltham unakabiliwa na upinzani pia. Mikutano ya watu wasiounga mkono walimbizi ilifanyika Novemba 5, huku upande unaowaunga mkono wakimbizi ukidai kushinda siku hiyo:

Wapinzani walishindwa mjini Eltham. Walikuja kutafuta kupigana lakini wakitana na watu wa amani

Maandamano ya watu wasiounga mkono wakimbizi yalilaumiwa na watu wasioishi kwenye eneo hilo:

Niko kwenye hatari ya kurudia yale yale: wengi wa wapinzani hawatoki Eltham bali Sydney, Bendigo na Melton

Waandaaji wa mikutano ya kupinga wakimbizi, Chama cha Uhuru (PF), wanaeleza kwenye ukurasa wao wa Facebookkwamba kikundi chao:

kikaukataa mwingiliano wa utamaduni, kinatetea sera ya wahamiaji inayozingatia kufanana kwa utamaduni, kinapinga u-Islam kwa kuuona kama kimsingi hauendani na tuni hizi, na unataka kutawala mipaka ya Australia.

Kuna angalau ukurasa mmoja wa Facebook wa Hamkaribishwi Eltham. Ukurasa huo hauko hai, labda kwa sababu ya msimamo wake.

Mwisho, video hii ya Eltham inaonesha wenyeji wakisoma maoni yaliyowekwa na wapinzani wa mtandaoni:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.