Tukio Mubashara la Facebook Kukuza Amani na Kupambana na Kauli za Chuki Nchini Kenya

The logo of the public Facebook group - Promoting Peace - Fighting Hate Speech.

Nembo ya kundi la mtandao wa Facebook:  kukuza amani- kupambana na kauli za chuki.

DW Akademie, taasisi ya Kijerumani kwa ajili ya maendeleo ya vyombo vya habari kimataifa, kinaandaa tukio mubashara kwenye mtandao wa Facebook kuhusu mikakati ya kupambana na kauli za chuki nchini Kenya wakati nchi hiyo ikielekea kwenye uchaguzi mkuu mwakani.

Tukio hili litafanyika leo Novemba 14 na Novemba 16 saa 12 jioni za Afrika Mashariki (UTC +3) kwenye kundi jipya la Facebook liitwalo: Promoting Peace – Fighting Hate Speech [Kukuza Amani – Kupambana Kauli za Chuki]

Waendesha mjadala wa kipindi hicho mubashara ni  Chrispin Mwakideu, mwandishi wa kujitegemea wa DW nchini Kenya, mwandishi na msanii wa sanaa za maonyesho, na Joan Okitoi, Meneja wa Mradi wa DW Akademie maktaba ya ugunduzi wa kidijitali, Shitemi Khamadi, mwandishi wa habari wa Kenya na mtaalamu wa kauli za chuki mtandaoni, atashiriki pia.

Kupambana na kauli za chuki ni muhimu sana, kwa kuangalia yaliyotokea nchini humo miaka ya hivi karibuni. Ghasia za baada ya uchaguzi  zilitokea baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 kufanyika. Mamia ya watu na makumi elfu walikimbia makazi yao.

Hapa chini unaweza kuona kipande kidogo cha video ya YouTube kuhusu tukio hilo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.