Serikali ya Ethiopia Yamshikilia Mwanablogu wa Zone9 Befeqadu Hailu kwa Kigezo cha ‘Hali ya Hatari’

Zone9 members rejoice at the release of Befeqadu Hailu (second from left, in scarf) in October 2015. Photo shared on Twitter by Zelalem Kiberet.

Wanakikundi wa Zone9 wakisherehekea kuachiwa kwa Befeqadu Hailu (wa pili kutoka kushoto, aliye na skafu) manamo Oktoba 2015. Picha iliwekwa kwenye mtandao wa Twita na Zelalem Kibret.

Befeqadu Hailu, mmoja wa watu wanaofahamika sana katika tasnia ya habari nchinin Ethiopia iliyonyimwa uhuru alikamatwa mnamo Novemba 10, 2016. Majira ya asubuhi, serikali ilimakamata Befeqadu akiwa nyumbani kwake na kumuweka katika sero iliyo katika kituo cha polisi kilicho karibu na nyumbani kwake. Alishikiliwa hapo kwa siku nzima na baadae alihamishiwa katika kituo cha jirani kiitwacho Kotebe.

Akiwa mmoja wa wanakikundi mzoefu wa kundi la Zone9 na pia mwandishi wa Global Voices, Befeqadu ni anatumia vyema sana karama yake ya uandishi kupitia Blogu na kwenye Twitter. Mara tu baada ya serikali ya Ehtiopia kutangaza hali ya hatari, aliandika:

Serikali ya Ethiopia “imetangaza hali ya hatari” inayodumu kwa miezi sita. Kama “ilivyo kawaida ya washukiwa”, kwa sababu ya ukosoaji wetu, mimi pamoja na marafiki zangu tuna hofu kuu isivyo kawaida. Kama kawaida, imekuwa ni jambo la hatari sana kuikosa serikali hapa (Ethiopia). Tamko hili limeipa serikali mamlaka ya kutukamata bila hata huruma. Ninachapisha maneno haya kupitia blogu kwani nina hofu kuwa ninaweza kukamatwa mda wowote. Kama itakuwa hivi, ninataka watu wanisome na wanielewe. Ninapenda pia watu waelewe namna ninavyokubali maandamano yenye changamoto tele nchini Ethiopia. Ni jaribio la kutaka kuishi kama mwanadamu mwenye utu.

Serikali haikuweka bayana lengo la kukamatwa kwa Befeqadu, hata hivyo walimwambia kuwa alikuwa anatakiwa kuonana na kiongozi wa ngazi ya juu wa jeshi (anayefahamika pia kama mwenye amri) kama sehemu ya utekelezaji wa hali ya hatari. baadae aliambiwa kuwa mahojianao aliyoyafanya na Idhaa ya Sauti ya Amerika katika lugha ya Kiamhari kuhusu hali ya hatari iliyotangazwa nchini Ethiopia ndio sababu ya kukamatwa kwake, na kwamba anaweza kukutwa na hatia au kupatiwa mafunzo “kabilishi”.

Rafiki na mwandishi menzake Zelalem Kibret alipakia katika ukurasa wa Twitter taarifa ya sauti ya dakika tano kutoka idhaa ya Kiswahili inayodhaniwa kuwa ndiyo iliyopekea Befeqadu kukamatwa. Kipande hiki cha sauti kipo katika lugha ya Kiamhari.

Maandamano yamekuwa yakifanyika nchini Ethiopia katika eneo la Oromia tangu Novemba 2015 na kusambaa katika maeneo mbalimbali ya nchi katika kipindi cha miezi kadhaa ya hivi karibuni, ambapo waandamanaji wamekuwa wakidai, utawala binafsi, uhuru na heshima miongoni mwa watu wa kabila la Oromo ambao kwa kipindi cha robo karne iliyopita wameshuhudia unyanyaswaji na ukandamizwaji wa makusudi. Serikali imekuwa ikitumia nguvu kubwa dhidi ya waandamanaji. Mnamo mwezi Oktoba, Umoja wa Muungano wa Oromo, ambacho ni chama cha upinzani kiliripoti mauaji ya kutisha ya takribani watu 600.
Tangu serikali ilipotangaza rasmi “hali ya hatari” mwezi uliopita, mitandao ya kijamii na mitandao ya intaneti ya simu mara kwa mara imekuwa ikifungwa, watu kukatazwa kutoka nje kwa muda fulani nchi nzima na pia kuonekana kwa kwa aina yoyote ya tamko au ishara inayoashiria kuikosa serikali inaweza kumpelekea mtu kuadhibiwa.

Zone9 bloggers Atnaf Berahane, Natnael Feleke and Abel Wabella waladvocate for Befeqadu's release in 2015. Image shared widely on Twitter.

Wanablogu wa Zone9 Atnaf Berahane, Natnael Feleke na Abel Wabella wakihamasisha kuachiwa huru kwa Befeqadu mwaka 2015. Picha ilisambazwa kwa wingi sana katika mtandao wa Twitter.

Kutokana na juhudi zake kuu za mtandaoni za utetezi wa haki za binadamu na utawala wa sheria nchini Ethiopia, kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita Befeqadu ameitumia akiwa gerezani. Sambamba na Wanablogu wenzake wa Zone9 , Befeqadu mwenye umri wa miaka 35 amekuwa akikamatwa na kufikishwa mahakamani mara kadhaa. mara kadhaa. Tangu Aprili 2014 hadi Oktoba 2015, walifungwa gerezani na kisha kushtakiwa kwa Sheria ya Makosa ya Ugaidi ya nchini Ethiopia.
Mnamo Aprili 2016, rufaa ilikatwa dhidi ya wanablogu watano wa Zone9 akiwamo Befeqadu. Mahakama Kuu ilitarajiwa kutoa hukumu ya kesi hiyo manomo Novemba 15, hata hivyo, imekuwa ikiahirishwa mara kwa mara.

Mahakama kuu inategemewa kutoa maamuzi yanayosubiriwa kwa muda mrefu kuhusu kesi ya wanablogu wa @Zone9ners kesho.

Kwa bahati mbaya, Befeqadu ana marafiki wazuri kutokana na uandishi wake uliotukuka nchini Ethiopia. Natnael Feleke, ambaye pia ni mmoja wa wanakikundi wa Zone9, mwezi Oktoba alijikuta akishikiliwa katika kituo cha polisi mara baada ya kukamatwa kwa kosa la kuzungumza kwa sauti akiwa na rafiki zake wakiwa katika hoteli moja kuhusu kundi kubwa la watu kukanyagana na kupelekea vifo vya watu takribani mia moja mwishoni mwa mwezi Septemba.

Seyoum Teshome, mwanablogu mashuhuri ambaye alikamatwa mwishoni mwa mwezi Septemba hatma yake bado haijajulikana. Miezi miwili tangu kukamatwa kwake, serikali bado haijaeleza sababu za kukamatwa kwake wala kusomewa mashtaka yoyote.

Jumuia ya Global Voices ipo pamoja na Befeqadu. Tunaitaka serikali ya Ethiopia kumwachia huru mapema iwezekanavyo. Jifunze zaidi kuhusu Befeqadu na Wanablogu wa Zone9 .

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.