Picha Iliyokuwa Kichekesho Yageuka kuwa Kampeni Kubwa ya Kuwachangia Watoto Nchini Ghana

Ghanaian Internet sensation Jake Amo. Photo taken by and shared on Instagram by

Picha ya Jake Amo iliyozua gumzo kwenye mtandao wa intaneti Ghana. Picha imepigwa na Carlos Cortes na kuwekwa kwenye mtandao wa Instagram na Solomon Adufah.

Ilianza na picha. Kwenye picha hiyo, kijana mdogo aitwaye Jake Amo anaonekana akichora kwa umakini mkubwa wakati wa somo la ubunifu na sanaa shuleni kwake katika kijiji cha Asempanaye nchini Ghana. Somo hilo lilifundishwa na Solomon Adufah, m-Ghana, anayesomea uchoraji kwenye Chuo Kikuu cha Illinois, nchini Marekani. Picha hiyo ilipigwa mwezi Agosti 2015 na rafiki yake Carlos Cortes, aliyekuwa anaandaa dokumentari ya safari ya Adufah nchini Ghana. Adufah aliweka picha hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram mwezi Januari 2016.

Picha hiyo ikageuka kuwa gumzo la mtandao katika miezi ya Septemba na Oktoba 2016. Inaamika kuwa hii ilikuwa ni baada ya Watumiaji wa mtandao nchini Sudani Kusini kuchanganya picha hii na ujumbe uliokuwa ukienea mtandaoni kama huu na huu.

When they ask you to write down your past job experiences & you're writing you were an admin of Facebook page & whatsApp group". Screenshot from No chill in Mzansi" Facebook group.

“Wanapokuomba uandike uzoefu wako wa zamani na unaandika ulikuwa admin wa ukurasa wa Facebook na kundi la Whatsapp”. Picha ya ukurasa wa Kundi la Facebook la No chill in Mzansi”.

Solomon Adufah ameweza kuifanya picha hii maarufu ya Jake kuwa mpango wa uchangishaji mkubwa kumsaidia yeye (Jake) na watoto wengine kama yeye nchini Ghana. Kufikia siku ya 12, kampeni hiyo ilikuwa imepata zaidi ya Dola 12,000 za Marekani kutoka kwa wafadhili zaidi ya 500.

Adufah anaelezea nia yake kwenye kipande hiki cha kuitambulisha kampeni yake:

Akitoa maoni yake kwa habari hiyo,  Ayuba Fowoke, mwandishi wa Innovation Village, alibaini namna umaarufu wa ujumbe wa mtandaoni na matokeo ya uchangishaji huo yanavyothibitisha usemi wa Kiafrika unaosema, “mtoto huelimishwa na jamii nzima.” Fowoke aliandika:

Kumekuwa na masimulizi mengi ya namna uchangishaji unavyoweza kutatua changamoto nyingi. Lakini inasisimua kuona ujumbe hasi na wa kuchekesha inavyogeuka kuwa simulizi zuri kama lile la Jake. Kwa nyongeza, ni afadhali kama ujumbe unaoenezwa kwenye mitandao unatumika kutatua matatizo ya kijamii.

Hiki ndicho kinachotokea pale serikali na mamlaka za mitaa zinapotelekeza majukumu yake. Kuna mamilioni ya watoto wasiokwenda shule barani kote Afrika wakati wale wanaokwenda shule wanajifunza kwenye mazingira mabovu.

[…]

Hakuna uhakika kwamba watumiaji wengi wa mtandao barani Afrika na duniani kote wataacha kutumia picha za Jake kwa kueneza ujumbe wa vichekesho mtandaoni. Hata hivyo, kilicho dhahiri ni kuwa Jake na rafiki zake kijijini Asempanaye, Koforidua watasoma kwenye mazingira bora zaidi kwa kutumia vifaa bora kabisa vya kuandikia! Shukrani kwa Jake anayeonekana kuwa mwerevu na mshamba, Solomon Adufah na Carlos Cortes.

Akitwiti kuhusu Jake, Olwethu Mthathi alibainisha matokeo yake:

Jake Amo ni shujaa, alama ya ujumbe wa mtandaoni na kizazi cha mitandao ya kijamii barani Afrika

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.