- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mazungumzo ya GV: Hisia Zetu Siku Sita Kabla ya Uchaguzi wa Marekani

Mada za Habari: Marekani, Uandishi wa Habari za Kiraia, GV Face

Ni nani ataibuka mshindi siku ya Novemba 8: Trump, Hillary au Stein?

Hata kama waandishi wetu wengi wa Global Voices hawataweza kupiga kura nchini Marekani, tunajisikia kuguswa kwenye uchaguzi huu wa Urais kama ilivyokuwa kwenye chaguzi nyinginezo.

Maswali tunayojiuliza:

Katika kuelezea hisia na mawazo yetu, kila Jumatano, kuanzia Okotba 26 hadi Novemba 9, watu wanne wa Global Voices watakutana pamoja na kujadili habari motomoto zinazohusu uchaguzi wa nchini Marekani, watu nje ya Marekani wana mitazamo gani, na namna wana Global Voices wenzetu wa Marekani-wanaosafiri katika maeneo mbalimbali ya dunia, walio na uzoefu wa mambo ya siasa katika nchi nyingine-wana maoni gani kuhusu uchaguzi wa Marekani.

Maongezi #2: Jumanne Novemba 2

Tukiwa tumebakiza siku sita kabla ya uchaguzi na kabla ya kumalizika kwa minyukano ya kampeni, kila mmoja anaisubiria siku ya uchaguzi kwa bashasha.

Katika kujadili mihemko yetu kutokana na kampeni, makala haya ya pili ya toleo hili lililo katika sehemu tatu ni la kufurahisha, majadiliano ya papo ka hapo kati ya:

Majadiliano haya yalisimamiwa na Nevin Thompson, Mhariri wa mitandao ya Kijamii wa Global Voices na pia ni mhariri wa Japan.

Wiki iliyopita, mhariri wetu wa mitandao ya kijamii kutoka Beirut-Zuhour Mahmoud alisimamia mjadala uliowahusisha mhariri wetu wa Mashariki ya kati na Afrika Kaskazini-Joey Ayoub, Tori Egherman aliyeko Amsterdam, mpiga kura wa Marekani na pia ni mchangiaji wa Global Voices kutoka Iran, pamoja na Sahar Ghazi, aliyeko San Francisco, mpiga kura katika uchaguzi wa Marekani na pia ni Mhariri Mtendaji wa Global Voices. Unaweza Kuitazama makala hiyo hapa.  [1]