- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Kama Ningekuwa na Bunduki

Mada za Habari: Marekani ya Kaskazini, Marekani, Haki za Binadamu, Mawazo, Sheria, Uandishi wa Habari za Kiraia, The Bridge
PHOTO: Public domain from Pixabay. [1]

PICHA: Kwa matumizi ya umma kutoka kwa Pixabay.

Sikiliza sauti ya Jeronimo Yanez [2] baada ya kumpiga risasi Philando Castile [3]. Hiki ndicho nilichokisikia: Sauti ya mtu aliyetaka kuwa mwema mwenye silaha, akipata shida kuwa angeweza kuwa mbaya -mwenye hofu, kijana anayejilinda na giza, na hawalindi wenzake kwa yale yanayowatisha, kwa sababu alijifikiria kama afisa wa polisi.

Au, angalau, nimesikia kwenye sauti yake akitambua kuwa kumpiga risasi mtu aliyekuwa na mkewe na mtoto kwenye gari kilikuwa kitendo kibaya, na hakikuwa na ushujaa wowote. Masikioni mwangu, nimesikia sauti yake ikiwa na maumivu na wasiwasi.

Nimekuwa nikifiri kuhusu Castile. Alibeba silaha kwa sababu alifikiri angeitunza. Labda alikuwa na matamanio fulani, au alikuwa na masimulizi aliyojiambia, kwamba angetumia silaha yake kuwalinda watu aliowapenda. Kama asingekuwepo mwenye silaha, Castile angekuwa hai, asingeweza kufanya makosa wala kuwa na upendo na chuki vyote ikikua, Yanez angeshasahau tayari mambo ya tiketi aliyoiandikana na Diamond Reynolds na binti yake angepambana na mazimwi maisha yake yote.

Nimekuwa nikifiri mara zote nilipojikuta nikitendewa vitendo vya matumizi ya nguvu, na kujikuta nikitumia silaha mawazoni mwangu. Majuma kadhaa yaliyopita, mwanangu alimwona mwanaume akimshambulia mwanamke kwenye gazeti la Telegraph. Nilijikuta nikisema maneno ya kijinga kama, “Hebu acha, unachofanya sio sahihi! Kauli hiyo ilivunja ukimya. Jamaa alinitaza, akapepesa macho na kuondoka zake. Kisha akarudi na kumwomba yule mwanamke msamaha na mimi pia (kwa namna ya pekee, lakini hiyo ni habari nyingine –na kweli, niliwapigia simu polisi, au nilijaribu kufanya hivyo –lakini tena, hiyo ni habari nyingine). Vipi kama ningekuwa na bunduki kwenye koti langu? Mkono wangu ungeichukua. Kuwepo kwa silaha ungeyafanya maneno yangu yawe magumu na yenye ugomvi. Mwanangu angeishia kuniona nikimpiga risasi yule mtu, au nikimpiga mpita njia. Au hata ningeweza kumpiga risasi mwanangu, kama jambo fulani lisingeharibika.

Lakini katika hayo hakuna lililotokea. Kila alibaki salama. Ninapofikiria nyakati kama hizi niliposhambuliwa au kuona mashambulizi, siwezi kufikiri hata mara moja namna gani silaha ingefanya matokeo yawe mazuri zaidi. Hiyo sio kusema kwamba silaha isingesaidia. Lakini uzoefu wangu unaniambia kuwa mara hii ingekuwa tofauti, si sheria.

Mwisho wa wiki, nikiwa na mwenzi wangu na mwanangu tulitembelea duka la silaha. Ni kweli, vijana walikwenda ndani na kuangalia mapanga, visu na bunduki. Nilielewa: vichwa vyao vilikuwa vimejaa icha za watu wema waliokuwa na bunduki maisha yao yote, na walihitaji kuingia kwenye maisha ya namna hiyo wakati ule. Nilikuwa na wasiwasi kidogo na Jeronimo Yanez na Philando Castile walikuwa kama vijana wangu.

Nikiwa sina hamu, nilitafuta ishara zikiuzwa kwenye kuta la duka hilo: Acha! Mmliki ana silaha na ni wa hatari! Ushibiti wa silaha unaweza kufikia lengo lako! Kila kitu kilikuwa na harufu ya woga na upweke. Hakuna kilichosemwa: Pumua na hesabu mambo mazuri uliyonayo maishani, na kukumbuka kuwa sisi ni wa thamani sana.