Vijana Wanaojifunza Mchezo wa Kuteleza Afrika Kusini Wafanya kama Filamu ya ‘Valley of a Thousand Hills’

A screenshot of the documentary "Valley of a Thousand Hills."

Picha iliyopigwa kwenye dokumentari iitwayo, “Bonde la Vilima Elfu.”

“Valley of a Thousand Hills” [Bonde la Vilima Elfu] ni filamu ya maisha halisi ya hivi karibuni inayohusu Kambi ya Indigo ya Kuteleza, mradi unaojaribu kutengeneza kizazi cha kwanza cha watelezaji wa ki-Zulu kwenye kijiji cha Isithumba, jimbo la Kwazulu-Natal nchini Afrika Kusini. Kijiji hicho kinazungukwa na vilima 1,000 ambavyo ndio sababu ya jina la filamu hiyo.

Kambi hiyo imeanzishwa na mtaalamu wa mchezo wa kuteleza nchini wa Afrika Kusini aitwaye Dallas Oberholzer. Mchezo wa kuteleza hauna umaarufu sana nchini Afrika Kusini, hasa miongoni mwa raia weusi.

Pamoja na mchezo huo wa kuteleza, watoto wapatao 30 mpaka 40 wanaoshiriki mpango huo wanafundishwa nidhamu, afya na usalama, sanaa na muziki.

Filamu hiyo iliyotengenezwa na Jess Colquhoun, mtayarishaji wa filamu na mpiga picha na Huck Magazine. Itazame hapa:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.