Urusi Inadaiwa Kuwa na Mpango wa Kuufungia Mtandao wa LinkedIn

The end of LinkedIn in Russia?

Mwisho wa mtandao wa LinkedIn nchini Urusi?

LinkedIn, mtandao mkubwa zaidi unaowaunganisha wataalam, uko hatarini kufungiwa nchini Urusi, ambapo maafisa wa serikali wanaopeleleza taarifa za watu wamefanikiwa kuishawishi mahakama kuufutilia mbali mtandao huo nchini humo.

Jaji wa mahakama nchini humo amejiridhisha kuwa LinkedIn hutumia taarifa binafsi za watu wasioutumia mtandao huo bila ridhaa yao. Katika kile kinachoonekana kuwa matokeo mabaya, mahakama moja mjini Moscow ilijiridhisha kuwa LinkedIn hukusanya taarifa za watumiaji wake wa Urusi bila kuzihifadhi nchini Urusi – kinyume na takwa la kisheria lililoanza mwaka jana kuyabana makampuni yote ya kigeni yanayotoa huduma za intaneti.

Kwa mujibu wa gazeti la Kommersant, wapelelezi wa taarifa za watu kutoka serikalini wameamua kupambanana na LinkedIn kufuatia kuvuja kwa taarifa za watuamiaji wake. Mapema mwaka huu, ilifahamika kuwa kampuni hiyo ilipoteza watumiaji wapatao milioni 167 kwa sababu ya kuvuja kwa taarifa zao – kiasi kinachozidi watumiaji milioni 6.5 waliokuwa wamekadiriwa hapo awali.

Wafuatiliaji wa serikali wanasema waliamua kwenda mahakamani kwa sababu LinkedIn haina wawakilishaji wake nchini Urusi. Mtandao huo unakadiriwa kuwa na watumiaji walioandikishwa wapatao milioni 5 nchini Urusi (nusu yao wanaaminiwa kuutumia mtandao huo mara kwa mara) na watumiaji milioni 400 duniani kote.

Katika kesi hiyo, wafuatiaji wa Urusi wanadaiwa kujenga hoja kuwa LinkedIn inakusanya na kutuma taarifa za raia wa Urusi, wakiwemo wa-Rusi wasio wanachama wa mtandao huo, na hivyo kuvunja sheria hadhaa za haki ya faragha. Mahakama hiyo imetoa hukumu hiyo na kuipa serikali ushindi mnamo Agosti 4, na kuiamuru polisi kuchukua hatua za kuzuia upatikanaji wa LinkedIn nchini humo.

Wakati makala haya yanapoandikwa, LinkedIn bado inapatikana kwa watumiaji wengi nchini Urusi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.