Upungufu wa Maeneo ya Wazi Wawalazimisha Watoto wa Mumbai Kucheza Katika Maeneo Machafu

Due to shortage of open space young people resort to play cricket on the streets of Mumbai. Image from Flickr by Mohamed Nanabhay. CC BY 2.0

Kutokana na upungufu wa maeneo ya wazi, vijana wameamua kucheza mpira wa magongo katika mitaa ya Mumbai. Picha kutoka Flickr kwa hisani ya Mohamed Nanabhay. CC BY 2.0

Bandiko hili mwanzo lilitokea kwenye Video Volunteers, ambayo ni jamii ya kimataifa iliyoshinda tuzo katika tasnia ya habari yenye makao yake huko India. Bandiko lililohaririwa limechapishwa hapo chini kama sehemu ya makubaliano ya kushirikishana habari.

Mumbai ni mji wenye wakazi wengi nchini India na inakadiriwa kuwa na wakazi wapatao milioni 18.4. Kwa asili eneo hili ni muunganiko wa visiwa saba, lakini mji umekuja kuwa na muundo endelevu wa sasa kutokana na mradi wa maboresho ya ardhi oevu kwa ajili ya matumizi uliofanyika katikati ya karne ya 18. Ukiwa ni mji wa masuala yafedha, biashara na starehe nchini India, umekuwa kivutio kwa watu wengi kwa miaka mingi na maeneo yake ya wazi yameanza kujaa sasa. Hata maeneo yake ya akiba yamevamiwa au kukodishwa.

Upungufu wa maeneo ya waz katika mitaa ya Mumbai inawaathiri watoto wanaotamani kukimbia, kucheza na kufurahi. Kuna vituo vya michezo vinavyokodisha maeneo na vifaa vya michezo kwa ada , lakini ni idadi ndogo sana ya watu wanaoweza kumudu gharama hizo hivyo kuwaacha walio wengi wakiwa bado na uhitaji. Upungufu huu wa meneo ya wazi umewasukuma vijana wa India kutafuta maeneo ya kucheza ambayo sio salama sana kwao, kama huko mitaani.

Amol Lalzare, ambaye ni mwandishi wa habari wa jamii ya Mumbai akishirikiana na Video Volunteers, amekuwa wakili wa kutengeneza maeneo kwa ajili ya watoto kucheza katika mitaa yenye makazi duni ya huko Mumbai kwa zaidi ya miaka kumi sasa. Ametuletea He brings us a ripoti ya video ikionesha jinsi watoto katika mitaa duni ya Mankhurd huko Mumbai wakipambana kucheza.

Dinesh, mwenye miaka 10, na marafiki zake hucheza mpira wa magongo katika maeneo yaliyozungukwa na majirani wanaojisaidia ovyo, vijana walevi, vigae vya vioo vilivyozagaa na uchafu mwingine. Walificha wazazi wao hali ya “eneo lao la kuchezea”. ” Hatuwaelezi wazazi wetu kuwa huwa tunacheza hapa.” Huwa wanadhani kuwa tunaenda kwenye maeneo rasmi ya kuchezea. Kama watagundua kuwa huwa tunacheza hapa, hawataturuhusu tena kwenda kucheza.” Dinesh alimweleza Amol.

Watoto hucheza mahali ambapo wanaweza kukutana na uonevu, kuumia na hata katika matukio mabaya kama vile kudhalilishwa kijinsia. Upungufu wa maeneo ya wazi kipekee inatengeneza kikwazo kwa wasichana maana usalama wao ni jambo la msingi sana kwa wazazi, kama video ya Amol inavyoonesha. Utafiti wa hivi karibu uliofanywa na Pukar, shirika lisilo la Kiserikali la huko Mumbai, unasema kuwa upungufu wa nafasi unawalazimisha wasicha kuacha kucheza watimizapo miaka 12. Ukilinganisha na wavulana ambao hucheza hadi wakiwa na miaka 20.

“Haijalishi ni aina gani ya michezo, ila kucheza ni sehemu muhimu sana katika maisha yetu,” Amol alisema katika tarifa hiyo ya video. ” Watoto wa maeneo ya jirani na kwangu wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kutafuta eneo salama la kucheza na ninakusudia kubadili hali hiyo kwa ajli ya watoto hao.”

Kwanini viwanja ni muhimu kwa watoto

Kutokana na kupungua kwa maeneo ya wazi katika mitaa, hasa viwanja vya kucheza, ni kawaida sana kuwaona watoto wakicheza katika barabara zenye magari mengi na sehemu nyingine kama hizo.

“Tarakimu tofauti zinaonesha kuwa uwiano wa maeneo ya wazi kwa mji wa Mumbai ni wa chini sana ukilinganisha na maeneo ya miji mikuu mingine ulimwenguni, na hasa kama mbuga za wanyama na mikondo ya mikoko haikujumuishwa katika maeneo ya wazi” alisema mwandishi wa masuala ya asilia Sunjoy Monga.

Ukilinganisha na miji mingine mikubwa kama vile New York na Singapore, Mumbai ina upungufu mkubwa wa bustani na viwanja vya kuchezea. Kwa tathimini iliyofanywa 2012 na Initiative Open Mumbai  ilionesha uwiano wa kutisha wa hekta 0.03 ya eneo la wazi kwa kila watu 1,000 — ikiwa ni tofauti kubwa na ile ya mji wa London ambayo ni kwa hekta 12, New York hekta 4 na Singapore ni hekta 6 kwa watu 1,000.

Mahakama kuu ya Mumbai, katika hukumu ya eneo la viwanda mwaka 2005, ilibainisha kuwa watoto wa mjini wanaweza kuzaliwa na mapungufu ya kiakili na kimwili kama kiwango cha oksijeni kitapungua kutokana na ukosefu wa maeneo ya wazi na maeneo ya burudani.

Kwa eneo hili, Amol anataka watoto wa Makhurd wawe na eneo salama kwa kucheza, kukimbia na kuwa huru kama vil watoto wanavyopaswa kuwa na ametuma maombi kwa mwakilishi wa eneo husika.

Waandishi wa jumuiya ya Video Volunteers’ wametokea katika jamii duni huko India na huzalisha video kwa ajili ya habari ambazo hazijaripotiwa. Habari hizi ni “habari kutoka kwa walioziishi”. Hutoa habari katika mazingira halisi ili kufikisha changamoto za maendeleo na Haki za Binadamu.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.