Taarifa Zaonesha Jinsi Wanasiasa wa Ghana Wanavyotumia Mitandao ya Kijamii Kuelekea Kwenye Uchaguzi

Ukurasa wa mbele wa ripoti.

Ukurasa wa mbele wa ya Ripoti ya Kuonesha Utawala na Mitandao ya Kijamii.

Penplusbytes wametoa toleo la pili la ripoti ya Kuonesha Utawala na Mitandao ya Kijamii (Governance Social Media Index (GSMI)), ambayo imepima na kupangilia uwepo wa vyama vya siasa, viongozi wa vyama vya siasa na mamlaka kuu zinazosimamia vyombo vya uchaguzi nchini Ghana katika mitandao ya kijamii ukiegemea hasa kwa wafuasi wao na kiwango cha kujihusisha na mitandao ya Facebook na Twitter.

Kwa ujumla, taarifa inaonesha kuwa watendaji wa vyama vya siasa nchini Ghana wameongeza matumizi ya mitandao ya Kijamii hasa wakati wanaelekea katika uchaguzi mkuu wa 2016.

Mlolongo wa mitandao ya kijamii inayojihusisha na masuala ya kisiasa sio kwamba hautambuliki, ulikuwepo hata kabla ya taarifa hii yabPenplusbyte. Inspekta Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Ghana John Kudalor hapo Mei 2016 aliwahi kugusia kuwa mamlaka za Ghana zinaweza kufikiria kufungia majukwaa ya Mitandao ya Kijamii katika kipindi cha uchaguzi mkuu hapo Disemba 7 “ili kutunza amani”.

Kufuatia kuibuka kwa mjadala miongoni mwa wadau wakuu baada ya kauli yake, Rais wa Ghana John Dramani Mahama alitangaza hapo Agosti 14 kuwa “serikali haina mpango wa kufunga mitandao ya kijamii katika siku ya uchaguzi.”

Penplusbytes ni shirika lisilo la kiserikali linalohamasisha utawala bora kwa kutumia teknolojia Barani Afrika. Malengo ya Shirika ni kuleta mabadiliko katika maeneo makuu matatu: kutumia teknolojia mpya ya kompyuta kuwezesha utawala bora na uwajibikaji, vifaa vipya na ubunifu, na kuendesha na kusimamia kwa ufanisi matumizi ya mapato ya migodi, mafuta na gesi na maliasili.

Utawala na Mitandao ya Kijamii imefuatilia umuhimu na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii katika Utawala. Taarifa ya kwanza ilichapishwa Juni 2016.

Toleo la pili la ripoti hiyo liliandikwa baada ya wagombea 13 wa Urais kuhenguliwa kutoka katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu na Tume ya Uchaguzi ya Ghana. Wagombea hao walijumuishwa katika taarifa hiyo kwa sababu walikuwa sehemu ya ripoti ya awali ya GSMI.

Ripoti inaonesha kuwa Rais Mahama yuko mbele ya wagombea wengine katika mtandao wa Facebook akiwa na wafuasi 1,007,595 ambao ni 125,171 zaidi ambapo mwezi Juni alikuwa na wafuasi 880,620. Nana Akufo-Addo, ambaye ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, anashika nafasi ya pili kwa kuwa na wafuasi 981,057 Facebook, ambapo ni ongezeko la wafuasi 265,341.

Ukija katika mtandao wa Twitter, ripoti inaonesha kuwa Akufo Addo ametumia fursa vizuri kwa kutumia jukwaa hilo kuwasiliana na wafuasi wake na ushahidi ni mabandiko yapatayo 4,000 ukilinganisha na mabandiko 842 ya Rais Mahama.

Kwa vyama vya siasa, Chama Cha Wazalendo Wapya kinaendelea kuongoza kwa kuvunja rekodi ya kuwa na wafuasi 307,963 katika mtandao wa Facebook. Kisha kinafuata Chama cha Maendeleo ya Watu kikiwa na wafuasi 33,193, ambacho kimekishinda chama tawala ambacho kina wafuasi 24,743 Facebook.

Mapema mwaka huu, Penblusbytes walitoa taarifa kuhusu Utawala na Mitandao ya Kijamii (SMI) katika machapisho, redio na katika vituo vya runinga.

Pakua taarifa nzima ya kuhusu Utawala na Mitandao ya Kijamii hapa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.