Sri Lanka Yaingia Hasara Kufidia Gharama za Matumizi Mabaya ya Serikali

SriLankan Airlines - Airbus A330-243, 4R-ALG touches the runway at London Heathrow. Image from Flickr by Michael Garnett. CC BY-NC 2.0

Ndege ya Shirika la ndege la SriLanka – Airbus A330-243, 4R-ALG ikipaa kwenye uwanja wa ndege wa London Heathrow. Picha kutoka Mtandao wa Flickr na Michael Garnett. CC BY-NC 2.0

Makala haya yalionekana mara ya kwanza kwenye Groundviews, tovuti iliyoshinda tuzo ya uandishi wa habari za kiraia nchini Sri Lanka. Habari hii iliyohaririwa imechapishwa hapa chini kama sehemu ya makubaliano ya kushirikiana kwa maudhui.

Hivi karibuni Sri Lanka ilitangaza kuwa italipa deni linalofikia Dola za Marekani Milioni 170 kwa kampuni inayotengeneza na kukodisha ndege AerCap Holdings, kama gharama za kuvunja mkataba wa kununua ndege nne aina ya Airbus A350, ambazo ziliagizwa na serikali ya Rais Rajapaksa wa nchi hiyo mwaka 2013.

Hatua hiyo ambayo maafisa wa serikali wanasema ni sehemu ya mpango wa marekebisho, Sri Lanka iliamua kusitisha bajeti ya ndege ya Mihin Lanka.

SriLankan Airlines imekuwa na madeni mengi kwa miaka hivi karibuni. Mara ya mwisho kampuni hiyo kuripotiwa kupata faida ni mwaka 2009, mwaka mmoja baada ya Emirates kuuza hisa zake za shirika hilo. Siku za hivi karibuni, shirika hilo liliripoti hasara ya Rupia. 16.33 bilioni (Dola za Kimarekani milioni 112) kwa mwaka huo.

Groundviews imetengeneza habari ya picha kuonesha namna gani serikali ingeweza kutumia fedha zilizotumika kufuta mpango wa kununua ndege nne.

Takwimu zilizopatikana kupitia ripoti ya mwaka 2015 ya Wizara ya Fedha.

Infographic by Groundviews.

Habari picha na Groundviews. 1 LKR = 0.00683338 USD

Rupia bilioni 25 ni kiasi kikubwa cha fedha, na tangazo hilo lilipokelewa kwa hasira zinazolingana na kiasi hicho kwenye mitandao ya kijamii:

Shirika letu la Ndege limefuta mpango wake wa kununua ndege aina ya A350, mpango unaogharimu faini ya Dola Milioni 98. Tunapoteza pesa zote bila sababu

Kama inavyoonekana kwenye habari picha hiyo, pesa hizo zimetumika kufuta mkataba wa kutengenezewa ndege hizo na kampuni ya Airbuses abazo zingetumiwa kulipia mafao ya uzeeni, malipo ya Samurdhi (ustawi wa jamii), madawa, au vifaa vya shule. Shirika la ndege la SriLankan limehangaika na deni hilo kwa miaka mingi (wakaguzi wa mahesabu walitahadharisha kuwa lingeongezeka tangu mwaka 2009), lakini serikali iliendelea na mpango wake wa kununua ndege hizo, hatua iliyokuza hasara ambayo tayari ilishapatikana.

Sasa, Sri Lanka italazimika kulipa gharama hiyo – kwa mamilioni ya dola za kimarekani.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.