Huduma zote za intaneti kwenye simu za mkononi zimezimwa nchini Ethiopia kwa siku saba sasa, wakati matukio ya ghasia za maandamano yakiendelea sambamba na “hali ya hatari” iliyotangazwa hivi karibuni.
Maandamano yamekuwa yakifanyika mara kwa mara kwenye majimbo ya Oromia tangu Novemba 2015, kufuatia madai ya kutaka kujitawala, kupata uhuru na kuheshimiwa kwa watu wa kabila la Oromo, ambao wamekuwa wakidaiwa kubaguliwa na kuteswa na mfumo wa serikali kwa zaidi ya robo karne iliyopita. Vyombo vya dola vimetumia nguvu kupita kiasi katika kujaribu kupambana na waandamanaji kwa zaidi ya tukio moja. Mnamo Oktoba 2 pekee, watu 52 waliuawa. Chama cha upinzani cha Oromo Federalist Congress (OFC), kimeripoti idadi ya vifo vinavyofikia watu 600.
Wakati baadhi ya mitandao ya kijamii ikifungwa kama vile WhatsApp kadri maandamano yanavyoendelea kushika kasi, jijini Addis Ababa, ambao ni mji mkuu, hili ndilo tukio refu zaidi ya kuzimwa kwa huduma za mtandao wa Intaneti kuwahi kutokea nchini humo.
Kunyamazishwa ghafla kwa waandamanaji kwenye mitandao ya kijamii kumewafanywa wale wanaofuatilia habari za maandamano hayo kwenye mtandao wa Facebook na Twitter kupatwa na wasiwasi.
Mobile internet, social media cut for +7 days in the “African capital” #AddisAbaba. Gov spox says service will be back “when deemed safe”…
— Karim Lebhour (@KaLebhour) October 11, 2016
Inteneti ya simu, mitandao ya kijamii imekatwa kwenye zaidi ya siku saba kwenye jiji hili la ki-Afrika
Kuzimwa kwa intenti ya simu za mkononi kunaweza kusababisha kupungua kwa habari zinazohusu maandamano hayo kwenye mitandaoani. Wanaharakati wanawasi kuwa maandamano hayo, ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakitegemea mitandao ya kijamii katika uratibu wake na kusambaza ujumbe kwenda kwa wafuatiliaji wa kimataifa, yataathirika sana kwa kukosekana kwa njia kuu ya mawasiliano. Ingawa si maeneo mengi yameunganishwa na mtandao wa intaneti, mitandao ya kijamii imekuwa muhimu sana -hasa kwa ajili ya maandamano yanayofanyika kwenye majimbo ya Oromia na Amhara. Habari zinazopatikana kwenye kurasa za Facebook na Twita hazioneshi kuwepo kwa machapisho mengi kama ilivyokuwa juma lililopita.
Namna #Ethiopia inavyofuatilia Facebook. Huku kukiwa na hali ya hatari iliyotangazwa hivi karibuni, tegemea vitendo zaidi vya #kuzimwa kwa intaneti na #ufuatiliwaji wa matumizi yake. #KeepItOn pic.twitter.com/pD2laTPzpF
— Moses Karanja (@Mose_Karanja) October 9, 2016
Namna #Ethiopia inavyofuatilia Facebook. Huku kukiwa na hali ya hatari iliyotangazwa hivi karibuni, tegemea vitendo zaidi vya #kuzimwa kwa intaneti na ufuatiliwaji wa matumizi yake
Serikali imekuwa ikikata mtandao wa intaneti na kuzuia mitandao ya kijamii kwenye maeneo ya Oromia na Amhara kwa zaidi ya miezi 12. Mwezi Juni serikali ilizima mitandao ya kijamii kwa madai ya kuzuia vitendo vya wizi wa mitihani, lakini hivi sasa haieleweki ikiwa serikali itazima huduma zote za simu za mikononi kuzuia maandamano yanayoendelea, au kama hatua hiyo inalenga kudhibiti maandamano hayo. Wale wanaoufuatilia mwenendo wa mambo wanahofia kuwa hatua hii inaweza kuwa dalili ya mwanzo mbaya kwa maandamano hayo yaliyoendelea kwa miezi 12.