Katika ziara ya Kiofisi huko Ujerumani wiki iliyopita, Rais wa Naijeria Muhammadu Buhari alitoa maoni ya ubaguzi wa kijinsia kuhusu mke wake Aisha Buhari, akisema, “Sijui mke wangu ni wa chama kipi, lakini ni wa jikoni kwangu, sebuleni kwangu na vyumba vingine nyumbani kwangu.” Maoni hayo yalitolewa katika mkutano wa habari uliohudhuriwa na Buhari na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.
Katika mahojiano ya hivi karibuni na BBC, Aisha Buhari alikosoa uongozi wa mumewe na teuzi zake, na alisema anaweza asimuunge mumewe mkono kama atarudia kugombea.
“Rais hafahamu watu 45 kati ya 50 alioteua nami siwafahamu pia pamoja na kuwa mkewe kwa miaka 27, alisema. “Bado hajaniambia kama mkewe, lakini nimeamua kuwa, kama mambo yataendelea hivi mpaka 2019, sitatoka na kwenda kumpigia kampeni na kumwambia mwanamke mwingine ampigie kura kama nilivyofanya hapo kabla. Sitafanya hivyo tena.”
Garba Shehu, msemaji wa Rais alijaribu kutuliza maji baadaye kwa kusema ulikuwa ni mzaha mdogo tu wa Rais Buhari:
Marafiki zangu, kiongozi hawezi kuwa na mzaha tena? Rais alicheka kabla hajatoa kauli ile.
— Garba Shehu (@GarShehu) Oktoba 14, 2016
Marafiki zangu, kiongozi hawezi kuwa na mzaha tena? Rais alicheka kabla hajatoa kauli ile.
Hata hivyo, watumiaji wengi wa mtandao wa intaneti huko Naijeria, walibaki na wasiwasi.
Kola Tubosun, mtaalamu wa lugha, yeye kwa ujumla hakushawishika:
@GarShehu Hahahhaha-Wewe ni mpumbavu-hahahahaha.
— Kọ́lá Túbọ̀sún (@baroka) October 14, 2016
Hahahhaha-Wewe ni mpumbavu-hahahahaha.
Yomi alisema kuwa mzaha huu unachochea ubaguzi wa kijinsia:
Haki za kijinsia bado ni jambo kubwa hapa Naijeria. Maoni ya Rais yalikuwa ya hatari na yanachochea ubaguzi mbaya sana wa kijinsia. Mzaha gani huo?
— Yomi Kazeem (@TheYomiKazeem) Oktoba 15, 2016
Haki za kijinsia bado ni jambo kubwa hapa Naijeria. Maoni ya Rais yalikuwa ya hatari na yanachochea ubaguzi mbaya sana wa kijinsia. Mzaha gani huo?
Jina la mgombea wa Urais wa Marekani kwa tiketi ya Republican, Donald Trump lilijitokeza sana kwa sababu ya ufunuo wa hivi karibuni kuhusu maoni yake ya hapo zamani ya ubaguzi wa kijinsia.
Kama umemkinai Trump, huyu hapa kiongozi wa SASA wa dunia ambaye anasema sehemu ya mke wake ni jikoni #sexism #Naijeria https://t.co/EDDos3bdni
— Sophie Garratt (@SophGarratt) Oktoba 14, 2016
Kama umemkinai Trump, huyu hapa kiongozi wa SASA wa dunia ambaye anasema sehemu ya mke wake ni jikoni
Gazeti la mtandaoni la YNaija lilichapisha maoni ya ushambulizi:
Zaidi ya mawazo hayo ya kibaguzi na kinafiki, lipo jambo la kutisha zaidi lililotanda kichwani mwake katika aina fulani ya upuuzi unaofana na ule wa siasa zinazofanywa na Donald Trump za ‘wakwapue kwa kutumia nye_* zao’.
Rais kwa kujaribu kumnyamazisha na hata kumdhalilisha mke wake, anasema hivi: ni wa jikoni na sebuleni kwangu na vyumba vingine.”
Wakati Wanaijeria wanajaribu kuendana na mkasa huu kwa kucheka badala ya kulia wamegeuza #ChumbaKingine kuwahashtagi maarufu, kila mtu mzima mwenye akili timamu anajua kabisa ni chumba gani ambacho Rais wa Naijeria alikuwa anakizungumzia, alidhani anatoa mzaha wa “chumba cha kufungia”: chumba cha kulala. Mara zote tumekuwa tukihisi kuwa Rais wetu ni wa kufuka, sio wa kisasa na huenda hana uwezo wa kuchuja na kutenganisha hisia tata na taarifa. Lakini ni nani angeweza kudhania kuwa kutoka kwenye msingi wake – mwanaume huyu anayejiweka kama ishara ya mamlaka, mwenye kujichunguza na mwenye nidhamu binafsi- mbaya?
Emeka anasema kuwa maoni hayo ni ya Rais tu na hayawakilishi mawazo ya wanaume wote wa Naijeria:
Kwako Angela Merkel, mtazamo wa Buhari juu ya mke wake hauwakilishi ule wa wanaume wa Naijeria. Yuko mwenyewe katika hilo.
— EMEKA (@EmekaEmezue) Oktoba 14, 2016
Kwako Angela Merkel, mtazamo wa Buhari juu ya mke wake hauwakilishi ule wa wanaume wa Naijeria. Yuko mwenyewe katika hilo.
Wanamitandao wengine walikataa, na kusema kuwa maoni na mtazamo wa Buhari unawawakilisha wanaume wengi wa Naijeria:
Katika hili #Naijeria ambapo wanaume wazee wanaoa wasichana wa miaka 14 na wake zao sehemu yao ni jikoni, je Trump hawezi kushinda uchaguzi ndani ya pigo moja la moyo?
— Femke van Zeijl (@femkevanzeijl) Oktoba 14, 2016
Katika hili #Naijeria ambapo wanaume wazee wanaoa wasichana wa miaka 14 na wake zao sehemu yao ni jikoni, je Trump hawezi kushinda uchaguzi ndani ya pigo moja la moyo?
Mwangwi wa maoni ya Femke ulirudiwa na Amara Nwankpa:
Usisahau kuwa kuna watu mashuhuri ndani ya nchi ambao bado wanaamini kuwa msichana mwenye miaka 14 sehemu yake ni #ChumbaKingine.
— Amara Nwankpa (@Nwankpa_A) Oktoba 14, 2016
Usisahau kuwa kuna watu mashuhuri ndani ya nchi ambao bado wanaamini kuwa msichana mwenye miaka 14 sehemu yake ni #ChumbaKingine.
Hivi karibuni, kiongozi wa mila huko Kaskazini-Mashariki mwa Naijeria “alimuoa” msichana wa miaka 14.
Rita alielezea hisia zake kuhusu RMB (Rais Muhammadu Buhari):
RMB ameharibu? Ndio Yeyote anaweza udhika? Sina hakika. Mtu gani aliweka amplifaya na vioo vya kukuzia kwenye fikra za wanaume wengi wa Kinaijeria?
— Rita C. Onwurah (@RitaOnwurah) Oktoba 15, 2016
RMB ameharibu? Ndio Yeyote anaweza udhika? Sina hakika. Mtu gani aliweka amplifaya na vioo vya kukuzia kwenye fikra za wanaume wengi wa Kinaijeria?
Somi Ekhasomhi anasema kuwa lazima Rais awajibishwe kwa maoni yake, kuliko kutumia visababu kuteta wengine:
Ninaona watu wasiotaka kumkosoa Buhari. Badala yake wanamtumia kama njia ya kuwafikia “wanaume wote wa Naijeria.”
— Somi (@SomiEkhasomhi) Oktoba 14, 2016
Ninaona watu wasiotaka kumkosoa Buhari. Badala yake wanamtumia kama njia ya kuwafikia “wanaume wote wa Naijeria”
Pia kulikuwa na mizaha ya kutosha, kwa kweli:
Mke wa Osibanjo: Yemi, sehemu yangu mimi ni wapi?
PYO: Hapa, pembeni yangu mpenzi. pic.twitter.com/5Rl7mJJxVX
— S. (@smugdisguise) Oktoba 14, 2016
Mke wa Osibanjo: Yemi, sehemu yangu mimi ni wapi?
PYO: Hapa, pembeni yangu mpenzi.
(PYO ni Profesa Yemi Osibanjo, Makamu wa Rais wa Naijeria.)
Mtumiaji mwingine wa Twita aliyejiita Atiku (Abubakar), Makamu wa Rais wa zamani wa Naijeria anaandika:
Kesho tarajia bandiko huko twita kutoka kwa Atiku akiwa jikoni amevaa aproni akituambia kati ya vitu anavyopenda ni pamoja na kupika mchele wa Jollof. 😭😭😭
— Óga (@BrownKaftan) Oktoba 14, 2016
Kesho tarajia bandiko huko twita kutoka kwa Atiku akiwa jikoni amevaa aproni akituambia kati ya vitu anavyopenda ni pamoja na kupika mchele wa Jollof.
Sam Hart anasema anajutia kuwa maoni ya kibaguzi dhidi ya wanawake yatafunika faida halisi ya kutembelea Ujerumani:
Kitu cha kusikitisha stori hii itafunika chochote alichoendea huko. https://t.co/jUsZEAWM3n
— Sam Hart (@hartng) Oktoba 14, 2016
Kitu cha kusikitisha stori hii itafunika chochote alichoendea huko.
Wakati huo huo Rais Buhari amekataa kuomba radhi:
VIDEO | Buhari akizidi kushindilia, akisisitiza kuwa mkewe Aisha sehemu yake ni jikoni pic.twitter.com/20kj7FGUdf
— SIGNAL (@thesignalng) Oktoba 16,, 2016
VIDEO | Buhari akizidi kushindilia, akisisitiza kuwa mkewe Aisha sehemu yake ni jikoni
Gazeti la YNaija linaliita jambo hili lote ni “lakutisha kweli”:
Mwandishi wa habari wa Deutsche Welle ya Ujerumani alimpa nafasi, na kama hatukumsikia vizuri hapo Ijumaa, Buhari alijibu kuwa jikoni na sebuleni ni majukumu ya mwanamke hata kama ana kazi- akielekeza kwa kusema kuwa kazi ya Aisha Buhari ni kumwangalia.
Hakujaribu hata kupotezea maoni yake kwa kusema ni jaribio la mzaha kidogo, hata hivyo labda ndio maana ushauri wa vyombo vyake vya habari ulishambuliwa vibaya. Alifikiri hatauhitaji. Kwa sababu anaamini kuwa yeye ni mwerevu kuliko wote, ni sawa.
Kwa kuthibitisha maoni yake ya mwanzo, Muhammadu Buhari ameonesha kuwa anafanana na mgombea wa urais wa Marekani mwenye ubaguzi wa wazi dhidi ya wanawake Donald Trump. Na hakika hili linaogopesha.