Picha za Mtandao wa Instagram Zaonesha Ukungu Unavyoifunika Khabarovsk

Source: Instagram. Catherine Afanasyeva (@kazhetsyatak)

Chanzo: Mtandao wa Instagram. Catherine Afanasyeva (@kazhetsyatak)

Wakazi wa Khabarovsk, mji ulioko Mashariki ya Mbali nchini Urusi, wamekuwa wakikaa ndani au kulazimika kuficha nyuso zao wanapokwenda nje tangu ukungu mzito kuufunika mji wao tangu Jumanne. Kwa mujibu wa habari za tovuti ya 2×2.su (.su ni anuani ya utambulisho unayotumiwa na Urusi), wenyeji wanasema ukungu huo umekwenda sambamba na harufu mbaya na iliongezeka katika siku mbili zilizopita moto ulipolipuka mjini humo na hata kwenye maeneo ya jirani. Maarifa wa Urusi wanachunguza kiwango cha hewa ya ukaa (carbon monoxide), ambacho kimeongezekan mara 1.5 zaidi tangu ukungu huo utande.

Moshi ulianza kutanda kwenye mji wa Khabarovsk takribani majuma mawili yaliyopita na unaonekana kuanzia kwenye mpaka wa nchi hiyo na China kwenye jimbo la Heilongjiang na Jamhuri huru ya Kiyahudi, ambao ni sehemu ya Urusi karibu na Khabarovsk. Maafisa wa Khabarovsk walisema kuwa moto katika eneo la Heilongjiang ndio sababu ya moshi huo, na walituma barua kwendakwa Idara ya Ulinzi wa Mazingira ya Heilongjiang kuziomba mamlaka za eneo hilo kudhibiti hali hiyo na kuchukua hatua za kuzuia matukio ya moto kwa siku zijazo. Mamalaka za Heilongjiang zilikanusha madai ya maafisa wa Urusi, na kuimbia Global Times leo kuwa wakulima wa jimbo hilo walikuwa hawajaanza kuvuna mazao au kuchoma mabua -na hawataanza kufanya shughuli hizo mpaka mapema mwezi Novemba kwa sababu ya hali mbaya ya hewa katika siku za hivi karibuni.

Picha ya sertilaiti kutoka “Fire Map,”(tovuti ya Urusi inayoonesha maeneo yenye moto duniani kote) inaonesha, moshi ulipoanza mjini Khabarovsk majuma mawili yaliyopita, kulikuwa na matukio ya moto kwenye eneo la Heilongjiang na hata kwenye Jamhuri Huru ya Kiyahudi:

Source: http://fires.kosmosnimki.ru/.

Picha ya Satilaiti inayoonesha matukio ya moto mnamo Oktoba 14. Chanzo: http://fires.kosmosnimki.ru/.

Wakati maafisa wa Heilongjiang wakijibu tuhuma hizo leo, hata hivyo, moto ulikuwa katika maeneo karibu yote ya kaskazini na magharibi mwa Khabarovsk:

Picha ya Satilaiti inayoonesha matukio ya moto mnamo Oktoba 27. Chanzo: http://fires.kosmosnimki.ru/.

Wakati majibizano yakiendelea kati ya maafisa wa serikali wa maeneo hayo, mtumiaji wa mtandao wa Instagram unimat093 alitania kuwa alikuwa amegundua nani hasa anahusika na matukio hayo ya moto, kwa kuweka picha ya moshi ukianzia kwenye bomba la kutolea moshi mjini Khabarovsk.

A photo posted by @unimat093 on

Kwazaidi ya majuma mawili, watuamiaji wa Instagram wamekuwa wakiweka picha za Khabarovsk kadri moshi ulivyokuja na kuondoka; picha hizo zinasaidia kuwa kama Tarifa ya Instagram kuhusiana na tukio hilo:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.