Matangazo ya ‘Kwa Kina': Kura ya Hapana kwa Amani ya Colombia

Matangazo ya ‘Kwa Kina’ ni matangazo mapya ya Global Voices yanayochimba kwa kina masuala ambayo hayapewi uzito kwenye vyombo vya habari.

Katika kipindi cha wiki hii, tunawasikiliza waandishi wetu wa Global Voices Robert Valencia na Andrés Lombana-Bermudez pamoja na mtetezi wa amani Diego Osorio kuhusu sababu za kupigwa kwa kura ya hapana katika kura ya maoni iliyokusudia kuidhinisha makubaliano ya amani kati ya serikali ya Columbia na kikundi cha waasi kiitwacho FARC, matokeo ambayo yangehitimisha zaidi ya miaka hamsini ya vita.

Katika kipindi hiki, tunasindikizwa na muziki wenye haki miliki ya Creative Commons kutoka maktaba ya Free Music na Blue Dot Sessions, ikiwa ni pamoja na Ray Gun – FasterFasterBrighter na Denzel Sprak, na We Are; wa A Ninja Slob Drew Me.

Picha inayopambia habari hii imepigwa na Manuel Chacón/Agencia Prensa Rural na imechapishwa kwa idhini ya leseni ya CC BY-NC-ND 2.0. Maandishi yanasomeka, “Watu. Vifo vingapi zaidi?”

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.