Kashfa Nyingine Yalikumba Kanisa la Orthodox la Nchini Urusi Kufuatia Kasisi Kuonekana na Saa Yenye Thamani ya $40,000

Image: Askofu wa Kanisa la St. Petersburg

Picha: Dayosisi ya St. Petersburg

Kanisa la Orthodox la nchini Urusi limekumbwa na kashfa kwa mara nyingine, kashfa inayohusishwa na saa ya mkononi ya mmoja wa Makasisi waandamizi wa St. Petersburg, ambapo hivi karibuni Dayoyisisi hiyo ilichapisha picha zilizochukuliwa katika moja ya safari za Kiaskofu za Varsonofiya alipokuwa akielekea Ugiriki. Katika moja ya picha katika matukio yake ya furaha, waandishi wa habari, waligundua kile kilichoonekana kuwa ni saa ya mkononi aina ya Rolex Daytona 116509 — yenye thamani inayokadiriwa kuwa fedha za Kirusi milioni 2.5 sawa na $40,000.

Varsonofiya alisafiri hadi Mt. Athos mnamo Oktoba 23, ambapo alikutana na Mkuu mpya wa Watawa katika nyumba ya watawa iliyopo karibu na Kanisa la Kirusi la Orthodox.

Kwa mujibu wa maelezo ya Varsonofiya, alimpongeza mkuu huyo wa Watawa kwa kuchaguliwa katika nafasi hiyo kwa kumzawadia msalaba mtakatifu. Ili kuweka kumbumbukumbu nzuri ya haafla hiyo, kanisa lilitoa picha kadhaa za mkutano huo, ikiwa ni pamoja na picha moja iliyoonesha kile kinachosadikiwa kuwa ni saa ya mkononi ya Varsonofiya inayoaminika kuwa ni ghali sana.

Rolex ilitambulisha toleo lake aina ya Cosmograph Daytona la mwaka 1963, iliyobuniwa mahususi kwa ajili ya “kukidhi mahistaji ya wakimbiaji wa kulipwa.” Mtengenezaji wa simu wa huko St. Petersburg anasemekana kuliambia shirika la habari la Fontanka kuwa saa ya mkononi aina Rolex Daytona 116509 inaweza kununuliwa katika maduka bubu ya Urusi kwa takribani Euro 25,000.

Mamlaka ya Habari ya Dayosisi ya St. Petersburg inasema kuwa Varsonofiya bado yupo Ugiriki na kwamba maelezo ya kina kuhusu saa yake yatatolewa kwa waandishi wa habari mara baaada ya Varsonofiya kurejea nchini Urusi.

Kumekuwepo na sintofahamu kama hii miaka minne iliyopita, pale watumiaji wa mtandao wa intaneti walipogundua kuwa Kanisa la Orthodox la Urusi lilihariri picha za Askofu Kirill kwa lengo la kuficha saa ya mkononi aina ya Brequet yenye thamani ya dola za kimarekani 30,000 to conceal his $30,000. Bahati mbaya kwa kanisa, wahariri wao wa picha walisahau kuondoa taswira ya saa hiyo iliyotokana na sehemu ya juu ya meza.

Katika wakati fulani, kanisa lilikanusha habari hiyo, hata hivyo, baaadae lilikuja kamlaumu “mfanyakazi wao ambaye hakuwa na uzoefu.”

Image: Patriarchia.ru

Picha: Patriarchia.ru

Tofauti na Makasisi wa Urusi, msemaji mkuu wa zamani wa Vladimir Putin, Outside Russia's clergy, ndugu Dmitry Peskov, alijikuta katikati ya tuhuma ya kisiasa mNmo Agosti 25 pale wanaharakati dhidi ya rushwa walipogundua kupitia picha za siku aliyofunga ndoa kuwa alikuwa amevaa saa ya mkononi aina ya Richard Mille RM 52-01 yenye thamani ya dola za Kimarekani 620,000. Peskov alidai kuwa saa ile alipewa kama zawadi kutoka kwenye mahari na kusisitiza kuwa ilikuwa na thamani ya dola za Kimarekani 3,500 tu, hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa yeye kuonekana katika picha akiwa amevaa saahiyo.

Habari imekuwa miongoni mwa mojawapo na habari kubwa ya kuweka mambo hadharani iliyoandaliwa na mwanaharakati Alexey Navalny kuhusu utajiri mkubwa wa watu wa karibu kabisa wa Vladimir Putin. Navalny ameendelea kuchapisha habari za kiuchunguzi kama hizo kwa takribani mwaka mmoja sasa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.