Yaliyojiri Wiki Hii Hapa Global Voices: Sisi, Raia

Matangazo ya yaliyojiri wiki hii hapa Global Voices yanaangazia baadhi ya habari kubwa zilizojitokeza kwenye habari zetu za Global Voices. Wiki hii tunaongea na our contributors Elizabeth Rivera, Giovanna Salazar pamoja na Juan Tadeo kuhusu hali ya kutokuridhishwa na mwenendo wa mambo nchini Mexico.

Tunakupeleka Colombia, India, Syria na Marekani, ambako tunakutana na watu wazima na watoto wenye ari ya kuleta tofauti.

Shukrani nyingi kwa Joey AyoubGabriela García Calderón, Tori EghermanPalash Ranjan Sanyal, na waandishi wetu wote, watafsiri na wahariri waliotusaidia kufanya kipindi hiki kikujie.

Katika kipindi hiki, tunasindikizwa na muziki wenye haki miliki ya Creative Commons kutoka maktaba ya Free Music, ikiwa ni pamoja na Please Listen Carefully wa JahzzarFirst steps on earth wa David Skeztay; Backward wa David Szesztay; Making A Change wa Lee Rosevere; Breezin wa Podington Bear; Indian Summer wa Zero V; na Cree wa Satellite Ensemble.

Picha inayopamba habari hii imetoka kwenyeukurasa wa Facebook wa Pedro Kumamoto na inasema “No nos soltemos, los muros sí caen” (Hatupuuzi, ukuta utaanguka).

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.