- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mwandishi wa Habari Jean Bigirimana Bado Hajapatikana katikati ya Mgogoro wa Kisiasa Unaoendelea Nchini Burundi

Mada za Habari: Burundi, Censorship, Haki za Binadamu, Maandamano, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Vita na Migogoro, Vyombo na Uandishi wa Habari, GV Utetezi
OU EST JEAN BIGIRIMANA IWACU FRONT PAGE

Ukurasa wa mbele wa Iwacu (n°385, 29/07/2016) unauliza “Jean Yupo Wapi?”

Mwandishi wa habari wa Burundi Jean Bigirimana hajaonekana [1] tangu Julai 22 2016. Vyanzo mbalimbali vimemdokezea mwajiri wake, gazeti lisilo la kiserikali la Iwacu [2], kwamba anashikiliwa na serikali. Hata hivyo, mamlaka za serikali zimekanusha madai haya.

Iwacu, linalowakilisha mhimili mdogo [3] wa hali ngumu inayopitiwa na vyombo vya habari nchini Burundi, wiki iliyopita lilibadilisha muonekano wa tovuti yake na kuwa ya nyeusi na nyeupe kama ishara ya kumuenzi [4] mfanyakazi wao asiyejulikana alipo.

#Ni Jamatatu nyingine mbaya kwa Burundi. Siku mbaya, wiki zisizo na matumaini, mwezi usio na mategemeo kwa familia ya mwandishi wa habari Jean Bigirimana.

Burundi imejikuta katika mzozo wa kisiasa tangu Rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kuwania nafasi ya Urais kwa awamu ya tatu mwaka uliopita, jambo lililozua  maandamano [8] na harakati [9] za kiraia zikidai kuwa kugombea kwake kumepuuza makubalino ya Arusha pamoja na katiba ya Burundi. Mashuhuda [10]wahanga [11], wanaharakati [12] wazawa na mashirika [13] ya haki za binadamu [14] yameripoti matukio kadha wa kadha ya kushikiliwa [15] bila sababu maalumu, unyanyasaji [16] wa kimkakati, na mauaji [17], yanayowalenga wanaharakati, waandishi wa habari pamoja na  wapinzani [18] wa Nkurunziza pamoja na kuwa maafisa wa serikali [19] wamekanusha tuhuma hizi.

Ni dhahiri kuwa tasnia ya vyombo vya habari nchini Burundi imeyaonja machungu ya upinzani wa awamu ya tatu wa kukabiliana [20] nguvu ya jeshi, hususani maeneno ya nje ya jiji la Bujumbura. Waandishi wa habari [21] wa Burundi na wale wa kimataifa [22]  wamekuwa wakikabiliwa na  mashitaka [23] ya kuikosoa serikali au kuhamasisha chuki dhidi ya serikali zinazoambatana na machafuko. Mkurugenzi wa Iwacu Antoine Kaburahe [24] kwa sasa naye anaishi uhamishoni nchini Ubelgiji.

Kabla ya kujiunga na Iwacu, Jean alikuwa akifanya kazi na kituo cha redio cha Rema FM. Iwacu anataarifu kuwa alipowasili Rwanda mwanahabari [25] mwenye Umri wa miaka 37 [25] alishaandika [25] kuhusu maisha ya raia wa Burundi wanaoishi uhamishoni nchi ya jirani. Rwanda na Burundi zina historia ndefu ya migogoro ya kisiasa na kidiplomasia.

Mnamo tarehe 22 Julai 2016, Jean aliondoka nyumbani [25] mara baada ya kupokea simu kutoka kitengo cha usalama wa Taifa. Tangu hapo, hajaonekana tena wala kusikika. Mke wake, Godeberthe alitoa wito [26] kwa hisia kali kuhusu kuachiwa huru kwa mume wake, na pia vyombo vya habari vimeshajaribu kufanya uchunguzi na kusambaza tukio hili kwa kuweka picha [27] nyingi kwenye mitandao ya kijamii.

#Burundi Picha kutoka kwenye kumbukumbu ya heshima ya mwandishi wa habari Jean @iwacuinfo

Iwacu imeapa [4] kuendelea kumtafuta Jean. Waandishi wa habari wa Iwacu walifanyauchunguzi [31] wao binafsi na kisha kuuchapisha kwenye mtandao wa intaneti na kutazamia kufungua mashitaka mahakamani, pamoja na kuwa hatua hii inaweza kushindwa kwa kuchukulia mifano ya matukio ambayo hayakufanyiwa uchunguzi [32] ya vifo na watu kupotea. Shirika linalotetea haki za raia la nchini Burundi,APRODH hivi karibuni lilitaarifu [33] kuwa polisi na vyanzo vya jeshi ambavyo haviungi mkono hali inayoendelea hivi sasa, vimetaarifu kuwa yamepatika makaburi 14 ya mamluki, huku yakidhaniwa kuhusisha miongoni mwa watu wanaosadikiwa kupotea.

Wakati wa upekuzi wao, miili ya raia wawili waliokuwa walioonekana kuteswa ilikutwa na polisi. Mke wa Jean alipoitwa ili kubaini kama mume wake alikuwa ni miongoni, alisema kuwa miongoni mwao, hakuwamo mume wake, hata hivyo, iliripotiwa kuwa miili hiyo ilizikwa bila kuwambuliwa na ndugu zao.

Msemaji wa polisi,Pierre Nkurikiye alithibitisha kuwa miongoni mwa miili miwili iliyokutwa, Jean hakuwamo:

#Taarifa ya Burundi/ Tukiio la Jean BIGIRIMANA (mwandishi wa habari/IWACU): Miili miwili ilitambuliwa: Jean hakuwa miongoni mwao. Mwendesha mashtaka Muramvya ataendelea na ufuatiliaji

Vyanzo vya habari vilionesha kuguswa kuhusu raia siyo tu kuhusu Jean, lakini pia kuhusu miili mingine ambayo kwa namna moja ama nyingine ambayo haijapatikana. Mtumiaji wa Twitter, Thierry Uwamahoro aliuliza:

siku 11 baada ya kupotea kwa Jean, Iwacu ililishutumu [40] jeshi la polisi kwa “ukimya wao wa kishindo” na kuonekana dhahiri kutokuwepo na ufuatiliaji. Iwacu ilijaribu kumfuatilia Jean kupitia kwa Abel Ahishakiye, mtu ambaye Jean aliwasiliana [41] naye kupitia simu kabla ya kupotea kwake, hata hivyo, naye ghafla alipotea.

Mapema mwezi Agosti, wafanyakazi wenzake na Jean walipokea ujumbe ulioonesha [42] kuwa Jean alishikiliwa kwa siri katika jimbo la Muramvya [43]. Msemaji wa polisi, Pierre Nkurikiye alikanusha kuwa Jean alikamatwa, na mapema agusti 5, tume huru ya haki za binadamu ya nchini Burundi(Commission Nationale Indépendante des Droits de l'Homme) ilieleza kuwa haikupata ushahidi wowote kuwa Jean alikuwa kwenye jela ya SNR.

Waandishi wengine wa habari pia wamelengwa kwenye matukio kama haya. mwandishi wa habari wa Oximity [44] Julien Barinzigo alikamatwa tarehe 17 Juni na kuachiwa tarehe 5 Agosti sambamba na makatazo kadhaa. Gisa Steve Irakoze wa kituo cha redio cha Buja FM alikamatwa [45] na SNR mapema mwezi agusti na kabla ya kuachiliwa tarehe 25 Agusti.

Baadhi hawajarejea. Mwanaharakati wa haki za binadamuMarie [46]-Claudette Kwizera, pamoja na wa shirika la kutetea haki, Ligue Iteka, hawajaonekana tangu mwezi Disemba 2015 mara baada ya kutaarifiwa kuwa walikamatwa na maafisa wa usalama. Rais wa APRODH, Pierre-Claver Mbonimpa yupo uhamishoni [47] mara baada ya kunusurika kwenye tukio la mauaji la mwaka jana, ambapo katika tukio hilo, ndugu zake waliuawa.

Hatari ya kushambuliwa inawakuta hata wanahabari [48] wanaoishi uhamishoni. Boaz [49] Ntaconayigize, mwanahabari nayefanya kazi na Bonesha, aliye uhamishoni jijini Kampala, alichomwa na kisu manamo tarehe 31 Julai. Alisema kuwa maafisa wa usalama waliwasili [50] kwa siri kwenye kambi za wakimbizi kutoka Bujumbura kwa lengo la kuwasaka waandishi wa habari na wanaharakati. Baadae, Boaz alihojiwa pia na polisi wa nchini Uganda.

Ikichukuliwa kuwa watu wengi wameshapotea katika mazingira ya kutatanisha au hata kukutwa wakiwa wamefarikiafter being detained [51], hali ya maafisa wa serikali kukanusha kushikiliwa kwa Jean kumewaweka marafiki na wafanyakazi wenzake na Jean katika hali hofu kuwa serikali inaweza kuwa inaficha taarifa za alipo au kuhusu kifo chake. Mnamo tarehe 25 Agusti, wahariri wa Iwacu walichapisha “ Barua [52] kwa Jean [52]” wakionesha matumaini yao ya kumpata Jean na pia hofu yao ya kupatwa na mabaya.

Cher Jean nous sommes tellement impuissants face à ceux qui ont fait de la mort leur spécialité.
(…)
Aujourd’hui nous n’avons que des mots.
Mais les mots sont plus forts que la mort.
Jean, ils ne gagneront pas !

Dear Jean we are so powerless against those who have made death their speciality.
(…)
Leo tuna maneno tu.
Hata hivyo, maneno yana nguvu kuliko kifo.
Jean, tunakuhakikishia hawataweza!