Mnamo tarehe 6 Septemba, mahakama ya rufaa ya jiji la Setif lililo Mashariki mwa Algeria ilithibitisha mashtaka ya mwanaharakati Slimane Bouhafs ya kuukashifu Uislam na Mtume Muhammad kupitia mtandao wa Facebook sambamba na kupunguza adhabu ya jela kutoka miaka mitano hadi mitatu.
Mnamo Agosti 7, mahakama ya mwanzo ilimhukumu kwenda jela kwa miaka mitano na faini ya dinari za Algeria 100, 000 (takribani dola la Kimarekani 900) kwa kosa la “kumkosea Mtume” na “kudhalilisha taratibu na maadili ya Uislam” chini ya kifungu cha 144 namba 2 cha kanuni ya adhabu ya nchini Algeria. Kwenye rufaa, mahakama ya rufaa ya Setif iliridhia mashitaka yake, hata hivyo, ilipunguza hadhabu ya kifungo hadi miaka mitatu pamoja na kupunguza fidia aliyopaswa kuitoa.
Bouhafs,aliyebadili dini na kuwa Mkristo na mwanaharakati akishirikiana na Muungano wa kundi la Mtakatifu Agustino la nchini Algeria kw pamoja wanapigania haki ya makundi madogo ya kidini nchini Algeria, kwa mara kadhaa amekuwa akichapisha makala kuhusiana na hali ya jamii ndogo ya kikristo nchini Algeria kupitia mtandao wa Facebook, his Google+ na kwenye blogu yake . Kwa mujibu wa shirika la Amnesty International, yeye pia ni mfuasi wa Harakati za Kujipambanua za Kabylia (MAK), kundi la kisiasa linalojitegemea limalojaribu kutafuta hali ya kujitawala katika eneo la Kabylia.
Alikamatwa Julai 31, kufuatia makala alizochapisha kati ya Mei na Juni 2016 kwenye ukurasa wake wa Facebook. Moja ya makala inayodhaniwa kuwa ndio iliyotumika kama ushahidi dhidi yake ilichapishwa Juni 21. Katika chapisho hilo, Bouhafs alisambaza kibonzo kilichoandaliwa na jarida la mizaha la Charlie Hebdo iliyomuonesha Mtume Muhammad akilia pamoja na kuweka maoni haya:
Muhammad analia kwa kuwa ameshajua kuwa hana nafasi tena Kabylia, hata na Algeria yote. Uongo wake utapotea kwa kuwa mwanga wa Kristo umewasili, kwani yeye ni amani, ukweli na njia ya kweli.
Kiungo cha makala yake kwenye mtandao wa Facebook na inayosadikiwa kuwa ndio iliyomsababishia kufungwa gerezani kwa sasa haina tena kibonzo cha Charlie Hebdo. Hata hivyo, makala hii ikiwa na kibonzo hicho badoHowever, inaonekana kwenye blogu yake.
Shirika la Amnesty International na Human Rights Watch kwa pamoja yamekosoa kukamatwa kwa Bouhaf pamoja na mashtaka yanayomkabili. Shirikisho la Watetea haki za Binadamu la nchini Algeria (ambalo liliteua mawakili wa kumuwakilisha Bouhaf kwenye kesi yake ya rufaa) ililaani hukumu iliyotolewa kwani ilikiuka katiba ya Algeria na makubaliano ya Kimataifa ya haki za binadamu na kuzitaka mamlaka husika kubadili kifungu cha sheria namba 144 cha kanuni ya adhabu kinachofanya kuwa ni jinai kukashifu dini pamoja na alama za Taifa. Serikali ya Algeria, mara kw mara imekuwa ikitumia kifungu hiki cha sheria kuwanyamazisha wale wanaokosoa Taifa au dini. Mwandishi wa habari Mohamed Tamalt kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka miwili gerezani kwa kumkosoa Rais Abdelaziz Bouteflika kupitia shairi alilolichapisha kwenye mtandao wa Facebook.