‘Kiwiko Chako Kikiwasha, Utapata Fedha,’ na Imani Nyingine za ki-Afrika

Three legged pots commonly used in Botswana. If a young woman eats out of them, she will not get married. Creative Commons image by Rach151.

Vyungu vyenye miguu mitatu vinavyotumika zaidi Botswana. Kama msichana akila chakula kikiwa kwenye chungu, inaaminiwa hataolewa. Picha ya Creative Commons imepigwa na Rach151.

Wa-Afrika, kama watu wengine duniani, hutumia mtandao wa Twita kwa namna mbalimbali. Wakati mwingine ni kwa ajili ya vichekesho. Wakati mwingine ni kutafuta yale yanayofanana kwa nchi na utamaduni tofauti. Wakati mwingine ni yote kwa pamoja.

Kwa mfano, @IGtiz, mwanafunzi wa Kenya, ameanzisha alama ishara ya #100AfricanMyths kujaribu kukusanya imani zinazorithishwa kutoka kizazi kimoja mpaka kingine kwa masimulizi, katika nchi za ki-Afrika.

Imani katika Afrika zinasaidia kukidhi mahitaji tofauti ya kijamii na kiutamaduni. Wazazi, kwa mfano, wanatumia imani hizi kwa ajili ya kuwafuatilia vijana wao.

Hapa ni baadhi ya mifano ya imani za ki-Afrika zinazochekesha.

Faith Mulungi, mtangazaji wa radio nchini Uganda, alitwiti:

Kiwiko chako kikiwasha, utapokea pesa

@PatohShanqueels alieleza imani maarufu mashuleni wakati wa kuchapwa viboko:

Kuweka kitunguu kwenye kwapa kunafanya uzimie mwalimu akikuchapa

Usikate kucha zako usiku, kwa mujibu wa @xolelwandengane aliyeko Afrika Kusini:

Huwezi kukata kucha zako usiku, kwa sababu wachawi watakuja na kuzichukua

Flo Letoaba, mtangazaji wa redio nchini Afrika Kusini, aliongeza hii kwenye majadiliano hayo:

Ukila chakula kikiwa bado kwenye chungu, hutaolewa

Kupiga mluzi usiku kwaweza kuwa hatari —inasemekana:

Ukipiga mluzi usiku, nyoka atakuja chumbani kwako

Watoto walifundishwa kutokumcheka mlemavu, kwa mujibu wa @NaughtyMilz aliyeko Uganda:

Kama ukimcheka mlemavu unaweza kuzaa mtoto kilema…

Bundi ni mjumbe wa kifo, anasema @iGitz_:

Kama bundi atalia karibu na nyumba yako, basi kuna mtu atafariki dunia

Usiifagilie bahati itoke nyumbani kwako, Vinnie wa Kenya alionya:

Usifagie uchafu usiku na ukaotoa nje, kufanya hivyo ni kuitoa bahati nyumbani kwako

Imani hizi zilitumiwa kuwafanya watoto wazingatie masomo:

Kukaa kwenye mstari wa kwanza shuleni kunakuhakikishia kufaulu

Ingawa imani hizi zimetoka katika sehemu mbalimbali za Afrika, Dickens Jnr, raia wa Marekani mwenye asili ya afrika aishiye Michigan, Marekani anasema amezisikia zote:

Hizi imani zote za ki-Afrika zilizosemwa mtandaoni zinachekesha. Haki ya Mungu nimeshazisikia zote

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.