Colombia Vijijini kuna Mwalimu Anayezunguka na Punda Wawili, Anatembeza Vitabu kwa Ajili ya Watoto Kujisomea

Biblioburro, biblioteca itinerante en Colombia. Acción Visual/Diana Arias - Wikipedia (CC BY-SA 3.0)

Biblioburros, Maktaba tembezi nchini Colombia. Image: Acción Visual / Diana Arias / Wikipedia (CC BY-SA 3.0).

Dunia ingekuwaje kama kusingekuwa na hali ya utayari na ubunifu miongoni mwa wale wanaoona mambo yanavyokwenda na kisha kutafakari wanaweza kufanya nini ili kuboresha? Ulimwengu ungekuwaje kama kusingekuwa na walimu?

Luis Soriano, mwalimu wa shule ya sekondari na raia wa Colombia aliyezaliwa huko Nueva Granada, anatambua thamani ya elimu. Amekulia kwenye jamii ya manispaa ya La Gloria, wilaya ya Cesar. Soriano alipata elimu ya stashahada ya Fasihi ya Lugha ya Kihispania, shukrani zimwendee Profesa aliyekuwa akizuru kijijini kwake kila baada ya miezi miwili.

Akiwa anatambua umuhimu wa kujisomea, Soriano anafanya kila juhudi ili kuhakikisha kuwa vitabu vinawafikia watoto hata pale ambapo katika hali ya kawaida wasingeweza kuvipata. “Biblioburros” (kwa maana nyingine “Punda Maktaba”) ni  maktaba tembezi inayosambaza vitabu katika maeneo mbalimbali ya Kaskazini mwa Colombia kwa punda kuvibeba migongoni mwao, punda wanaojulikana kwa majina ya Alfa na Beto, ambapo majina yao kwa pamoja yanaunda neno alfabeto, au “herufi” kwa lugha ya Kihispania. Na jambo jingine zaidi: hawa ndio “ punda walio na akili kuliko wengine wote duniani,” kwa mujibu wa blogu ya Narrative Journalism ya Marekani ya Kusini:

En 1997 [Soriano] tuvo una idea que para muchos fue maravillosa, pero para otros constituyó una verdadera locura: por su propia cuenta decidió cargar en el lomo de dos burros 70 libros de matemáticas, literatura geografía e historia. ¿Su objetivo? Llevarlos a diferentes niños sin recursos ubicados en apartadas zonas de su municipio.

Mwaka 1997, [Soriano] alikuwa na wazo ambalo wengi walilifurahia pamoja na kuwa kuna baadhi waliona kama ni uwendawazimu: kwa utashi wake aliamua kuwabebesha punda wawili vitabu 70 vya hisabati, fasihi, Jiografia, na historia. Lengo lake lilikuwa nini? Lengo lilikuwa kuwafikishia vitabu watoto masikini wanaoishi maeneo ya mbali sana na mji.

Luis Soriano amekuwa akifurahia kujisomea tangu alipokuwa mdogo-tabia aliyoipata kutoka kwa shangazi yake, ambaye kupitia yeye  alifahamu kuhusu shairi la kihistoria lililoandikwa na mtunzi wa mashairi raia wa Nicaragua Rubén Darío:

Sin duda Soriano es un quijote colombiano, que enloqueció como el Caballero de la Triste Figura con los libros. Cuando su tía le leyó “Margarita está linda la mar”, no pudo dormir en ocho días. Tenía cuatro años y si no lo adivinaba entonces, al menos intuía que su vida estaría íntimamente ligada con la literatura.

Hakuna shaka katika hili, Soriano ni mfalme wa riwaya aliye na mapenzi yaliyopitiliza, ni kama ilivyo kwa Don Quixote, kwa usomaji wa vitabu. Wakati shangazi yake alipomsomea “Margarita,namna bahari ilivyotulia,” hakuweza kulala kwa siku nane. Kwa wakati huo alikuwa na umri wa miaka minne na kama kwa wakati huo hakuweza kuona kipaji chake, angalao aliweza kuwa na utambuzi kuwa katika siku zijazo angalijikita kwenye fasihi.

Hivi karibuni, Soriano aliongea na tovuti ya CCN.com, huku akitaja baadhi ya mambo yanayomhamasisha kwenye mradi wake wa Punda Maktaba. Kwa mujibu wa tovuti hii:

Maeneo ya vijijini, mtoto ni lazima atembee au apande punda kwa takribani dakika 40 ili kufika katika shule ya karibu. […] Watoto wana nafasi ndogo sana ya kuendelea na masomo ya sekondari. […]. Pia, ni walimu wachache sana ambao wangependa kufundisha katika maeneo haya ya vijijini.

Anapendelea pia siyo tu kusambaza vitabu vilivyo katika lugha ya Kihispania pekee: Pia, Soriano anawapatia vitabu vichache vilivyo katika lugha ya Kiingereza wasomaji wake wachanga:

Akiwa katika jitihada yake ya kufa na kupona ya kufuta ujinga katika maeneo ya vijijini, Soriano anatazamia kukuza zaidi mradi wa vitabu vya kiingereza ambavyo kwa sasa ni vichache mno. Kwa kutambua umuhimu wa kufahamu lugha zaidi ya moja kwenye nchi ambayo siku hadi siku inazidi kuunganishwa na mataifa mengine kupitia njia za kidigitali na machapisho, anaona ni muhimu sana kwa watoto wa vijijini kujisomea maandiko yaliyo katika lugha inayotumika kwa kiasi kikubwa kabisa duniani.

Video hapa chini inamuonesha Luis Soriano akiwa kazini, akibainisha ugumu anaokabiliana nao wa kupata vitabu katika maeneo mbalimbali. Hata hivyo, hapa ndipo umuhimu wake na punda wake unapoonekana.

Tengo 3,480 libros guardados en cajas, metidos en anaqueles, en burriquetes, en cajas, cajitas. En donde mis amigos tengo también porque no habría espacio para mí ni para los libros. […]

Alfa es la que prácticamente lleva toda la biblioteca, 120 títulos cargamos en esta biblioteca para el goce y el disfrute de los niños del campo. Tenemos recorridos de 3, 4, 5, hasta de 11 horas. Son 8 horas montado en burro.

Este es mi compromiso de vida. Sentirme útil a la sociedad a la que pertenezco.

Nina vitabu 3,480 vilivyohifadhiwa kwenye maboksi, kupangwa kwenye rafu ana kwenye viboksi vidogo. Vingine nimeviombea kwa rafiki zangu, vinginevyo, kusingalipatikana nafasi ya ziada kwa ajili yangu wala ya vitabu. […] Alfa ndiye punda anayebeba vitabu vyote, tuna takribani vitabu 120 kwa ajili ya watoto wa vijijini kujisomea. Tunafunga safari kwa masaa 3, 4, 5, na hata masaa 11. Hii ina maana kuwa, kuna masaa 8 ya kupanda punda.

Hili ni jukumu langu la kudumu na la manufaa la kuitumikia jamii yangu.

Katika makala iliyoonekana kwenye tovuti ya habari ya Quartz, Biblioburros ilitajwa kama moja ya maktaba nane ambazo kila mpenzi wa vitabu anapaswa kuitembelea. Pia, Quartz iliamsha shauku miongoni mwa wazungumzaji wa kiingereza na ambao ni watumiaji wa mtandao wa Twitter.

Kufuatia juhudi zake, imefikia mahali Luis Soriano amepewa sifa ya heshima ya kudumu kwenye kitabu cha watoto kilichoandikwa na Jeanette Winter!

El maestro Luis un día decide cargar sus dos burros, Alfa y Beto, con libros, para llevarlos a los niños que, por vivir en alejadas zonas rurales, no tienen acceso a ellos. Desde entonces, recorre el país con su biblioteca ambulante.

Siku moja, Mwalimu Luis aliamua kuwatwika vitabu punda wake, Alfa na Beto na kisha kuvipeleka vitabu hivyo hadi maeneo ya vijijini kwa ajili ya watoto ambao hawakuwa na uwezo wa kuvipata vitabu hivyo. Tangu wakati huo, amekuwa akipita maeneo mbalimbali ya nchi na maktaba yake tembezi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.