- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Nchini Naijeria, Unaweza Kukamatwa kwa Kumwita Mbwa Jina Linalofanana na la Rais

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Naijeria, Haki za Binadamu, Uandishi wa Habari za Kiraia, Ubaguzi wa Rangi, Uhuru wa Kujieleza
Nigerian citizen named his dog after the Nigerian president Muhammadu Buhari. Creative Commons photo by e Tasnim News Agency. [1]

Raia wa Nigeria alimpatia mbwa wake jina lifanananalo na la Rais wa nchi hiyo Muhammadu Buhari. Picha kwa hisani ya Erfan Kouchari wa Shirika la habari la Tasnim na imetumiwa kwa masharti ya Creative Commons .

Mfanyabiashara ajulikaye kwa jina la Joe Fortemose Chinakwe amekamatwa na maafisa wa polisi wa Nigeria baada ya kumwita mtoto wa mbwa wake jina la “Buhari,” ambalo ni jina la ubini la Rais wa Nigeria, tukio amnbalo linahusisha historia ndefu ya mivutano ya kimakabila nchini Nigeria.

Mbwa huyo alipewa jina la mtu aliyefahamika kwa jina la Alhaji Buhari, ambaye ni jirani yake na ndugu Chinakwe. Hata hivyo, jirani mweingine alitoa taarifa ya tukio hilo, na watu wengi wametafsiri kuwa jina hilo limetokana na jina la Rais Muhammadu Buhari [2] (PMB).

Mamlaka zilitaarifu kuwa Chinakwe angeshitakiwa kwa “kosa la kutaka kuvunja amani,” hii ni kwa mujibu wa Gazeti la Vanguard [5] kwenye taarifa yake ya tarehe 17.

Unajua raia wa kawaida wa Kaskazini atajihisi vibaya kwa jambo kama hili. Linaweza kusababisha ugomvi mbaya sana au mvutano wa kidini kwani kwa kumpatatia mtu mwingine jina hilo ni kama vile unamdhalilisha kwa namna fulani.

Nigeria ni taifa la mrengo wa makabila [6] likiwa na zaidi ya makabila 250 sambamba na historia ya mivutano mibaya [7]. Makabila makubwa matatu ni Hausa na Fulani kwa upande wa Kaskazini, WaYoruba kwa upande wa Magharibi na WaIgbo kwa upande wa Mashariki. Nigeria bado inayavumilia makovu ya miaka mingi ya hali ya kutokuaminiana, The country still bears the scars of years of distrust, mabishano na mipasuko iliyotapakaa kila kona ya nchi na ambayo imendelea kukuzwa vibaya na ukereketwa wa kidini. .
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya nchini Nigeria [8], vilivyoanaza mwaka 1967 hadi 1970, vyanzo vikuu vya mgogoro vya mrengo wa kikabila na kidini na ambavyo bado havijatatuliwa [9] vimechukua nafasi kubwa kwenye masuala ya kijamii na kisiasa nchini Nigeria tangu wakati wa uhuru [10] mnamo mwaka 1960 havijaweza kusaidia kutatua changamoto hii. Kana kwamba haya hayakutosha, wahamasishaji wa makosa yanayowalenga watu wa makabila fulani hawaadhibiwi na utamaduni huu wa kutokuadhibiwa unaendelea kushamiri.

Ni kwa sababu ya historia hii ngumu kuielewa iliyo na mrengo wa kikabila, ndio maana kumpachika mbwa jina- amapo katika hali ya kawaida lilipaswa kuwa jambo la kawaida kabisa– limepewa kipau mbele kikubwa kabisa kwenye vyombo vya habari nchini Nigeria.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, Chinakwe alimwandika mbwa wake kweye pande zote za ubavu na kisha kumpitisha mbwa huyo kwenye maeneo ya majirani zake ambao weingi wao ni wa kabial la Hausa. Kwa kawaida, kabila la Hausa ni wachache Kusini Magharibi mwa jiji la Osan, ambapo ndipo yalipo makazi ya Chinakwe.

Rais Muhammadu Buhari kwa upande wake, yeye ni wa kabila la Fulani.

Katika hali ya kawaida, habari za kukamatwa kwa Chinakwe na sababu za kukamatwa kwake hazikupokelewa vizuri na raia wa Nigeria. Abimbola Adedokun [11], mwandishi wa magazeti, alionesha madhara kuruhusu kuwepo kwa mipasuko ya kimakabila au ya kidini:

Historia imetufundisha kuwa, pale “raia wa kawaida wa kutoka kaskazini” anaposema “hafurahishwi na jambo fulani”, wengine wote hatuna budi kujisahihisha na kubadili mienendo yetu haraka sana. Tuanaambiwa tuchukue tahadhari ya vikwazo visivyoonekana na ambavyo wale wasio na imani hawaruhusiwi kuvivuka. Kwa hali ilivyo, wengi wetu tumejiwekea vikwazo dhidi ya hali ya kujizuia kujiingiza kwenye chuki hii. Tumeainisha “maeneo tusiyopaswa kupita” ya mijadala ya wazi ambayo tunajipitia huku kukiwa tumejiweka kwenye hatari kubwa kabisa. Tumeshajionea matokeo ya kuvuka mipaka hii na matokeo yake si mazuri. Kutokea kwenye mauaji ya Gideon Akaluka hadi kwenye machafuko ya kampeni ya kidini ya Reinhard Bonnke, vurugu za mashindano ya Mlimbwende wa Dunia, suala la katuni za kidenishi pamoja na matukio mengine mengi yaliyotokea na kupelekea machafuko ambayo hayakutarajiwa, kwa muda sasa tumegundua kuwa tunakabiliana na mzimu aliyejeruhiwa na mwenye hasira ambaye anahitaji sisi tutoe utu wetu sadaka ili atuache tuendelee kuishi.

Gideon Akaluka alikuwa ni mfanyabiashara wa Nigeria kutoka kabila la Igbo ambaye alikatwa kichwa hadi kufa na kundi la watu [12] mnamo mwaka 1994 kwa kile kinachodhaniwa kuwa alikashifu Koran. Mwaka 1991 Nigeria ilitembelewa na mwingilisti wa kikatoliki, Mjerumani Reinhard Bonnke yaliibuka machafuko mabaya [13] huko Kusini mwa jimbo la Kano mara baada ya kuripotiwa kuwa aliwabadili dini baadhi ya Waislamu na kuwa Wakristu.

Mwaka 2002, zaidi ya watu 200 waliuawa na makumi mawili ya makanisa kushambuliwa wakati wa machafuko ya siku tatu mfululizo huko kaskazini kufuatia Nigeria kuwa mwenyeji wa shindano la kumpata mlimbwende wa Dunia [14]. Na mwaka 2005, gazeti la Kidenishi lililochapisha katuni zilizokuwa zikimzungumzia Nabii Muhammad ziliibua maandamano [15] kwenye nchi mbalimbali, Nigeria ikiwa miongoni.

Adedokun aliendelea:

Tatizo nni kuwa hii laana ya machafuko inayoikaba jamii yetu ni vigumu sana kuipunguzaThe trouble is that this evil spirit of violence who has a chokehold on our society is implacable. Laana hii imegharimu maisha ya watu wengi wasio na hatia na kujihakikishia umiliki halali wa maisha yetu. Machafuko nchini Nigeria, yanatokea siyo kwa sababu ya watu wasio na hofu wala kujali ambao wanasema mambo yanayowafanya watu wengine wajisikie vibaya. Kinyume chake, wanatokana na mitazamo iliyojengeka ya wale wanaofikiri kuwa maisha ya watu wengine ni halali yao, na hawana hofu yoyote ya sharia inayowakataza kutekeleza uhalifu.

Hakuna msingi wowote wa sharia dhidi ya shtaka la Chinakwe, hii ni kwa mujibu wa Monday Ubani [16], ambaye ni Makamu wa pili ajae wa Jumuia ya Kitaifa ya Wanasheria wa Nigeria:

Kwa maujibu wa sharia, siyo kosa la jinai kwa mtu fulani kumpatia jina la mtu fulani mbwa wake. Inaweza kuwa ni uonevu kufuatilia mazingira ya u tukio hilo.

Watumiaji wa Twita nchini Nigeria wamelaumu kwa tukio la Chinakwe kutiwa nguvuni. Mwanamuziki wa Nigeria Seun Anikulapo Kuti, [17] the son of the legendary Fela Kuti [18], alisema:

Wanasheria wetu wa haki za binadamu wako wapi? Hapa haki haijatendeka kabisa, kwa nini serikali haikumkamata OBJ aliyempa Sokwe wake jina la Patience?

OBJ ni kifupisho cha Rais aliyepita wa Nigeria Olusegun Obasanjo, ambaye hapoa awali alikuwa na mtoto wa sokwe [21] aliyempa jina la Patience, linalodaiwa kuwa ni jina la Patience Jonathan, mke wa Rais mwingine mstaafu, Goodluck Jonathan. Obasanjo alikataa kumpigia kampeni Jonathan kwenye uchanguzi mkuu wa mwa Nigeria wa mweaka 2015, ambapo Rais wa sasa, Muhammadu Buhari alishinda.

Reno Omokiri, msemaji mpya wa Rais mstaafu Jonathan, wa kupitia vyombo vya habari, alitanabaisha kuptia ukurasa wake wa Twita kuwa ilikuwa vyema kwa watu kutilia maanani maoni yake:

Omokiri amerejea Makala yake ya Twita ya tarehe 11 Agusti [24]: “Kama unataka kufahamu kama kuna mabadiliko nchini Nigeria, mtukane PMB [Muhammadu Buhari] namna ulivyokuwa unamtukana GEJ [Goodluck Jonathan] na hapo ndipo utakapojua haswa nini maana ya ‘badiliko'!” Buhari alishiriki kwenye mdahalo mrefu wa jukwaa la “mabadiliko” [25] dhidi ya Jonathan kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Mtumiaji wa Twita, MaziNze aliwalaumu polisi kwa kuwa na ubaguzi kwenye matumizi ya sheria:

Vingozi wa jamii ya wafugaji wa kabila la Fulani [27] walituhumiwa kwa kosa la kuvamia [28] jamii [29] za wakulima nchini Nigeria na na kuwaacha kifo [30] kikiwanyemelea [31].

Na mwezi Juni, mwanamke mmoja aliuawa na kundi la watu huko Kano kwa kosa lililodhaniwa la kumkashifu [32] Nabii Mohammed. Tukio kama hilo lilitokea kwa mwanamke mwingine mezi wa Julai, ambaye alikatwakatwa hadi kufa [33] katika mji mkuu wa Nigeria, tukio linalodhaniwa kufanywa na Waislam wenye msimamo mkali.

Kemi alichapisha picha za Ali Baba, mchekeshaji wa Nigeria akiwa na mbwa wake aliowapa majina ya watu maarufu na viongozi maarufu ulimwenguni.:

Kwa mujibu wa Inibehe Effiong, imeripotiwa kuwa Chinakwe ameshaachiliwa kwa dhamana. Kwenye ukurasa wake wa Facebook aliandika kuwa, watu wawili—mmoja kutoka upande wa Kaskazini na mwingine kutoka upande wa Kusini – walichangisha fedha fedha za kugharamia mahitaji yake ya kisheriadonated. Alifafanua [36]:

Yeyote ambaye ana mashaka kuhusu kesi hii kuhusishwa na siasa anapaswa kuifuatilia dhamira yake kwa ukaribu kabisa. Kwa wale wanaotumia ukabila, dini na mrengo wa kisiasa ili kulikuza kupita kiasi shauri hili, wanapaswa kufahamu kuwa Nigeria ni nchi ya sheria.

Jumuia ya wasimamizi wa haki za binadamu hawataweza kukaa kimya na kutazama raia wasio na hatia wakifadhaishwa na kudhalilishwa.

Kwa kuwa watu wawili waliochangia fedha wanatokea Kaskazini na Kusini Magharibi inaonesha kuwa nguvu ya undugu na usawa miongoni mwa waNigeria wazalendo ni zaidi ya watu wa mzaha na walio na ushawishi hasi wa ukabila na udini.