‘Watu Wanapanda Boti hizo kwa Kuwa Bado Wanahitaji Kuishi’

Capture d'écran d'une action de sauvetage du projet SOS méditerranée via YouTube

Picha iliyochukuliwa kutoka kwenye kamapeni ya uokozi ya SOS Méditerranée kupitia YouTube

Hali ya migogoro na kukosekana kwa amani kunakozisumbua nchi za Kaskazini na Magharibi mwa Afrika pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea huko Syria, watu wanaendelea kuhatarisha maisha yao kwa kuvuka bahari ya Mediterranean kwa kutumia boti zisizofaa kwa ajili ya kutafuta hifadhi kwenye mataifa ya Ulaya.

Njia hizi zimegharimu kwa kiasi kikubwa kabisa maisha ya watu. Mwaka 2015, zaidi ya watu milioni moja walikadiriwa kuwa waliingia kwenye mataifa ya nchi za Ulaya kwa njia ya bahari, mara tano zaidi ya mwaka uliopita. Hadi sasa, mwaka 2016, idadi hii imefikia zaidi ya watu 240,000. Kwa mujibu wa Shirika la Wakimbizi la UN , mwaka 2014, takribani watu 3,500 waliojaribu kuhamia Ulaya walipoteza maisha, ama hawakujulikana walipo kwenye bahari ya Mediterranean. Mwaka 2015, idadi hii ilipanda na kufikia watu 3,771. Mwaka huu, watu 2, 944 wameshateketea.

Na hapa ndipo nafasi ya SOS Méditerranée inapoonekana. SOS Mediterranée ni taasisi inayolenga kutoa msaada kwa mtu yeyote anayepatwa na matatizo baharini, ikiwa ni wanaume, wanawake au watoto, wahamiaji au wakimbizi wanaojikuta katika hali ya hatari pindi wanapojaribu kuvuka bahari ya Mediterranean. Mradi huu unafadhiliwa na wafadhili binafsi na misaada kutoka serikalini. Fedha zinazopatikana zinatumika kwa ajili ya kukodisha boti pamoja na gharama za kila siku za matengenezo na uokozi.

Le bateau Aquarius en 2012 à Cuxhaven CC BY-SA 3.0

MS Aquarius huko Cuxhaven, 2012. CC BY-SA 3.0

Meli inayotumika kwenye kampeni hii ni Aquarius. SOS Mediterranée ilianzishwa na Baharia mfanyabiashara wa Ujerumani kapteni Klaus Vogel na Sophie Beau wa Ufaransa walio na uzoefu wa programu za utoaji wa misaada ya kibinadamu. Mradi huu ulianzishwa mara baada ya Operation Mare Nostrum ya jeshi la majini la Italia, mradi uliolenga pia kuwaokoa wahamiaji waliopatwa na misukosuko baharini.

Blogu ya SOS Mediterranée imeweka maelezo ya baadhi ya watu waliosafiri katika safari hizi za hatari. Zifuatazo ni baadhi tu ya simulizi zao.

Kebba ni kijana wa miaka 22 na ni fundi wa kuchomea vyuma kutoka nchini Gambia. Aliondoka nchini mwake kwa sababu ya uongozi wa kidikteta na pia kutokana na kukosekana kwa ajira:

La seule façon d’avancer est de devenir soldat, et je n’ai pas voulu faire ça. J’ai perdu mon père et il fallait que je soutienne ma mère et mes jeunes soeurs, alors je suis parti chercher du travail ailleurs. En Libye, j’ai été kidnappé. J’ai été détenu dans un camp pendant deux mois. Il n’y avait presque pas de nourriture, pas d’eau, pas d’endroit pour dormir. Ils ont tué six personnes que je connaissais dans les camps. Ils disent ‘donne-nous ton argent ou on te tue’, et ils tiennent parole. J’ai voulu rentrer chez nous mais je n’avais aucun moyen de m’y rendre. Alors j’ai décidé de prendre ce risque de partir en Europe. Les trafiquants nous ont gardé dans un autre camp, pendant deux ou trois semaines. Le jour venu, ils nous ont entassés dans le bateau en caoutchouc. Il n’y avait pas de capitaine, seulement la volonté de Dieu. J’ai deux rêves— de devenir soudeur en mer et d’écrire un livre sur ce voyage. Mais si la vie ne m’accorde rien d’autre, j’espère au moins pouvoir vivre en paix

Namna pekee ya kusonga mbele ni kuwa mwanajeshi, na mimi sikuhitaji kufanya hivyo. Nilimpoteza baba yangu na hivyo nilichukua jukumu la kumwangalia mama yangu pamoja na dada zangu wadogo, kwa hiyo ilinilazimu nitoke kutafuta fedha. Nikiwa nchini Libya, nilitekwa. Nilishikiliwa kwenye kambi kwa muda wa miezi miwili. Kwa ujumla, hakukuwa na chakula, wala maji na hata sehemu ya kulala. Kambini pale, waliwaua watu sita niliokuwa ninawafahamu. Walikuwa wakisema, “Nipe fedha uliyonayo, vinginevyo, ninakuua”, na hatimaye walitekeleza walichosema. Nilifikia hatua ya kutaka kurudi nyumbani, hata hivyo sikuwa na namna ya kuondoka. Kwa hiyo, niliamua kujaribu kuelekea Ulaya. Wavushaji walituweka kwenye kambi nyingine kwa muda wa kati ya wiki mbili au tatu. Siku ilipowadia, walitushindilia kwenye boti ya mpira. Hakukuwa na mwongoza boti, ilikuwa ni kudra za mwenyezi Mungu tu. Nina ndoto mbili: yakwanza ni kuwa mchomeleaji wa vyuma wa majini na pia kuandika kitabu kuhusu safari hii. Hata hivyo, kama maisha hayata nitunuku jambo jingine, angalao nina matumaini ya kuishi kwa amani.

Capture d'écran de la vidéo du projet sur YouTube

Picha kutoka kwenye video ya uokozi wakati wa operesheni –Chaneli ya YouTube

Cyrill ni afisa wa Cameroon aliyekimbia ukatili wa wanamgambo wa kundi la Boko Haram huko Kaskazini mwa nchi yake. Aliongelea kuhusu nyumba za mateso, unyang’anyi pamoja na machafuko aliyoyashuhudia nchini Libya, ambayo ndio sehemu ya pekee ya watu kuondoka kwa boti zinazoelekea Ulaya:

La Libye est un pays hors du monde, qui a perdu tout sens moral. Un monde revenu à la condition de la chair animale. Ces enfants qui s’entraînent à tirer sur les noirs dans la rue, les rackettent en leur mettant une lame sur la gorge ou apprennent à torturer les migrants sous le regard de leurs parents. Ils parlent du viol systématique des femmes sur la route, de ces passeurs ou geôliers impitoyables qui les battent et leur crachent dessus en leur répétant qu’ils ne valent pas le pain qu’on leur donne.

Libya ni nchi iliyo kwenye ulimwengu mwingine- ni nchi iliyopoteza kabisa thamani ya utu. Ni chi iliyorudi kwenye zama za unyama. Mitaani kuna watoto wanaofundishwa kuua watu weusi kwa risasi, kunyang’anya mali kwa kuwatishia watu kuwa wangewakata makoo kwa nyembe, au wanajifunza kuwatesa wahamiaji ilihali wakitazamwa na wazazi wao. Wanaongea kuhusu utaratibu wa kuwabaka wanawake mitaani, wavushaji binadamu wasio na utu pamoja na walinzi wanawapiga na kuwatemea mate na kisha kuwatukana kuwa hawana thamani kama ilivyo kwa mikate wanayowapatia.

Gode Mosle ni kijana wa miaka 22 kutoka nchini Syria aliyekuwa anaishi Damascus. Kwa sasa yupo nchini Swiden lakini huwa anasongwa sana na hali ya kuweweseka pindi akumbukapo namna alivyoweza kujiokoa:

J'ai dit à mes amis en Syrie de ne pas prendre ces bateaux. Il faut qu'ils viennent par la Turquie et la Grèce, même si c'est beaucoup plus cher. On était environ 700 dans le bateau mais il n'y avait en fait de la place que pour la moitié .Ces passeurs sont des animaux. Ils crient sur les gens, les volent et les frappent quand ils embarquent. C'était une sorte de torture psychologique qui a commencé avant même le bateau. Deux Africains sont morts dans la cale. Ils ont été asphyxiés, ils ne pouvaient pas respirer à cause des émanations du moteur. C'était bancal, on ne pouvait pas se mettre debout ou bouger. Dès que quelqu'un le faisait le bateau menaçait de chavirer .Il y avait beaucoup de hurlements. Je ne referais pas ce voyage. Je ne peux pas oublier ce que j'ai vu. Les gens veulent vivre, c'est pour ça qu'ils embarquent sur ces bateaux.

Niliwaambia rafiki zangu walioko Syria kuwa wasithubutu kutumia boti hizi. Ni vyema wapitie Uturuki na Ugiriki pamoja na kuwa ni gharama zaidi. Kwenye boti, tulikuwemo takribani watu 700 lakini nafasi iliyokuwepo haikuwa ya kutosheleza hata nusu yetu. Wavushaji wale ni wanyama. Wanawakaripia watu, wanawaibia na kuwapiga watu wanapopanda kwenye boti. Ilikuwa ni namna ya kuwaathiri watu kisaikolojia hata kabla ya kupanda kenye boti. Waafrika wawili walipoteza maisha wakiwa kwenye sehemu ya kuwekea mizigo. Waliishiwa pumzi; hawakuweza kupumua kwa sababu ya hewa chafu kutoka kwenye injini. Hali ilikuwa tete sana, hatukuweza kusimama wala kusogea. Pale tu mtu alipojaribu kujisogeza, kulikuwa na hatari ya boti kupinduka. Kulikuwa na mayoye ya mara kwa mara. Sitakaa tena kurudia safari ya namna hiyo. Sitaweza kusahau kile nilichokishuhudia. Watu wanazitumia boti hizo kwa kuwa bado wanahitaji kuishi.

Kwa mengi zaidi kuhusu habari kama hizi, For more on the subject, a French-language Makala za video zilizoandaliwa na Jean Paul Mari katika lugha ya Kifaransa zinazonesha changamoto wanazokabiliana nazo SOS Méditerranée katika muda wa mwaka mmoja wa kazi yao:

https://www.youtube.com/watch?v=LdD0oOlhmeY

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.