Wananchi wa Uganda Wanataka Serikali Isaidie Kunusuru Shule, Sio Matajiri

A public school in Uganda. Tweeps argue that taxpayers money need to bail out schools like this one. Image released under Creative Commons by The Sustainable Sanitation Alliance.

Shule ya umma nchini Uganda. Watumiji wanasema fedha za walipa kodi zinahitaji kunusuru shule kama hizi. Picha ya Creative Common na The Sustainable Sanitation Alliance.

Pale  habari zilipoenea kwamba serikali ya Uganda inakusudia kutumia kiasi cha shilingi za Uganda Trilioni moja (Dola za Kimarekani milioni 300) za walipa kodi kwa ajili ya kunusu biashara kubwa, wa-Ganda walio kwenye mtandao wa Twita waliuita mpango huo kama ‘ufisadi’ na kupendekeza kwamba fedha hizo zingetumika kunusuru shule za umma zilizotelekezwa.

Makampuni ambayo serikali inataka kuyanusuru na mzigo wa madeni makubwa yaliyotokana na mikopo iliyochukuliwa kutoka kwenye mabenki mbalimbali nchini Uganda. Biashara nyingi zinaendeshwa na wafanyabiashara wakubwa wenye nguvu. Baadhi ya maafisa wa benki kuu na wizara ya fedha wamepinga mpango huo.

David Mpanga, mwanasheria wa Uganda, aliuita mpango huo kuwa ni ‘kuwafanya wananchi walipe hasara':

Kubinafsisha faida na kuchangia hasara. Lazima wote tugharamie hasara ya biashara za matajiri lakini lini tulichangia faida wanayopata?

Allan Ssenyonga alishangazwa nkufahamu kwamba mmoja wa makampuni yaliyoorodheshwa kuingia kwenye mpango huo ni biashara ya manyoya:

Club Silk ni moja wapo ya makampuni yanayohitaji kunusuriwa. Hivi kweli hiki ni kipaumbele kwa Uganda?

Fredrick Tumusiime alipendekeza:

Ili hatua zozote za kutoa ruzuku kwa makampuni zifanyike, lazima wananchi wawe na hisa kwenye kampuni husika. Fedha za umma zisitumike kugharamia dhambi za watu binafsi

Wa-Ganda walihoji umuhimu wa mipango hiyo ya kuwasaidia wafanyabiashara wakubwa wenye uhusiano na wanasiasa nchini humo wakati serikali ikiwekeza kidogo sana kwenye miundombinu, shule na huduma za afya.

Sarah Bireete alipendekeza kwamba serikali inusuru shule za umma zenye hali mbaya:

Wa-Ganda masikini wanaendelea kutoa ruzuku kwa matajiri. Kwa nini tusiziokoe shule zisizokuwa na madarasa, vitabu na vyoo?

Jeff aliweka picha ya kampuni moja ambayo alifikiri serikali ingeweza kuisaidia kumaliza madeni yake:

Picha inaonesha ‘kampuni’ ambayo inahitaji sana kupata msaada wa fedha za walipa kodi

Picha nyingine ya shule ya umma yenye hali mbaya:

Shule ya Msingi Karungu, Wilaya ya Buhweju. Hivi shule hii haihitaji msaada? Hapana, tusaidie makampuni ambay0 hata hivyo yanakwepa kodi

Wakati huo huo Samwise Gamgee alishauri:

Kama kutoa msaada kwa makampuni haya ni suala lenye Maslahi ya Taifa, kutoa faida yanayopata makampuni hayo ni suala lenye Maslahi ya Taifa pia

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.