- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Matangazo ya Sauti ya ‘Wiki Ilivyokwenda’ Global Voices: Ndugu, Timiza wajibu Wako: Uhuru, Si Udhibiti

Mada za Habari: China, India, Myanmar (Burma), Nepali, Puerto Rico (Marekani), Censorship, Haki za Binadamu, Maandamano, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vita na Migogoro, Podikasti za Global Voices

Juma hili tunakupeleka hadi Kasmir, Jimbo linalotawaliwa na India [1], Nepal [2] na China [3]. Tutaongea na mwandishi wa Global Voices Angel Carrion kuhusu hatua ya Puerto Rican kupinga bodi ya Marekani kudhibiti fedha [4], na tutaongea na mwandishi wa Global Voices Thant Sin kuhusu kuungwa mkono kwa afisa mmoja nchini Myanmar [5] aliyeamua kuvunja kimya kwa kukemea ubaguzi unaofanywa na kikundi cha kidini cha Kibudha.

Kipindi hiki kina habari ziliandikwa na Kisholoy Mukherjee, Vishal Manve, Sanjib Choudhary, Oiwan Lam, Angel Carrion na Thant Sin. Shukrani nyingi kwa waandishi wetu, watafsiri na wahariri waliowezesha hilo kufanyika.

Kwenye matangazo haya ya “Wiki Ilivyokwenda hapa Global Voices”, tunasindikizwa na muziki wenye leseni ya Creative Commons kutoka Maktaba ya mtandaoni ya Free Music Archive, ikiwa ni pamoja na Please Listen Carefully wa Jahzzar [6]; The Universal Fluff Theory [7] wa Krackatoa; Anamorphic Orchestra [8]wa Alan Singley; Origami 1726 [9]wa the Blue Dot Sessions; Driving me backwards [10] wa Phil Reavis; and Carcrashlander Instrumentals [11]wa Cory Gray.

Picha iliyotumiwa kwenye nembo ya Soundcloud ni kwa hisani ya Andres Musta [12]. Imewekwa kwenye mtandao wa Flickr. Imepigwa mnamo Januari 2, 2012. (CC BY-NC-ND 2.0)