Maafisa wa Myanmar Waungwa Mkono Mitandaoni Kupinga Kikundi Cha Ki-Buddha Chenye Msimamo Mkali

13615377_10157158526775422_5694356960349658329_n

Picha ilitumwa katika ukurasa wa Facebook wa kitamaduni wa Myanma kwa hisani ya Htet Myat Lynn. Huu ni mfano wa mawazo yanayoonesha uhasama uliopo baina ya Waziri Kiongozi wa Yangon; Phyo Min Thein (Kwee Phyo) na Wirathu, kiongozi wa kikundi cha ki-Budhha chenye msimamo mkali.

Phyo Min Thei Waziri Kiongozi wa mji wa Yangon huko Myanma, ametoa kauli yenye uthubutu wiki iliyopita wakati alipotangaza kuwa kundi la ki-Buddha lenye msimamo mkali Ma-Ba-Tha (Chama cha Ulinzi wa Kikabila na Dini)“halihitajiki tena” kwa kuwa kamati ya Kiserikali ya Sangha Maha Nayaka tayari inayashughulikia masuala ya Wabuddha nchini.

Wirathu, kiongozi wa Ma-Ba-Tha mwenye ushawishi mkubwa,ameitathreatened maandamano kwa nchi nzima kama serikali haitamchukulia hatua Phyo Min Thein.

Lakini watumiaji wengi wa mtandao wa intaneti wamezindua kampeni ya kumwunga mkono Waziri huyo.

Kikundi cha Ma-Ba-Tha kilichoundwa mwaka 2013, ni kikundi chenye mrengo wa kidini na kiraia na kimeundwa na watawa wa ki-Buddha na wafuasi wao ambao wamekula kiapo cha kulinda u-Buddha, wa-Buddha na Myanma dhidi ya kinachoitwa “hatari ya kuongezeka na kupanuka kwa Uislam.” Asilimia kubwa ya wananchi wa Myanma ni wa-Buddha, ingawa ina zaidi ya vikundi vingine vidogo vidogo vipatavyo 100 vya madhehebu mengine

Ma-Ba-Tha imejipatiaumaarufu kwa sababu ya kauli zake na vitendo vya kuupinga Uislam. Kwa hakika, kimekuwa chanzo na nguvu kubwa nyuma ya mashambulizi yanayofanywa dhidi ya watu wa Rohingya ambayo ni kikundi cha jamii ya Kiislam inayoishi Magharibi mwa Myanma. Wafuasi wa itikadi hiyo ya Ma-Ba-Tha pamoja na viongozi wake, wamekuwa wakitoa kauli za chuki zikiishurutisha serikali kuwafukuza wa-Rohingya, kwa kuwatuhumu ni wahamiaji haramu na pia ni magaidi. Makundi mengi ya haki za binadamyanadhania kuwa jamii hiyo ya Rohingya ni moja ya vikundi vidogo vya kijamii vinavyoonewa zaidi ulimwenguni.

Phyo Min Thein anayejulikana kama Kwee Phyo na wafuasi wake, ni sehemu ya chama kipya kinachotawala cha National League for Democracy (NLD), na kinaongozwa na mshndi wa tuzo ya Nobel Aung San Suu Kyi. Chama hicho cha NLD kiliingia madarakani Februari 2016 baada yadefeating jeshi kushindwa na chama katika uchaguzi mkuu. Jeshi limekuwa likiingoza nchi tangu 1962 hadi mapema mwaka huu

Kama Waziri Kiongozi wa Yangon Phyo Min Thein amejijengea jina miongoni mwa jamii na kuanzisha mijadala migumu kadhaa reforms, kama ule wa udhibiti wa majengo aliouanzisha wakati wa maadhimisho ya juma la maji ambalo hufanyika kila mwaka Aprili. Lakini wiki hii ameanzisha mada moto zaidi baada ya wiki iliyopita kuongea hadharani akikishutumu kikundi chenye nguvu cha Ma-Ba-Tha.

Bahati nzuri Phyo Min Thein ameungwa mkono na watumiaji wa mitandao na Hashtag #hapanaMaBaTha iliwekwa kwenye kurasa za Facebook kama sehemu ya kampeni za kumtetea na kumuunga mkono waziri dhidi ya watu wanaunga mkono kikundi cha wa-Buddha wenye msimamo mkali

Watumiaji hao hao wa Facebook wanatumia picha hii kwenye kurasa zao kumuunga mkono Waziri Kiongozi:

13590272_1142414625780939_683725030431344279_n

Hii ni sehemu ya majibizano kwa hashtag #‎NOMaBaTha. Htin Linn Aye iliyowatofautisha Ma-Ba-Tha na watawa wengine wa kiBuddha nchini kote:

မြတ်စွာဘုရားရဲ့ တရားတော်တွေကို ကျင့်ကြံအားထုတ် နေထိုင်တဲ့ ဘုရားသားတော်တွေကို ကြည်ညိုတယ်…

ဒါပေမယ့်…

#‎NOMaBaTha‬

Ninawasalimu wote wana wa Buddha mnaofata mafundisho yake

Lakini…

#‎hakunaMaBaTha‬

Hapo chini ni chapisho lililosambaa sana huko facebook:

မဘသ မရှိရင် မင်းခွေးဖြစ်သွားလိမ့်မယ် ပြောနေသူတွေက လွန်ခဲ့တဲ့ မဘသမရှိခင် နှစ်ပေါင်းများစွာက

ခွေးဖြစ်ခဲ့ကြလို့များလား မေးပီလေ အိုင်းစ် :p:p:p:p:p

credit

‪#‎hakunaMaBaTha‬

Kwa wote wanaosema tutakuwa mbwa kama Ma-Ba-Tha haitakuwepo tena, nataka kuwauliza; je tumekuwa mbwa kipindi chote ambacho Ma-Ba-Tha hawakuwepo? :p:p:p:p:p

credit

‪#‎NOMaBaTha‬

Moe Kaung San nafikiri vitendo vya Ma-Ba-Tha vinaichafua taswira ya u-Buddha:

မဘသဟူသော အဖွဲ့အစည်းသည်

အမျိုးဘာသာ သာသနာအား ဗန်းပြ၍

လူမျိုးရေးမုန်းတီးမှု ဘာသာရေးခွဲခြားမှုများဖြင့်

တိုင်းပြည်မငြိမ်သက်အောင် ပြုလုပ်ပြီး

နိုင်ငံရေးတွင်ခြေရှုပ်ကာ ဗုဒ္ဓဘာသာကို

ညိုးနွမ်းစေသောကြောင့်…………….

‪#‎မဘသအလိုမရှိ‬

‪#‎NoMaBaTha‬

Kwa sababu taasisi hii inayoitwa Ma-Ba-Tha ina

jishughulisha na siasa na kuifanya nchi ikose amani kwa

kutengeneza chuki za kikabila na ubaguzi wa kidini kwa jina la kulinda dini na kabila/asili

na wanauwekea v-Buddha picha mbaya
#hatuitamaniMaBaTha

#‎HakunaMaBaTha‬

Piailitengenezwa fomu maalum huko Google kwa ajili ya uungwaji mkono wa kauli ya Waziri Kiongozi wa Yangon aliyoitoa dhidi ya Ma-Ba-Tha.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.