- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Katuni Maarufu ya Ukraini Yaweka Mazingira ya Wazazi Kuzungumzia Usafirishaji Haramu wa Binadamu

Mada za Habari: Ulaya Mashariki na Kati, India, Misri, Ugiriki, Ukraine, Elimu, Filamu, Mawazo, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vichekesho
Screen shot from "How the Cossacks Rescued Their Fiances" (1973). [1]

Picha iliyopigwa kwenye filamu ya “Namna Wakulima wa Kirusi Walivyowanusuru Wachumba Zao” (1973).

Vitendo vya usafirishaji wa binadamu vimekithiri duniani. Kwa mfano kuna taarifa za utumwa wa ‘kimila’ [2] nchini Mauritania; ukahaba wa kulazimishwa [3] barani Ulaya; na vitendo vya utekeaji wa mabibi arusi [4] nchini Kyrgyzstan. Mwaka 2016, inakadiriwa watu milioni 45.8 [5] walikuwa wahanga wa namna fulani ya utumwa katika nchi 167, kwa mujibu wa Kipimo cha Utumwa duniani.

Ingawa vitendo vya utumwa vinaendelea kuzisumbua jamii nyingi duniani, majadiliano kuhusu usafirishwaji wa binadamu na namna mbalimbali za utumwa hayaonekani kupea nafasi kwenye mijadala ya wazi, na mazungumzo haya hayapewi nafasi wazazi wanapozungumza na watoto.

Lakini kipande kilichopo kwenye mfululizo wa katuni maarufu ya Ukraini kinaonekana kuvunja mwiko wa kutokuzungumzia masuala haya ya utumwa na usafirishaji wa binadamu tangu mwaka 1973 katuni hizo zilipoanza kuoneshwa. Hivi sasa kwapitia mtandao wa YouTube, takribani nusu karne baadae, katuni ya, “Namna Wakulima wa Kirusi Walivyowanusuru Wachumba Zao” (How the Cossacks Rescued Their Fiancees”), iliyo kwenye mfululizo uuitwao “Namna Wakulima wa Kirusi..”, zinaonekana kurudia umaarufu wake wa awali. Kipande kimoja cha mfululizo huo, [6] kilichowekwa kwenye tovuti ya video, kimetazamwa mara milioni moja.

Kipande kinachohusu usafirishwaji wa binadamu kimetazamwa zaidi ya mara 500,000 na kinaweka mchanganyiko wa masimulizi ya kale na mazungumzo ya kawaida ya kijamii kwa namna ambayo inaweza kutumiwa kuanzisha mazungumzo kuhusu suala zito la utekaji nyara na utumwa.

Kipande hiki kina urefu wa dakika kama 17 hivi, lakini kinafaa kutazamwa, kwa sababu mwongozaji wake Vladimir Dahno amechanganya mbinu za kutumia katuni na ucheshi sambamba na muziki mzuri. Kipande hiki kinasumulia namna Wakulima watatu wa Kirusi wanaojaribu kuwafuatilia wahuni wanaoteka watoto katika nchi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na zile zinazoaminika kuongoza kwa vitendo hivi yaani, Ugiriki, Misri na India. Maongezi hayajapewa nafasi zaidi ya vitendo, kufanya iweze kuwafaa watazamaji wa nchi zote na umri wowote.

Kama unapenda kipande hiki basi wawezi kutazama kwa kutumia orodha iliyopo kwenye tovuti ya UA Post:  katuni 10 za ki-Ukraini zinazoweza kuwafanya wanao wakawa werevu zaidi [7].