Je, Waziri Mkuu wa Malaysia Ndiye Mhusika Mkuu wa Kashfa ya Ufisadi wa Dola Bilioni Iliyotajwa na Marekani?

This 'Malaysian Official 1' meme adopts the logo of 1Malaysia, a program of Prime Minister Najib Razak. Source: Facebook

Huu ni ujumbe unaosambazwa kwenye mitandao kwa jina la ‘Afisa wa Malaysia 1′ ukiwa na nembo ya 1Malaysia, mradi wa Waziri Mkuua Najib Razak. Chanzo: Facebook

Baada ya Wizara ya Sheria ya Marekani kufungua mashitaka mashtaka wakiwatuhumu maafisa wa Malayasia na wasaidizi wao kwa kutakatisha zaidi ya dola bilioni moja za marekani kupitia taasisi za ki-Marekani, wa-Malaysia wanahoji kama mtu aliyepachikwa jina la ‘Afisa wa Malaysia 1,’ anayeonekana mara 36 kwenye hati ya mashitaka yenye kurasa 136, ni waziri mkuu Najib Razak.

Waziri Mkuu anaendesha Mradi wa kampuni ya uwekezaji wa Kimaendeleo ya 1Malaysian Berhad (1MDB), ambao ndio hasa kiini cha shitaka hilo. Mtoto wake wa kambo ni moja wapo wa watuhumiwa. Mashataka hayo yanalenga kunyang'anywa mali zipatazo 17 nchini Marekani, ambazo zinadaiwa kupatikana kwa fedha za mradi wa 1MDB. Shitaka hilo linadai fedha hizo zilitumiwa na mradi huo kwa ajili ya hoteli, sanaa, makazi ya kifahari kwenye majiji ya New York, Los Angeles, na London, na hata kwenye filamu ya 2013 ya Hollywood iitwayo “The Wolf of Wall Street.”

Hii si mara ya kwanza kwa jina la Najib Razak kuhusishwa na kashfa za ufisadi. Kipindi cha nyuma, waziri mkuu alituhumiwa kujipatia fedha zaidi ya dola milioni 600 kupitia miamala isiyoeleweka. Baada ya kuhusishwa na akaunti kadhaa kubwa zenye kutumia dola, alidai fedha hizo zilikuwa michango ya kisiasa kutoka kwenye familia ya ki-Falme nchini Saudi Arabia.

Maafisa wa Marekani walisema shtaka hilo ni “hatua kubwa zaidi kuwahi kuchukuliwa chini ya Mpango wa Kuokoa Mali wa Kleptocracy.” Waliapa kurudisha fedha hizo kwa watu wa Malaysia:

Idara ya ya Sheria haitaruhusu mfumo wa fedha wa Marekani utumike kufanya vitendo vya kifisadi. Kwa hatua hizi, tunatafuta kunyang'anya na kurudisha fedha hizo zilizokuwa zimelengwa kukuza uchumi wa Malyasia na kuwaidia watu wa Malaysia. Badala yake, wameibiwa, kutapeliwa kupitia taasisi za ki-Marekani na kuwawezesha vigogo wachache kujitajirisha na marafiki zao.

raia wengi wa Malaysia wanaamini maandishi yanayoonekana kwenye shitaka hiyo ni ushahidi tosha dhidi ya Najib.

Sioni namna gani huyu anayeitwa AFISA WA MALAYSIA1 anaweza kuwa mtu mwingine zaidi ya Najib kwenye shitaka hili la Wizara ya Sheria ya Marekani kwenye kashafa hii

Kwa nini ni vigumu kumpata mtu huyu?

Waziri Mkuu wa Zamani Mahathir Mohamad, anayemtaka Najib ajiuzulu, aliiomba Marekani kumtaja Najib kwenye sitaka hilo:

Kama Marekani inaamini kwa dhati kabisa katika kuukomesha ufisadi na utakatishaji wa fedha haramu unaoihusisha nchi yao, lazima wawe majasiri na kutaja majina ya wahusika na kuruhusu taratibu za kisheria kufanyika.

Mwizi anapokuwa mkuu wa polisi na idara za mashataka, hapo tunahitaji msaada wa nchi za kigeni kuhakikisha haki inapatikana.

Mbunge Lim Kit Siang alimsauri Najib kujibu tuhuma hizo kwamba yeye ndiye ‘Afisa wa Malaysia1′ aliyetajwa kwenye shitaka hilo:

Naomba rasmi nitangaze wazi kwamba mimi sio “Afisa wa Malaysia1.”

je, Waziri Mkuu, Datuk Seri Najib Razak atasema msimamo wake – kukanusha rasmi au kuthibitisha kwamba yeye ndiye anayetajwa kwa jina la “Afisa wa Malaysia 1” na kama ni kweli, anapendekeza hatua gani zichukuliwe.

Kambi ya Najib inasisitiza kwamba jina la waziri mkuu halipo kwenye mashtaka hayo, ikiwa na maana kwamba hakuna msingi wa kumtuhumu waziri mkuu kwa ufisadi unaotajwa kwenye kashfa hiyo ya 1MDB.

Wanaomwunga mkono Najib kwa sehemu wanakiri kwamba “Afisa wa Malaysia1” anaweza kuwa waziri mkuu lakini wanadai taarifa zinazotolewa na serikali ya Marekani si sahihi.

ALama ishara ya #MalaysianOfficial1 imekuwa maarufu baada ya watumiaji wa mtandao kupata habari za taarifa ya Wizara ya Sheria ya marekani. Baadhi ya watumiaji wa mtandao wameanzisha kampeni ya kuwaomba watumiaji wengine wa mtandao kumtafuta ‘Afisa wa Malaysia1’ halisi.

Ninaheshimu nafasi ya Waziri Mkuu lakini nimepoteza heshima yangu kwa mtu aliyeshikilia madaraka hayo kwa sasa

Nina hasira kwamba fedha za wananchi zinatumiwa kama vile ni za mtu binafsi. Hazira yangu inakuwa kali kwa sababu huyu ‘Afisa wa Malaysia1′ hakamatiki hapa

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.