- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Hiyo Ndiyo Sababu ya Google Kubadili Majina ya Baadhi ya Miji ya Crimea—na Sasa Inarudisha Majina ya Awali

Mada za Habari: Ulaya Mashariki na Kati, Ukraine, Urusi, Siasa, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vita na Migogoro, RuNet Echo
As if by magic, Google Maps changed some town names in Crimea overnight. Images edited by Tetyana Lokot. [1]

Kama vile ni miujiza, Ramani za Google zilibadili ghafla baadhi ya majina ya miji kwenye pwani ya Crimea. Picha zimehaririwa na Tetyana Lokot.

Mnamo Julai 27, Google ambao ndio mtandao mkubwa zaidi kwenye intaneti ilibadili majina ya baadhi ya miji, vijiji na mitaa ya Crimea -peninsula ya Ukraine ambayo imekuwa ikitawaliwa na Urusi tangu mapema 2014 —kwa kutumia huduma yake ya Ramani za Google. Mabadiliko hayo yalikuja baada ya bunge la Ukraine kubadili majina ya maeneo ya kijiografia yapatayo 70 kwa mujibu wa kampeni ya “kupambana na ukomunisti” mwezi Mei 2016.

Watumiaji wa Ramani za Google kwa ki-Rusi na ki-Ukraine waligundua mabadiliko hayo mara moja. Kwa mfano, kwa mujibu wa taarifa [2] iliyoandikwa na tovuti ya habari ya Meduza, mji wa Krasnoperekopsk ulibadilika kuwa “Yany Kapu,” Sovetskoe ukawa “Ichki,” na Kirovskoe ulibadilishwa kuwa “Islyam-Terek.” Majina mengi mapya yalikuwa na asili ya lugha ya ki-Crimea Tatari na historia nyinginezo, na kuodnoa majina yaliyokuwa na asili ya ki- Soviet.

Mabadiliko ya Ramani za Google yalichokoza hasira za maafisa wa Urusi na Crimea. Mkuu wa Crimea Sergey Aksyonov aliituhumu Google kwa bandiko la facebook [3] “lililotengenezwa na wafanya propaganda” na kwa “kujaribu kutengeneza ukweli wanaouona wao.” Waziri wa mawasiliano nchini urusi Nikolay Nikiforov pia aliungana na Sergey [4] kukosoa mabadiliko hayo, akisema kwamba kama Google haitaheshimu sheria za Urusi na majina ya Urusi kwa miji na vijiji (huko Crimea), basi “ingeizuia kampuni hiyo kufanya biashara nchini Urusi.”

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ukraine Pavlo Klimkin alijibu maneno hayo kwneye mtandao wa twita, akirejea kile ambacho Ukraine inakiamini kuwa kukaliwa isivyo halali kwa Crimea na Urusi:

Kubadili majina ya sehemu zilizoibwa ni kucheza bahati nasibu: hatua hiyo itashindwa na ukweli

Mnamo Julai 28, msemaji wa Google aliiambia [7] tovuti ya habari ya RBC kwamba walikuwa wanafahamu kwamba mabadiliko ya majina hayo yalifanyika kwamujibu wa sheria ya “kuachana na ukomunisti” ya Ukraine na hatua ambayo Urusi hawaifurahii. Google iliiambia RBC kwmaba walikuwa “wanafanya kazi kwa bidii kurudisha majina ya zamani kwenye toleo la Ramani za Google kwa ki-Rusi.”

Serikali ya Ukraine imepoteza udhibiti wa peninsula ya Crimea kwenye msimu wa masika ya 2014, kufuatia kura ya maoni iliyoamua kujitenga kwa eneo hilo kutoka Ukraine na kujiunga na Shirikisho la Urusi. Jumuiya ya Kimataifa haiitambui hatua hiyo ya Urusi kuichukua Crimea. Crimea.