Wa-Belarusi Waamua Kuchapa Kazi Wakiwa Uchi (Kutii Wito wa Rais)

Belarusian Internet users stripped in their workplaces to respond to the President's call to put more effort into their work. Image from Instagram.

Watumiaji wa mtandao wa intaneti wa ki-Belarusi waliamua kuvua nguo zao wakiwa kazini kutii wito wa Rais wa kuongeza bidii kwa kazi zao. Picha kutoka mtandao wa Instagram.

Wananchi wa Belarusia hawana kawaida ya kutii amri za rais wao aliyedumu madarakani kwa kuda mrefu, Alyaksandr Lukashenka. Kwa hakika, utawala wake wa kiimla nchini humo unaokosolewa sana. Lakini inavyoonekana, kila sheria ina mazingira fulani ya kukiukwa.

Mnamo Juni 22, Lukashenka alizungumza kwenye mkutano unaofahamika kama ‘Wa-Belarusi Wote’, na alimalizia hotuba yake kwa kuwataka wananchi wote kujibidiisha katika kujitafutia maisha bora.

Наша жизнь в простом. Надо раздеваться и работать. До седьмого пота. Не будет этого – погибнем.

Maisha yetu yanahusu mambo rahisi na ya kawaida. Lazima tuvue nguo tuchape kazi. Tuchape kazi hata jasho litutoke. Tusipofanya hivyo, ndugu zangu tutapotea.

Video ya hotuba ya Lukashenka imesambaa sana kwenye mitandao ya kijamii, huku watumiaji wa mitandao hiyo wasioamini kama kwenye Rais aliyatamka maneno hayo na kujaribu kuthibitisha kama kweli Rais alitumia neno “kuvua nguo” (раздеваться) na sio neno jingine lenye matamshi kama hayo lenye maana ya “ku[ji]endeleza” (развиваться).

Lakinihotuba iliyoandikwa na kuwekwa kwenye tovuti ya ikulu ya nchi hiyo inathibitisha kwamba kweli Rais alimaanisha wananchi wavue nguo. Kwa hiyo wananchi wakaamua kweli kutekeleza agizo hilo.

Punde, mitandao ya kijamii ikafurika picha na video (nyingi zikiwa za vijana) wa ki-Belarusi wakiwa maofisini na makazini, uchi, huku wakifunika kidogo sehemu zao za siri kwa meza, kompyuta mpakato, na vifaa vingine na kuonekana wakiendelea na kazi zao. Tovuti ya habari nchini humo iitwayo CityDog ilikusanya baadhi ya picha hizo kwenye mitandao ya kijamii.

#раздеватьсяиработать #ялюблюсвоюработу #чутьчтомыодеты #четкаяконспирация #minsk

A photo posted by Маргарита Воропаева (@margo_voropaeva) on

Batka (jina la utani la Lukashenko) alisema tuvue nguo tufanye kazi, kwa hiyo tumeamua kubaki uchi tuchape kazi.

Tunazingatia ushauri wa Rais))

Tunafanya lolote liwezekanalo kukuza uchumi wa nchi.

Maelfu ya wa-Belarusi wameweka picha kwenye mitandao ya Instagram, Facebook, na Twitter kwa kutumia alama ishara ya #раздеватьсяиработать (#vuanguofanyakazi).

#раздеватьсяиработать #музейбровки #ниднябезбровки #музей

A photo posted by Музей Петруся Броўкі (@museum_brovka) on

Nilichuma matunda leo. Nikajiuliza nawezaje kutekeleza amri ya Rais?

Vituko vya picha hizo vilishika kasi kiasi cha kuwavutia watumiaji wa mtandao katika nchi nyingine Urusi kushiriki.

Tunaunga mkono harakati za wa-Belarusi!

Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa intaneti walikwenda hatua kadhaa mbele na kuweka video za nyimbo zilizotungwa mahususi kwa wakati huo. Kwenye video hizo, wananchi wanaimba wakiwa karibia na uchi. Hatua hiyo inaonekana kutuma ujumbe kwamba viongozi wa nchi wnaahitaji kuwa makini na kile wanachokitamka hadharani.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.