Ubaguzi wa India kwa Waafrika Waibuka Tena Baada ya m-Kongo Kuuawa kwa Kupigwa

A lynch mob mercilessly beat three Nigerian students in Delhi and they could not save themselves after fleeing inside a police booth. Screenshot from Video "No Country For Black Men"

Kikundi cha wahuni kikiwapiga wanafunzi watatu wa ki-Nijeria jijini Delhi mwaka 2014. Picha ya video “No Country For Black Men”(Hakuna Nchi Inayowafaa Weusi)

Majuma machache yaliyopita, Masonga Kitanda Olivier, mwenye miaka 23 kutoka Kongo (DRC) aliuawa kwa kupigwa na wanaume watatu kwenye eneo la Vasant Kunj Kusini mwa Delhi. Olivier alihamia India kwa ajili ya masomo ya chuo kikuu na alikuwa ameanza kufundisha Kifaransa kwenye taasisi moja binafsi. Watu hao waliompiga wanadaiwa kusukumwa na hisia za ubaguzi wa rangi kwa sababu walimtukana.

Hili halikuwa tukio la kwanza la ukatili dhidi ya Waafrika wanaoishi nchini India. Mnamo Mei 25, mwanafunzi wa Naijeria, Bamilola Kazim mwenye miaka 26, alipigwa kwa nondo baada ya kutokea kutokuelewana kuhusiana na eneo la maegesho kwenye jiji la Hyderabad. Alitibiwa kwenye hospitali moja na kuruhusiwa.

Mwezi Januari, mwanamke wa ki-Tanzania mwenye miaka 21 anayesoma India alipigwa, kuvuliwa nguo na kutembezwa akiwa uchi kwenye mitaa ya jiji la Bangalore na wahuni kwa sababu walidhani gari lake lilikuwa limemgonga na kumwua mwanamke mmoja. Marafiki zake watatu nao walidhalilishwa na gari walilokuwa nalo liliteketezwa kwa moto. Baada ya hayo, wahuni hao walikwenda kwenye nyumba ambazo wanafunzi wa ki-Afrika huishi na kuwafanyia vurugu.

Katika kipindi chote cha  miaka ya hivi karibuni, mashambulio kama hayo yakiwalenga raia wa ki-Afrika na watu wenye asili ya Afrika  yameendela kugonga vichwa vya habari. Je, matukio hayo yanamaanisha India inalo tatizo la ubaguzi wa rangi dhidi ya wa-Afrika?

Jibu ni hapana kama utamwuuliza waziri wa Mambo ya Kigeni wa India Sushma Swaraj, ambaye alikataa kukubali kuwa mauaji ya Masonga Kitanda Olivier yalisukumwa na hisia za ubaguzi wa rangi. Swaraj alisisitiza kuwa udhalilishaji huo ulikuwa na chembechembe za kimatabaka na kudai kwamba kusema suala hilo lilikuwa ni ubaguzi wa rangi isingekuwa haki kwa wa-Hindi, ambao kwa ujumla wanaamini katika undugu na umoja.

Ningependa niwahakikishie wanafunzi wa ki-Afrika kwamba tukio hili baya na lisilotarajiwa limesababishwa na wahuni wa eneo husika

Swaraj aingia kwenye mtandao wa Twita kuwasihi wa-Hindi kuwaambia wa-Afrika kuwa India inawapenda  na wawashike mikono. Hata hivyo, watu wengi walichukulia matamshi hayo kama kutokuelewa hali halisi au basi unafiki, kwa kuangalia matukio ya udhalilishaji wa hivi karibuni uliofanywa dhidi ya wa-Afrika pamoja na ubaguzi unaoendelea kwenye sekta nyinginezo katika jamii ya wa-Hindi.

Hata baada ya miaka 70 ya Uhuru, hatuwezi kuwafanya wa-Hindi wapendane, na wanatutaka tuwaambie wa-Afrika eti tunawapenda

Labda tuangalie namna bora ya kuongeza uelewa wa jambo hili na sio kutazama mambo kujuu juu. Hata hivyo, haki zisitegemee upendo

Mimi: India inakupenda
Raia wa ki-Afrika: Afrika si nchi

Afadhali hata hivyo. Wasihi wa-Hindi wenzako wasiwe wabaguzi wa rangi na wasichukie wageni. Hebu tubadilishe utambulisho wetu

Sema, “India inakupenda,” kwa wa-Islamu, wa-Daliti, wa-afrika, wasio na dini…na kisha rudi ukawapige makofi?

Hata hivyo, watumiaji wachache kwenye mtandao wa Twita wanaonekana kufikiri wazo la mhe Waziri ni zuri.

Nimejaribu kwa jamaa mmoja wa ki-Kenya na alifurahi…aliniambia namna gani wa-Hindi wengi wanafanya akzi Kenya na namna wanavyoheshimiwa na nikajisikia vizuri

Kwa ndugu zangu wa-Afrika,
India nakupenda

‘Mabaki ya Imani za Kikoloni kwa wa-Afrika’ bado Yangalipo

Wa-afrika na serikali zao hawajabaki kimya kufuatia mashambulio ya hivi karibuni. Al Jazeera iliripoti kwamba kikundi cha mabalozi wa ki-Afrika kimeungana na kutoa kauli ya pamoja kwa niaba ya wananchi wao waishio India, ambao wanaamini wanaishi kwenye “Mazingira ya hofu na kukosekana usalama” baada ya mashambulio hayo dhidi ya wa-Afrika. Wameonya kwamba kama mashambulio hayo yataendelea na waliohusika wakaruhusiwa kuponyoka mkono wa sheria, wataziomba serikali zao kuacha kuwaruhusu wanafunzi kwenda India.

Hii si mara ya kwanza kwa suala hili kuwasumbua wanadiplomasia wa Afrika, hata hivyo. Mwaka 2015, kabla ya mkutano wa tatu wa Jukwaa la Ushirikiano wa India na Afrika, mabalozi wa ki-Afrika jijini Delhi walidaiwa kutaka kususia  maadhimisho ya Siku ya Afrika, ilikuwa imeandaliwana Baraza la Mahusiano ya Kiutamaduni la India jijini Delhi, kwa madai ya chuki dhidi ya wageni wanaoyokabiliana nayo raia wa Afrika wanaoishi India.

Mabalozi 40 nusra wasusie Siku ya Afrika
Waafrika wameenda kwenye vyombo vya habari kulaani ubaguzi wa rangi unaofanywa India
Na waziri analaumu vyombo vya habari
Yaliyosema yametosha

Baadhi ya wa-Afrika wameandika kuhusu visa vya ubaguzi wa rangi unaofanyika kwenye vyombo vya habari. Katika makala ya Juni 4 iliyoandikwa kwenye tovuti ya Scroll.in, mwanafunzi wa Afrika Kusini mwenye asili ya Asia Kusini alizungumzia namna moja ya imani za kibaguzi na kiutamaduni zinazoonekana nchini India:

Ni kawaida kwa wanafunzi wengi hapa kuzungumza na mimi, mazungumzo ambayo wao huyachukulia kwa uzito, kuhusu Afrika na wa-Afrika, hujikita kwenye imani za kikoloni kwa wa-Afrika kama watu wanaothamini asili, wanaoongea kwa bashasha au hata, kwamtazamo wa jumla, kuwa ni watu wenye uume mkubwa. Wakati wanafunzi wengi chuoni kwangu wanaonekana kuwa na uelewa mkubwa wa historia yao ya ukoloni, uhuru, utamaduni wa baada ya uhuru, siasa, masuala ya kijamii na kidini, pamoja na uelewa wa nadharia na falsafa za kimagharibi, na wengi huwa na mitazamo ya siasa za mrengo wa kushoto kama zile zinazothamini sana umoja wa Kusini-Kusini, lakini uelewa wao wa historia ya Afrika kijamii, kisiasa na kiutamaduni pamoja na hali halisi ya sasa ulikuwa mdogo.

Kumekuwa na maadamano pia. Kwa mfano, baada ya mauaji ya Obodo Uzoma Simeon, raia wa Naijeria mwenye miaka 36, nje ya mgahawa wa ki-Afrika jimboni Goa mwaka 2013, zaidi ya wa-Naijeria 50 walifunga barabara kuu. Walisimamisha msafara wa msiba uliokuwa unasafirisha mwili wa Simeon na kuburuta mwili wake barabarani kama namna ya kuvuta hisia za watu kwa suala hilo na kuzuia kufichwa kwa mauaji hayo.

Mamlaka za serikali, hata hivyo, zilijibu maandamano hayo kwa kuendesha zoezi la kuwafukuza wa-Naijeria waliokuwa wakiishi bila kufuata taratibu, zoezi ambalo lilionekana kama kukuza na kufanya hisia za ubaguzi dhidi ya wa-Afrika zionekane wazi zaidi. Hisia mbaya ziliendelea baada ya mauaji ya Masonga Kitanda Olivier. Akijibu madai ya tuhuma za ubakaji unaodaiwa kufanywa na raia wa Naijeria, waziri wa utalii wa jimbo la Goa aliwatuhumu wa-Naijeria hadharani kwa kufanya vitendo vya kiuhalisi kwa lengo ya kuongeza muda wa kuishi nchini India. “Lazima tuwe makini kusimamia sheria ili tuweze kuwafukuza. Lakini ni bahati mbaya hatuna sheria kama hiyo nchini India kwa sasa,” alisema.

Upo wasiwasi kwamba mwendelezo wa mashambulizi kwa wa-Afrika umeichafua sifa ya India mbele ya jumuiya ya kimataifa na umetikisa uhusiano wa nchi hiyo na nchi za ki-Afrika. Katika jitihada za kusafisha sura hiyo, Sushma Swaraj has amewahakikishia mabalozi wa ki-Afrika na watu wengine nchini India kuwa hatua stahiki zitachukuliwa. Kundi la wanafunzi wa ki-afrika liliahirisha maandano kwenye mji mkuu wa nchi hiyo kuitikia wito huo.

Huenda, nchi hiyo itarudi mapema kwenye njia ya kuwahihikishia amani na usalama wa-Afrika na jamii nyingine za wageni nchini India.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.