Raia Mwingine wa Tanzania Asomewa Mashtaka kwa Ujumbe wa Whatsapp ‘Unaomtukana’ Rais

Statement of offence shared on Twitter by @samirasawlani.

Hati ya mashitaka iliyowekwa kwenye mtandao wa Twita na @samirasawlani.

Raia wa Tanzania Leonard Mulokozi amesimamishwa kizimbani mnamo Juni 22 chini ya Sheria ya nchi hiyo ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta kwa kosa la ujumbe wa WhatsApp ambao mamlaka zinasema ulikusudia ‘kumtukana’ rais wa nchi hiyo, John Magufuli. Mulokozi amekana mashtaka yake kwneye mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu na tuko nje kwa dhamana. Kesi iyo itatajwa tena Julai 18.

Inadaiwa kwamba mnamo Juni 2 Mulokozi alituma ujumbe ufuatao kwenye mtandao wa WhatsApp:

Hivi huyu Pombe nd'o kwamba hana washauri? Hashauriki? Au ni zuzu? Bwege sana huyu jamaa; he doesn't consider the law in the place before opening his mouth au na yeye anaumwa ugonjwa wa Mnyika?

(Maneno ya Kiingereza yanasema): haheshimu sheria zilizopo kabla ya kufungua mdomo wake

Mulokozi ni mhanga wa hivi karibuni zaidi wa Sheria ya Makosa ya Mtandao nchini humo, iliyopitishwa na Bunge Aprili 2015 kushugulikia masuala kama picha za ngono kwa watoto, udhalilishwaji wa mtandaoni, matumizi mabaya ya taarifa za watu, kuingilia mawasiliano ya watu isiyo halali, na kuchapisha taarifa za uongo.

Pamoja na upinzani mkubwa kutoka kwa wanasiasa, wataalam wa mitandao ya kijamii, na wanaharakati wa haki za binadamu, muswada huo ulipelekwa haraka bungeni baada ya majadiliano au mdahalo wa kiwango cha chini. Rais mstaafu Jakaya Kikwete aliusaini muswada huo mnamo Mei 2015 kuwa sheria.

Wanaopinga Sheria ya Makosa ya Mtandao wanasema kwamba sheria hiyo inawapa mamlaka makubwa — bila udhibiti wowote– polisi, ukiwapa uwezo wa kupekua nyumba za wanaotuhumiwa kuvunja sheria hiyo, kukamata vifaa vya kielektroniki, na kudai taarifa-pepe (data) kutoka kwenye makampuni yanayotoa huduma za mtandao wa intaneti. Wanaonya kwamba polisi au dola inaweza kutumia mamlaka hayo kuwabughudhi wanaharakati wa mtandnaoni au watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Mwananchi mwingine wa Tanzania Isaac Abakuki Emily alihukumiwa mwezi huu kwa kosa la kumtukana Rais wa Tanzania John Magufuli kwenye ukurasa wake wa Facebook na Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Arusha.

Emily anaweza kwenda jela miaka mitatu, au kulipa faini ya shilingi milioni tano za Tanzania (Dola za Marekani $2300), ambacho ni kiasi kikubwa sana nchini Tanzania, ambapo Wastani wa Pato la Mwananchi ni chini ya Dola za Marekani $1000 . Kiasi hiki kilipunguzwa kutoka milioni saba kwa rufaa ya mwanasheria wake, kwa mujibu wa tovuti ya habari nchini humo iitwayo The Citizen. Lazima alipe faini hiyo ifikapo mwezi Agosti 8, vinginevyo atalazimika kutumikia kifungo.

Mwezi Oktoba 2015, wa-Tanzania wawili walikuwa wahanga wa kwanza wa sheria hiyo mpya. Benedict Angelo Ngonyani, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 24 katika Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam, alishitakiwa kwa kuchapisha maudhui ambayo “ni ya uongo au hayajathibitishwa na mamlaka zinazohusika.” Inadaiwa kwamba alichapisha bandiko la Facebook lililodai kwamba Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange, alikuwa amelazwa kwa sababu alikuwa amekula chakula chenye sumu.

Mwezi Novemba 2015, wa-Tanzania wengine wanne — Leila Sinare, Godfrey Soka, Deo Soka na Monica Gaspary Soka — walishitakiwa chini ya kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya 2015 kwa kuchapisha taarifa za uongo za kielektroniki kwenye mtandao wa kuandikiana ujumbe mfupi uitwao WhatsApp. Wanne haoa walisimamishwa mbele ya Hakimu Mkazi jijini Dar Es Salaam mnamo Novemba 6, 2015. Mwendesha mashtaka wa serikali alidai kwamba watuhumiwa hao walichapisha taarifa ya sauti kwenye kundi la WhatsApp linaloitwa “Soka Group”, ambayo ilikusudia kupotosha umma wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015 nchini Tanzania , ambao uligubikwa na madai ya wizi wa kura.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.