- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mwanaume wa Uganda Aswekwa Rumande kwa Kuvaa Tisheti Yenye Picha ya Kiongozi wa Chama cha Upinzani

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Uganda, Haki za Binadamu, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia
Screen Shot 2016-05-30 at 12.02.17 PM

Picha ya posti ya ukurasa wa Facebook wa Samson Tusiime

Kuanzia jumapili ya tarehe 29 Mei katika mtandao wa Twitter nchini Uganda kumekuwa na mzizimo wa  kampeni zenye hastag #mfungulieniSamwyiri [1]. Kampeni hizi zimefuatia kukamatwa kwa mwanaume wa Kiganda anayeitwa Samson Tusiime [2] aliyekamatwa kwa kuvaa na kugawa tisheti zenye picha za kiongozi wa chama cha upinzani wa huko Uganda Kizza Besigye.

Polisi nchini Uganda wanadai kuwa mwanaume huyo alikuwa anaandaa maandamano haramu na alikuwa na mpango wa kuzigawa tisheti hizo nchi nzima. Gazeti  la Uhuru la Uganda, linasema kuwa Waganda wengine wawili ambao walifahamika kwa majina ya Ismail Muyinda na Asia Nanyanzi, nao pia walikamatwa.

Tarehe 28 Mei Tusiime aliweka ujumbe  katika ukurasa wake wa Facebook unaosema kuwa anamtafuta rafiki yake Ysmyl Muyinda [3] akiwa amevaa tisheti hiyo anayoshutumiwa nayo (Inasadikiwa kuwa ndie Ismail Muyinda [3]aliyetajwa hapo juu kuwa alikamatwa) Ismail ndie mmiliki wa kampuni iliyozalisha na kuchapisha tisheti hizo. Tusiime aliandika kuwa ameenda katika vituo mbalimbai vya polisi akimtafuta rafiki yake. Baada ya marafiki wengine kugundua kuwa hata Tusiime naye haonekani pia, walianzisha hashtag #MfungueniSamwyiri [1]. Baadae polisi walithibitisha  [4] kuwa alikuwa amekamatwa.

Kesi hii imewashtua watu wengi nchini Uganda na wengi wameshangaa  kuwa kumbe hata tisheti tu inaweza kumfanya mtu akamatwe na kuwekwa rumande!? Mwana Blogu mmoja wa huko Uganda aitwae Joel Nevender amewauliza polisi kuwa;

Mnamkamata @Samwyri [5] kwa sabau ameutumia uhuru wake wa kujieleza? Kwa sababu ya Tisheti? Tisheti?

Wakati Ogutu Daudi alitwiti kwamba:

Je tunaweza kutoka na kusema kwa sauti kuwa hii sio demokrasia kwa sababu sio? Tisheti Upuuzi gani!? Kwa nini msituweke wote kwenye maovaroli ya njano sasa?

Miezi ya hivi karibuni mamlaka nchini Uganda imeshindwa kabisa kuvumilia kukosolewa. Mwezi wa pili mwaka huu 2016 Raisi Yoweri Museveni alishinda uchaguzi na kurudi madarakani kwa muhula wa tano. Uchaguzi huo uliokuwa na sintofahamu nyingi ambapo vyama vya upinzani nchini humo vimekuwa vikilalamikia matokeo ya uchaguzi huo kupindishwa au kuchakachuliwa. Viongozi wa upinzani na wanaharakati wengine nchini Uganda wamekuwa wakikosoa na kupinga ushindi wa Museveni kupitia maandamano mbalimbali…. “kampeni za kususia” [9]

Tangu uchaguzi uishe mwezi Februari, mamlaka imemkamata na kumsweka rumande mara kadhaa Kizza Besigye na viongozi wengine wa upinzani pamoja na kufungia [10] mitandao ya kijamii mara mbili kwa masilahi ya “usalama wa taifa” [11].

Baada ya kukamatwa kwaTusiime, Josephine Karungi alishangaa na kusema :

Kuna vitu havijakaa sawa kabisa…ati tumemweka rumande sasa kisa ni nini……..kweli hamuwezi kusema eti kisa ni tisheti tu…mnaweza kusema ndivyo?

Patoraking, yeye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu alisema kuwa hiki kitendo ni kibaya kuliko enzi za dikteta Idi Amini aliyeitawala Uganda tangu mwaka 1971 hadi 1979.

Wazazi wetu hawawezi hata kutuambia tena “enzi za Idi Amini………..” kwa sababu kipindi hiki tuko katika nyakati mbaya zaidi kuliko hata zile za Idi Amini.

Shirika la msaada wa kisheria liitwalo Chapter Four Uganda, liliitikia vuguvugu la kampeni hiyo kwa kupeleka timu ya wanasheria katika kituo cha polisi:

Afisa wetu yuko SIU Kireka kuchukua maelezo kutoka kwa @Samwyri [5] ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa

SIU Kireka ni kifupi cha (Special Investigation Unit at Kireka) yaani ni Kitengo Maalum cha Upelelezi katika eneo la Kireka katika mji mkuu wa Kampala.

Haijajulikana ni mashataka yapi hasa yamefunguliwa dhidi yake; hata hivyo, mwandishi wa habari wa Uganda Qatahar Raymond amekuwa akiifuatilia kwa ukaribu kabisa kesi hii ya Tusiime tangu akamatwe na anadhani kuwa Tusiime anaweza kushtakiwa kwa kosa la kuchochea vurugu.

Tumegundua kuwa @Samwyri na marafiki zake wanaweza kushtakiwa kwa kosa la ” uchochezi”