Mwanaume wa Tanzania Ahukumiwa Kifungo cha Miaka Mitatu Jela kwa “Kumtukana” Rais kwenye Mtandao wa Facebook

Image shared on Twitter by Tanzanian Member of Parliament Zitto Kabwe Ruyagwa. (@zittokabwe)

Picha iliwekwa kwenye mtandao wa Twita na Mbunge wa Tanzania Zitto Kabwe Ruyagwa. (@zittokabwe)

Raia wa Tanzania Isaac Abakuki Emily alipatwa na hatia ya kumtukana Rais wa Tanzania John Magufuli kwenye ukurasa wake wa Facebook na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Arusha.

Emily anaweza kwenda jela kwa miaka mitatu, au kulipa faini ya shilingi milioni tano (Dola la Marekani $2300), kiwango kikubwa sana nchini tanzania, ambapo wastani wa pato la mwaka (GDP) ni chini yaDola za Marekani $1000 kwa mwaka. Faini hii ilipunguzwa kutoka milioni saba baada ya maombi ya mwanasheria wake, kwa mujibu wa tovuti ya chombo kimoja cha habari nchini humo The Citizen. Lazima alipe faini hiyo ifikapo Agosti 8, au akatumikie kifungo chake jela.

Emily alisimama mbele ya mahakama kwa mara ya kwanza mnamo Aprili 15, 2016 kujibu mashtaka y ‘kumtukana’ rais wa nchi, John Magufuli, ikidaiwa kuwa alikwenda kinyume na Ibara ya 16 ya Sheria ya Makosa ya Jinai ya Tanzania Na. 14 ya 2015, inayosema:

Mtu yeyote anayechapisha taarifa, takwimu au habari katika picha, maandishi, alama au kwa namna nyingine yoyote katika mfumo wa kompyuta ambapo taarifa hizo, takwimu au habari hizo ni za uongo, zenye udanganyifu, zenye kupotosha ukweli au zisizo sahihi atakuwa anatenda kosa, na akitiwa hatiani atatakiwa kulipa fidia ya si chini ya shilingi milioni tatu kifungo jela kisichopungua miezi sita jela au vyote viwili kwa pamoja

Emily anadaiwa kuweka ujumbe wenye utata kwenye ukurasa wake wa Facebook, ulioandikwa kwa Kiswahili, mnamo Machi 17, 2016, wakati akijua kuwa kuchapisha kauli za uongo au zinazopotosha ukweli kuhusu rais wa nchi ni kinyume cha sheria. Maoni yake hayo yalihusiana na hatua ya Rais Magufuli kupiga simu isiyotarajiwa kwa kipindi cha 360, kinachohusiana na mambo yanayotokea kwenye kituo cha televisheni cha Clouds TV. Wangali hewani, rais aliwashukuru watangazaji na kuonesha alivyoshabiki wa kipindi hicho.

Emily anadaiwa kuchapisha ujumbe wenye utata kwenye mtandao wa Facebook kwa lugha ya Kiswahili mnamo Machi 17, 2015, hali akijua kwamba kumkosoa rais wa nchi ni kinyume cha sheria. Maoni yake hayo kwenye mtandao wa facebook yalihusu kitendo cha Rais Magufuli kupiga simu isiyotarajiwa kwenye kipindi kinachooneshwa na kituo cha televisheni cha Clouds TV kinachohusu habari zinazojiri kiitwacho 360. Rais alitumia kipindi hicho kuwashukuru watangazaji wa kipindi hicho na kuonesha alivyo shabiki wa kipindi hicho.

Hizi siasa za maigizo, halafu mnamfananisha huyu bwege and Nyerere wapi buana.

Hukumu yake imekuja wakati muswada mpya wa makosa ya uhalifu wa kimtandao, uliopitishwa mnamo april 1, 2015, ulipotungwa kushughulikia masuala ya kimtandao kama vile picha za ngono za watoto, udhalilishaji wa kimtandao, matumizi ya taarifa za watu isivyosahihi, uzalishaji wa maudhui yanayochochea ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa wageni, ujumbe unaoutumwa bila ruhusa yake, udukuzi wa mawasiliano kinyume na sheria, na kuchapishwa kwa taarifa za uongo.

Pamoja na upinzani mkubwa kutoka kwa wanasiasa, wataalam wa mitandao ya kijamii, na wanaharakati wa haki za binadamu, muswada huo ulipelekwa haraka bungeni baada ya majadiliano au mdahalo wa kiwango cha chini. Rais mstaafu Jakaya Kikwete aliusaini muswada huo mnamo Mei 2015 kuwa sheria.

Wanaopinga Sheria ya Makosa ya Mtandao wanasema kwamba sheria hiyo inawapa mamlaka makubwa — bila udhibiti wowote– polisi, ukiwapa uwezo wa kupekua nyumba za wanaotuhumiwa kuvunja sheria hiyo, kukamata vifaa vya kielektroniki, na kudai taarifa-pepe (data) kutoka kwenye makampuni yanayotoa huduma za mtandao wa intaneti. Wanaonya kwamba polisi au dola inaweza kutumia mamlaka hayo kuwabughudhi wanaharakati wa mtandnaoni au watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Mwezi Oktoba 2015, wa-Tanzania wawili walikuwa wahanga wa kwanza wa sheria hiyo mpya. Benedict Angelo Ngonyani, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 24 katika Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam, alishitakiwa kwa kuchapisha maudhui ambayo “ni ya uongo au hayajathibitishwa na mamlaka zinazohusika.” Inadaiwa kwamba alichapisha bandiko la Facebook lililodai kwamba Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange, alikuwa amelazwa kwa sababu alikuwa amekula chakula chenye sumu.

Mwezi huo huo, mtumiaji mwingine wa mtandao, Sospiter Jonas, alisimamishwa kizimbani kwenye mahakama ya mwanzo mkoani Dodoma kwa kosa la ‘kutumia vibaya mtandao’ baada ya kubandika ujumbe kwenye mtandao wa Facebook akisema Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda “atakuwa mhubiri wa dini.”

Mwezi Novemba 2015, wa-Tanzania wengine wanne — Leila Sinare, Godfrey Soka, Deo Soka na Monica Gaspary Soka — walishitakiwa chini ya kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya 2015 kwa kuchapisha taarifa za uongo za kielektroniki kwenye mtandao wa kuandikiana ujumbe mfupi uitwao WhatsApp. Wanne haoa walisimamishwa mbele ya Hakimu Mkazi jijini Dar Es Salaam mnamo Novemba 6, 2015. Mwendesha mashtaka wa serikali alidai kwamba watuhumiwa hao walichapisha taarifa ya sauti kwenye kundi la WhatsApp linaloitwa “Soka Group”, ambayo ilikusudia kupotosha umma wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015 nchini Tanzania , ambao uligubikwa na madai ya wizi wa kura.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.