Matangazo ya Sauti ya ‘Wiki Ilivyokwenda’ Global Voices: Mashujaa Wasiofahamika

Matangazo ya Sauti ya ‘Wiki Ilivyokwenda’ Global Voices: inaangazia baadhi ya habari ambazo tumezichapisha kwenye tovuti ya Global Voices.

Wiki hii, tunakuchukua mpaka Bosnia na Herzegovina, Japan na Myanmar. Aidha, tunazungumza na mhariri wa Global Voices Brazil,m Taisa Sganzerla kuhusu kesi ya ubakaji ambayo imeifanya Brazil na sehemu nyingine za dunia kupiga kelele na pia tutazungumza na mwandishi wetu Leila Nachawati Rego kuhusu riwaya yake inayoangazia maisha ya watu wanaoishi, wanaoipenda na kupambana kwa ajili ya Syria.

Shukrani nyingi kwa waandishi, watafsiri na wahariri wetu waliowezesha kipindi hiki kikafanikiwa. Kipidni cha leo kina habari zilizoandikwa na Filip StojanovskiNevin ThompsonMong Palatino, Fernanda Canofre na Taisa Sganzerla, na Firuzeh Shokooh Valle.

Kadhalika, tunakuburudisha na muziki wenye leseni ya Creative Commons kutoka maktaba ya matandaoni ya Free Music, ikiwemo Please Listen Carefully wa JahzaarMachine Elves wa Alan Singley; Looking For That Moment When Time Stands Still wa Will Bangs; All My Light wa Cory Gray; Shamon’s Roar wa Sergey Cheremisinov; na A Storm At Eilean Mor wa Jon Luc Hefferman.

Tarajia kusikia sauti zetu kwa mara nyingine katika kipindi cha majuma mawili. Tunakutakia usikilizaji mwema!

Picha kwenye alama ya SoundCloud imepigwa na Filip Stojanovski, CC BY.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.