- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Du! Kosa la Facebook Kugeuza Bendera ya Ufilipino Laifanya Nchi Ionekane iko kwenye ‘Hali ya Vita’

Mada za Habari: Asia Mashariki, Ufilipino, Historia, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vichekesho
Facebook joined Filipinos in celebrating the Philippine Independence Day. However, it unintentionally inverted the country's flag. [1]

Facebook iliungana na wa-Filipino kusherehekea Siku ya Uhuru wa Ufilipino. Hata hivyo, ilifanya kosa la kutokukusudia kwa kugeuza bendera ya nchi hiyo.

Juni 12 ni Siku ya Uhuru nchini Ufilipino. Ufilipino ilijitwalia uhuru wake kutoka nchi ya Uhispania mnamo Juni 12, 1898 baada ya zaidi ya miaka 300 ya ukoloni.

Katika kuenzi siku hiyo muhimu, Facebook iliwasalimu wa-Filipino kwa kuonesha bendera ya nchi yao. Hata hivyo, bendera hiyo ilikuwa imegeuzwa, kitendo ambacho kuashiria nchi hiyo iko vitani.

Gazeti la Star nchini humo lilibaini [1] haraka kosa hilo:

TAZAMA: Katika kuenzi Siku ya Uhuru wa Ufilipino, Ukurasa wa kwanza wa Facebook unawasalimu watumiaji wa mtandao wa Ufilipino kwa tangazo lenye bendera ya Ufilipino -bahati mbaya tu ni kwamba sehemu nyekundu ya bendera hiyo iko juu na bluu iko chini, kuonesha kwamba nchi iko vitani.

Kufuatia kosa hili, watumiaji wa mtandao wa Facebook nchini Ufilipino wanacheka ingawa wengi wanaishukuru Facebook kwa kuwatumia salamu za Siku ya Uhuru.

Hata hivyo, kuna watumiaji wa mtandao wanaoikosoa Facebook kwa kuweka bendera ya nchi yao kimakosa.

Hapa chini ni baadhi tu ya miitikio kwenye mtandao wa Facebook na Twita:

Mtumiaji wa Facebook, Berniemack Arellano aliuliza [2] kama kosa hilo ni ujanja wa kutangaza filamu:

Wapendwa Facebook,
Has the President and the Congress declared war on some country? Ano to, marketing ng Independence Day: Resurgence?

Wapendwa Facebook,
Je, Rais na Bunge limetangaza tunaingia kwenye vita na nchi fulani? Mmefanya nini, mnatangaza Filamu ya Siku ya Uhuru?

Facebook inasema tuko vitani. Heri ya Siku ya Uhuru, Ufilipino. Na tuwe huru kweli kweli.

Facebook: Bendera ionekane hivi na iwe Siku ya Uhuru. Kweli?

Hii ni namna sahihi ya kuonesha bendera ya Ufilipino. Katika historia ya nchi hiyo, sehemu nyekundu ilionekana [10] juu ya bluu wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia mwaka 1941 mpaka 1945.

Philippine flag. Image from the official website of the Philippine government [11]

Bendera ya Ufilipino. Picha kutoka tovuti ya serikali ya Ufilipino