Juni 12 ni Siku ya Uhuru nchini Ufilipino. Ufilipino ilijitwalia uhuru wake kutoka nchi ya Uhispania mnamo Juni 12, 1898 baada ya zaidi ya miaka 300 ya ukoloni.
Katika kuenzi siku hiyo muhimu, Facebook iliwasalimu wa-Filipino kwa kuonesha bendera ya nchi yao. Hata hivyo, bendera hiyo ilikuwa imegeuzwa, kitendo ambacho kuashiria nchi hiyo iko vitani.
Gazeti la Star nchini humo lilibaini haraka kosa hilo:
TAZAMA: Katika kuenzi Siku ya Uhuru wa Ufilipino, Ukurasa wa kwanza wa Facebook unawasalimu watumiaji wa mtandao wa Ufilipino kwa tangazo lenye bendera ya Ufilipino -bahati mbaya tu ni kwamba sehemu nyekundu ya bendera hiyo iko juu na bluu iko chini, kuonesha kwamba nchi iko vitani.
Kufuatia kosa hili, watumiaji wa mtandao wa Facebook nchini Ufilipino wanacheka ingawa wengi wanaishukuru Facebook kwa kuwatumia salamu za Siku ya Uhuru.
Hata hivyo, kuna watumiaji wa mtandao wanaoikosoa Facebook kwa kuweka bendera ya nchi yao kimakosa.
Hapa chini ni baadhi tu ya miitikio kwenye mtandao wa Facebook na Twita:
Mtumiaji wa Facebook, Berniemack Arellano aliuliza kama kosa hilo ni ujanja wa kutangaza filamu:
Wapendwa Facebook,
Has the President and the Congress declared war on some country? Ano to, marketing ng Independence Day: Resurgence?
Wapendwa Facebook,
Je, Rais na Bunge limetangaza tunaingia kwenye vita na nchi fulani? Mmefanya nini, mnatangaza Filamu ya Siku ya Uhuru?
Facebook says we're at war. Happy Independence Day, Philippines. May we truly be free. #Kalayaan2016 o #Kasarinlan pic.twitter.com/SktzRNSJMj
— Camille Conde (@Cam_Conde) June 12, 2016
Facebook inasema tuko vitani. Heri ya Siku ya Uhuru, Ufilipino. Na tuwe huru kweli kweli.
Dear @facebook: It's not a happy Independence Day if our flag is like this. Like seriously. pic.twitter.com/fo8U4ffdYu
— Ethel (@econcepcion) June 12, 2016
Facebook: Bendera ionekane hivi na iwe Siku ya Uhuru. Kweli?
Hii ni namna sahihi ya kuonesha bendera ya Ufilipino. Katika historia ya nchi hiyo, sehemu nyekundu ilionekana juu ya bluu wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia mwaka 1941 mpaka 1945.