- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mfalme wa Rumba lenye Mahadhi ya ki-Kongo Afariki Dunia. Tunamkumbuka kwa Hili

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Cote d'Ivoire, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Muziki, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia
Papa Wemba, December 30, 2015. Photo: Flickr user dicap ipups / CC 2.0. [1]

Papa Wemba, Desemba 30, 2015. Picha: Mtumiaji wa Flickr dicap ipups / CC 2.0.

Mwananamuziki nguli wa ki-Afrika Papa Wemba alifariki dunia mnamo Aprili 24, 2016, jijini Abidjan, baada ya kuanguka akiwa jukwaani wakati wa moja wapo ya maonesho yake ya kimuziki. Alifanya kazi kubwa ya kuutangaza muziki wa ki-Kongo kwenye majukwaa ya muziki ya kimataifa, na alifahamika kwa kuwaibua na kuwakuza nyota wengine wa muziki wa ki-Mataifa, akiwamo Koffi Olomidé na mfalme Kester Emeneya. Siku tatu za maombolezo ya kitaifa zimetangazwa kufuatia kifo chake, na mazishi ya kitaifa yalifanyika mnamo Mei 4, 2016, kwenye Kanisa moja jijini Kinshasa. Zaidi ya watu elfu moja wanasemekana kuhudhuria mazishi hayo:

Pamoja na umaarufu wake mkubwa kwa wapenzi wa muziki wa ki-Afrika, bado hafahamiki sana nje ya bara la Afrika. Kama ndio kwanza umemsikia nguli huyu wa ki-Afrika, hapa kuna dondoo nne za mafanikio yake ya kimuziki.

Mtu Mbunifu wa Muziki

Papa Wemba alipewa jina la utani la Mfalme wa Rumba lenye mahadhi ya ki-Kongo, muziki unaendelea kubadilika na kutengeneza miondoko mipya kama vile Soukous na Ndombolo. Kama jina lake linavyoonesha, rumba lhili la ki-Kongo lina asili ya rumba la ki-Kuba, ambalo lilianza Kongo kwenye miaka ya 1930. Hapa chini ni video ya kipindi cha “Africanités”, kinachotangazwa na kituo cha televisheni cha TV5 Monde, kuonesha historia ya muziki kwa kutumia vibao vinavyokuwa vimechaguliwa:

Mchango wa Papa Wemba na wenzake kwenye mageuzi ya rumba lenye mahadhi ya ki-Kongo kwenye miaka ya 1970 ulikuwa mkubwa, wakati ambao mahadhi ya muziki huo yalianza kutumia vyombo vya kisasa badala ya vile vya asili, pamoja na kuongezwa mapigo ya haraka, yanayochanganywa na miondoko ya wenyeji wa Kongo ikienda sambamba na rumba asili ya Kuba.

Ziara ya Marekani na Ulaya akiwa na Peter Gabriel

Mwaka 1993, Papa Wemba alizuru Marekani ya Kaskazini na Ulaya kwa ziara iliyopewa jina la “Ziara ‘LIve’ ya Siri ya Dunia” akiongozana na Peter Gabriel, ambaye wakati huo alikuwa moja wapo wa nyota wa muziki huo. Papa Wemba alipata utambulisho mkubwa wa Kimataifa. Kwenye video ifuatayo wasanii hao wawili wanaonekana kwenye onesho la “In Your Eyes”. (Papa Wemba anaanza kuimba kwa ki-Lingala kwenye dakikaya 7:40.)

Peter Gabriel anafahamika kimuziki kwa harakati zake za haki za binadamu kwa kupitia taasisi aliyoianzisha, inayoitwa WITNESS [2]. Peter Gabriel alihudhuria mazishi ya Papa Wemba kwa mazingira yanayokaribia usiri.

Capture d'écran de l'émission de Taratata avec l'interview par Nagui de Papa Wemba et de Peter Gabriel [3]

Picha ya ya video ya kipindi cha televisheni kiitwacho Taratata inayomwonesha Nagui akifanya mahojiano na Papa Wemba pamoja na Peter Gabriel


Nyimbo Zisizopitwa na Wakati

Katika kipindi chote cha miaka 40 ya maisha yake ya muziki, Papa Wemba alirekodi ‘vibao’ vingi vilivyojipatia umaarufu mkubwa. Hapa unaweza kuona baadhi ya nyimbo zake maarufu zaidi:

Yolele:

Maria Valencia:

Show Me the Way:

Papa Wemba alikuwa maarufu kwa kushirikiana na nyota wengi wa muziki wa ki-Afrika,mmoja wapo akiwa Koffi Olomide, mfano katika wimbo wa “Wake Up”:

Akiwa na Extra Musica kwenye ‘kibao’ cha Etat Major:

Muziki Wake Umebeba Ujumbe wa Kiutamaduni

Katika miaka ya 1970, Papa Wemba alitengeneza vuguvugu aliloliita “SAPE”, ambacho ni kifupi cha maneno Société des Ambianceurs et des Personnes Elégantes (au ‘Wazee’ wa Mitoko na Watanashati). (Neno hili ndio chanzo cha neno “sapé” la ki-Faransa, ambalo lina maana ya mtu mwenye maneno mengi lakini mtanashati.) Papa Wemba alipenda kuvaa kitanashati na, kuwa wakati alifahamika kama Mfalme wa Sape. Kongo kwa sasa ni inafahamika kama nchi inayoongoza duniani kwa utanashati, shukrani kwa sehemu zinamrudia Papa Wemba. Dokumentari ifuatayo ina maelezo ya kina kuhusu asili ya jina la utani la ‘Mfalme wa Sape':

Na hivyo tumempoteza Papa Wemba, mwanzilishi wa rumba la ki-Kongo na ‘Mfamle wa Sape”. “Kwa heri na asante sana kwa msanii huyu,” tunasema sisi wa Global Voices.