‘Biko Zulu’, ‘Wananiita Daktari’ na ‘Hadithi za Mama’ Miongoni mwa Washindi wa Tuzo za Blogu Kenya

Some of the BAKE Awards 2016 winners – L to R, Dr. Claire Kinuthia (theycallmedaktari.com), Maryann Waweru (mummytales.com), Rachael Muthoni (safari254.com), Diana Kaluhi (kaluhiskitchen.com) and Lucia Musau (luciamusau.com). Photo used with permission.

Baadhi ya washindi wa Tuzo za Blogu Kenya (BAKE) kwa mwaka 2016 (Kushoto kwenda kulia: Dk. Claire Kinuthia (theycallmedaktari.com), Maryann Waweru (mummytales.com), Rachael Muthoni (safari254.com), Diana Kaluhi (kaluhiskitchen.com) na Lucia Musau (luciamusau.com). Picha na Umoja wa Wanablogu Kenya (BAKE) na imetumiwakwa ruhusa.

Washindi wa Tuzo za Blogu Kenya 2016 walitangazwa katika dhifa maalum iliyofanyika mnamo Mei 14 jijini Nairobi, Kenya.

Blogu ya Biko Zulu ilitwaa tuzo mbili: Blogu Bora ya mwaka kwa Ubunifu. Washindi wengine walikuwa pamoja na Techweez kwa kundi la Blogu Bora ya Kiteknolojia; Ben Kiruthi kwa Blogu Bora ya Picha; They Call Me Daktari Blogu Bora Mpya; na Hadithi za Mama kwa Blogu Bora ya Masimulizi.

Yakiwa yameanzishwa mwaka 2012 na Umoja wa Wanablogu Kenya (BAKE), Tuzo za Blogu, zinazofahamika pia kama Tuzo za BAKE, hutambua na kutuza wanablogu wanaoonesha uwezo wa kipekee. Mashindano hayo, kwa mujibu wa waandaaji, yako wazi kwa wa-Kenya wote na hata makampuni yanayofanya kazi zake nchini Kenya.

Mashindano yalianza kwa awamu ya kwanza ya kupeleka mapendekezo katika makundi 19 kuanzia Januari mpaka Februari 10, 2016. Kisha majaji walichagua blogu tano bora kwa kila kundi, kabla ya zoezi la kupiga kura mtandaoni halijafunguliwa kwa watu wote mnamo Machi 3, 2016.

 

Tazama orodha kamili ya washindi katika makundi yote 19 kwenye tovuti ya tuzo hizo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.