Zoezi la upigaji kura kwa ajili ya Tuzo za Blogu Bora Kenya 2015 linaendelea. Upigaji kura ulianza mnamo Machi 3 na utaendelea mpaka Mei 1, 2016.
Zoezi hilo lililoanzishwa mwaka 2012 Chama cha Wanablogu Kenya (BAKE), Tuzo la Blogu za Kenya, zinazofahamika pia kama Tuzo za BAKE, zinawatambua na kuwatuza wanablogu mahiri wa ki-Kenya. Mashindano hayo, kwa mujibu wa waandaaji, yapo wazi kwa wa-Kenya na makampuni yote yanayofanya kazi zake nchini Kenya.
Mashindano hayo yalianza na hatua ya kwanza ya kupendekeza majina kuanzia Januari 8 hadi Februari 10, 2016. Kisha majaji walichagua blogu tano bora zaidi kwa kila kipengele, kabla zoezi la upigaji kura halijafunguliwa kuruhusu wananchi kupiga kura kuanzia Machi 3, 2016.
Washindi wa mwaka 2016 watatangazwa kwenye tafrija ya wazi mnamo Mei 7, 2016.
tazama video hii ya mtandao wa YouTube kwa muhtasari wa yaliyojiri kwenye Tuzo za Blogu Kenya 2015:
Kuna vipengele 19 mwaka huu baada ya waandaji kuongeza kipengele kimoja, Blogu Bora ya Imani au Dini.
Tazama orodha ya blogu zinazowania tuzo hizo kwa vipengele 19 kwenye tovuti ya tuzo hizo, na upige kura yako hapa.