Mwanablogu wa Irani Agoma Kula kwa Siku 18, Afya Yake Yazorota Akipambana Kudai Uhuru

Inaweza kuwa posti ya mwisho lakini ninamatarajio ya kupata uhuru wangu tena kwa sababu sina hatia. Maoni hayajibiwi kwa kutupwa gerezani.

Afya ya mwanaharakati na mwanablogu wa kupinga kuminywa kwa uhuru wa kujieleza Hossein Ronaghi Maleki yazorota akipambana kudai uhuru. Alianza mgomo wa kula mnamo Machi 26, kupinga kitendo cha uongozi wa gereza alimofungwa kumnyima huduma stahiki za afya na kudai kuachiliwa huru. Afya yake kwa sasa imezorota kwa kasi na inaendelea kuwa mbaya.

Kwa mujibu wa mawasiliano kati ya baba yake Maleki na Kampeni ya Kimataifa ya Haki za Binadamu nchini Irani (ICHRI), mamlaka “zimemtisha kwamba ikiwa familia yake itapiga kelele kuhusu suala lake basi atahamishiwa kwenye gereza la Rajaee Shahr,” lililoko kwenye mji wa kaskazini uitwao Karaj. Gereza la Rajaee Shahr linafahamika kwa mazingira machafu, hususani kwa wafungwa wa kisiasa. Taarifa zilizopita zinadai kwamba safari za binafsi za watu wanaotaka kumtembelea gerezani zitadhibitiwa, kama sio kuzuiwa.

Alhamisi hii, Aprili 14 itakuwa ni siku ya 20 tangu Maleki aanze mgomo wa kutokula. Wanaomwunga mkono wanaomba jumuiya ya kimataifa ya wanaharakati na wanateknolojia wanaopigania uhuru na upatikanaji wa habari kupaza sauti zao kwa niaba ya Maleki kwa kutumia alama ishara ya #NoJail4Hossein[HosseinHastahiliJela].

Maleki alikuwa akiblogu kwa kutumia jina la uandishi la Babak Khorramdin, jina la mpigania uhuru wa kale wa Persia aliyetoka Azerbaijan (Maleki ni mu- Irani mwenye asili ya Azeri). Ni mtaalamu wa program za kompyuta aliyefanya kazi ya kutengeneza tovuti zinazokwepa udukuzi wa kimtandao.

Ipo mitandao mingi ya wadau wa kimataifa wanaoshughulika na uhuru wa mtandao wa Intaneti na kubuni mbinu za kuwawezesha wa-Irani kupata mtandao wa intaneti. Maleki ni sehemu muhimu wa jamii hii, lakini tofauti na wanaharakati wenzake, kazi yake imemfanya aingie kwenye matatizo.

Maleki alikamatwa Desemba 2009, miezi sita baada ya uchaguzi wa rais wa Irani ulioshutumiwa kwa vitendo vya udanganyifu. Mara baada ya kukamatwa alipelekwa kwenye gereza la Evin, akiishi chini ya ulinzi mkali kwa siku 376 kabla ya kushtakiwa mwaka 2010. Mashitaka hayo yalifanya akahukumiwa kifungo cha miaka 15 kwa mashitaka ya “kueneza propaganda kinyume cha utawala”, “kuwa mwanachama wa kikundi cha inteneti kiitwacho Iran Proxy” na “kumdhihaki kiongozi mkuu wa Iran na rais wa nchi.”

Shitaka langu kuu ni kutetea uhuru wa kujieleza (kinyume cha udhibiti wa habari) na kusababisha nihukumiwe kifungo cha miaka kumi isivyohaki

Maleki aliachiliwa huru 2015 kwa muda mfupi wa miezi sita ili kumwezesha kupata matibabu ya matatizo ya figo, lakini alirudi gerezani mnamo Januari 19, 2016. Alirudishwa gerezani pamoja na ushauri wa Daktari kwamba afya yake hairuhusu kukaa kwenye magereza ya Iran. Ni kawaida kwa wafungwa wa kisiasa na wafungwa wa makosa ya kihalifu kunyimwa huduma za afya.

Kitengo cha utetezi cha Global Voices na washirika wa Iran wanawahamasisha watu wanaoguswa na suala hili kulitangaza kadri inavyowezekana kwa kusambaza habari hii kwenye mitandao ya kijamii, na kwa kutumia alama ishara za #NoJail4Hossein. Miito ya kuachiliwa kwake inaweza kutumwa pamoja na nakala kwa Rais Hassan Rouhani  au Kiongozi Mkuu. Twiti za Kiinegerza zitumwe kwa @HassanRouhani na @Khamenei_ir. Twiti za ki-Persia zitumwe kwa @Rouhani_ir na @Khamenei_fa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.