- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Hivyo Ndivyo Afrika Ilivyo-Twiti Mwaka 2015

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia
A screenshot of a graph showing how Africa tweets.

Picha ya grafu inayoonesha namna Afrika inavyo-twiti.

Portland, kampuni yenye makazi yake jijini London ikishughulika na mawasiliano, imechambua twiti zipatazo bilioni 1.6 kwa kuzingatia maeneo na alama ishara (hashtag) zipatazo 5,000 barani Afrika kwa ajili ya ripoti ya tatu ya “Afrika Ilivyotwiti [1]“.

Ripoti hiyo ina mada 12 zinazogusa namna gani mtandao wa twita unavyohusiana na masuala kama ugaidi barani Afrika, hatua za kukabiliana na Ebola, na maendeleo ya kiuchumi barani humo.

Kampuni hiyo ilitumia nyenzo maalumu ya kuchambua mitandao ya kijamii iitwayo Sysomos [2] ili kukusanya na kuchambua alama ishara zipatazo 5,000. Hata hivyo, haikuweza kukusanya taarifa za Sudani Kusini na Jamhuri ya Kongo kwa sababu ya kukosekana kwa takwimu zake kwenye mitandao ya kijamii.

“Tafiti zetu zilizopita zilionesha kwamba mtandao wa Twita barani Afrika ulikuwa ni kama uwanja wa watu kukutana au kufanyia mazungumzo ya utani. Utafiti huu umeonesha kwamba jukwaa hili linazidi kuwa maarufu likisheheni mijadala makini inayohusu siasa na serikali,” Mark Flanagan, Mkuu wa Maudhui na Mikakati ya Kidijitali ananukuliwa katika taarifa yake kwa vyombo vya habari [3].

Mambo Muhimu Yaliyojitokeza:

Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa twita wamekuwa wakijadili matokeo hayo kwenye mtandao wa Twita kwa kutumia alama ishara ya #HowAfricaTweets [4] [AfrikaInavyoTwiti].

Matukio ya mwanzo ya Ebola yalijadiliwa kwenye mitandao ya kijamii kabla ya tangazo rasmi kutolewa na Shirika la Afya Duniani [WHO] na wengineo.

Waafrika walipaza sauti kwenye matukio machache ya kimataifa kwenye mtandao wa twita ikiwa ni pamoja na kikundi cha Kigaidi cha Dola ya Kiislam [ISIS]

Gabon ni nchi inayotumia Kifaransa Afrika ya Kati, lakini twiti zake tatu maarufu zilihusiana na matukio ya Naijeria

#AfrikaInavyoTwiti
Alama Ishara tano maarufu kutoka Uganda
1. #Uganda [12]
2. #UgandaYaamua [13]
3. #Habari [14]
4. #HabariMpya [15]
5. #MUFC [16]

The small island of Comoros had the highest level of Tweets Per Capita of 0.77 across the continent. #howafricatweets [11]

— Grace Natabaalo (@Natabaalo) April 6, 2016 [18]

Kisiwa kidogo cha Komoro kilikuwa na kiwango cha juu cha twiti kinachofikia twiti 0.77 kwa kila mtu

Ripoti hiyo, kwa ujumla, imepokewa kwa maoni chanya. Hata hivyo, Mwesigwa Daniel, mwandishi wa True Africa [19] alitwiti:

Ripoti hii nayo ni namna nyingine ya kutafuta umaarufu wa haraka. Mengi yameachwa.

Akijibu twiti ya Reed Kramer, Demba Kandeh, mwandishi [21]wa Global Voices, alikuwa na haya ya kusema:

Matokeo yanayofikirisha; inaonekana kama kulinganisha maembe na machungwa, #AfrikaSioNchi