Hivyo Ndivyo Afrika Ilivyo-Twiti Mwaka 2015

A screenshot of a graph showing how Africa tweets.

Picha ya grafu inayoonesha namna Afrika inavyo-twiti.

Portland, kampuni yenye makazi yake jijini London ikishughulika na mawasiliano, imechambua twiti zipatazo bilioni 1.6 kwa kuzingatia maeneo na alama ishara (hashtag) zipatazo 5,000 barani Afrika kwa ajili ya ripoti ya tatu ya “Afrika Ilivyotwiti“.

Ripoti hiyo ina mada 12 zinazogusa namna gani mtandao wa twita unavyohusiana na masuala kama ugaidi barani Afrika, hatua za kukabiliana na Ebola, na maendeleo ya kiuchumi barani humo.

Kampuni hiyo ilitumia nyenzo maalumu ya kuchambua mitandao ya kijamii iitwayo Sysomos ili kukusanya na kuchambua alama ishara zipatazo 5,000. Hata hivyo, haikuweza kukusanya taarifa za Sudani Kusini na Jamhuri ya Kongo kwa sababu ya kukosekana kwa takwimu zake kwenye mitandao ya kijamii.

“Tafiti zetu zilizopita zilionesha kwamba mtandao wa Twita barani Afrika ulikuwa ni kama uwanja wa watu kukutana au kufanyia mazungumzo ya utani. Utafiti huu umeonesha kwamba jukwaa hili linazidi kuwa maarufu likisheheni mijadala makini inayohusu siasa na serikali,” Mark Flanagan, Mkuu wa Maudhui na Mikakati ya Kidijitali ananukuliwa katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Mambo Muhimu Yaliyojitokeza:

  • Naijeria, Afrika Kusini, Ethiopia, Burundi na Misri ziliongoza kwa majadiliano makali zaidi ya kisiasa kwenye mtandao wa Twita.
  • Mijadala ya kisiasa inavuka mipaka ya kitaifa. Kwa mfano, alama ishara kuhusu uchaguzi wa rais Naijeria na mapigano nchini Burundi zilikuwa moja wapo ya alama ishara zilizotumika zaidi kote barani Afrika.
  • Kiingereza ni lugha inayotawala zaidi kwenye mtandao wa Twita barani Afrika. Katika alama ishara 5,000 zilizochambuliwa, asilimia 77 zilikuwa na twiti za Kiingereza. Lugha nyingine maarufu kama Kiarabu na Kifaransa zilizkuwa na twiti chache -asilimia 7 na 4 kwa mtiririko.
  • Mtandao wa Twita unatumiwa kwa kiasi kidogo kwa kampeni za kibiashara barani Afrika kuliko kwenye maeneo mengine duniani.
  • Misri inatwiti zaidi kuliko nchi yoyote barani Afrika ikitawala twiti za Afrika kwa asilimia 28 (ikiwa na twiti zinazofikia milioni 500). Naijeria (twiti milioni 360), Afrika Kusini (twiti milioni 325), Kenya (twiti milioni 125) na Ghana (twiti milioni 70).
  • Rwanda ilikuwa nchi pekee ambayo Rais wake, Paul Kagame, alikuwa miongoni mwa alama ishara maarufu zaidi kwenye mtandao wa twita.

Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa twita wamekuwa wakijadili matokeo hayo kwenye mtandao wa Twita kwa kutumia alama ishara ya #HowAfricaTweets [AfrikaInavyoTwiti].

Matukio ya mwanzo ya Ebola yalijadiliwa kwenye mitandao ya kijamii kabla ya tangazo rasmi kutolewa na Shirika la Afya Duniani [WHO] na wengineo.

Waafrika walipaza sauti kwenye matukio machache ya kimataifa kwenye mtandao wa twita ikiwa ni pamoja na kikundi cha Kigaidi cha Dola ya Kiislam [ISIS]

Gabon ni nchi inayotumia Kifaransa Afrika ya Kati, lakini twiti zake tatu maarufu zilihusiana na matukio ya Naijeria

#AfrikaInavyoTwiti
Alama Ishara tano maarufu kutoka Uganda
1. #Uganda
2. #UgandaYaamua
3. #Habari
4. #HabariMpya
5. #MUFC

The small island of Comoros had the highest level of Tweets Per Capita of 0.77 across the continent. #howafricatweets

— Grace Natabaalo (@Natabaalo) April 6, 2016

Kisiwa kidogo cha Komoro kilikuwa na kiwango cha juu cha twiti kinachofikia twiti 0.77 kwa kila mtu

Ripoti hiyo, kwa ujumla, imepokewa kwa maoni chanya. Hata hivyo, Mwesigwa Daniel, mwandishi wa True Africa alitwiti:

Ripoti hii nayo ni namna nyingine ya kutafuta umaarufu wa haraka. Mengi yameachwa.

Akijibu twiti ya Reed Kramer, Demba Kandeh, mwandishiwa Global Voices, alikuwa na haya ya kusema:

Matokeo yanayofikirisha; inaonekana kama kulinganisha maembe na machungwa, #AfrikaSioNchi

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.