Wachoraji Wazindua Kampeni ya Mtandaoni Kushinikiza Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini Malaysia

Image from Grupa

Picha kutoka kwa Grupa

Kikundi cha wasanii wa uchoraji nchini Malaysia kimezindua kampeni ya mtandaoni ya kutumia mabango ili kushinikiza kupatikana kwa uhuru wa vyombo vya habari mara baada ya serikali kuamuru kufungwa kwa tovuti mbalimbali na blogu ambazo zimekuwa zikitaarifu kuhusu tuhuma za rushwa zinazomhusisha waziri mkuu.

Grafik Rebel Untuk Protes & Aktivisme (Grupa) ilitaarifu kuwa kampeni hii inalenga kuihamasisha jamii kuunga mkono kazi za wanahabari wa kujitegemea:

Tambueni kuwa muda umewadia kwa raia wa Malaysia kudai uhuru wa vyombo vya habari na utumiaji wa mtandao wa intaneti kufuatia matukio ya kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari nchini Malaysia. Ni kupitia mbinu hii, waandishi wengi wa kujitegemea wamekuwa wakikabiliana na changamoto kubwa pale wanaporipoti habari za watunga sheria nchini humo na pia wanahabari wa vyombo vya serikali wanalazimika kutumia majina bandia ya vigogo wa serikali kwa kulazimishwa kufanya hivyo..

Tangu Januari, serikali ya Malasia imeshazifunga tovuti tatu za habari na blogu tatu za mrengo wa kisiasa. Serikali ilifungia tovuti za habari za Medium na Asia Sentinel kwa kuchapisha habari ambayo hapo awali ilichapishwa na tovuti ya Sarawak Report, habari iliyohusu tuhuma za rushwa zilizomhusisha Waziri Mkuu Najib Razak. Tovuti ya Sarawak Report ilipigwa marufuku nchini Malasia mwaka 2015. Wiki mbili zilizopita, tovuti ya The Malaysia Insider ilifungwa kwa kile kilisemwa kuwa ni kuchapisha taarifa ‘isiyokuwa imethibitishwa’ iliyohusu kesi ya rushwa ya Najib.

Najib is anatuhumiwa kupokea zaidi ya dola la kimarekani milioni 600 kutoka kwa taasisi ya serikali ya uwekezaji. Najib amekanusha hili na kusema kuwa kiasi cha fedha kilichopo kwenye akaunti zake za benki ziliokana na michango ya ushirikiano wa kisiasa kutoka kwa familia ya kifalme ya Mashariki ya Kati. Jambo hili lilichochea kutokea kwa maandamano makubwa nchini Malaysia na pia baadhi ya washirika wake wa karibu walimtaka Najib kujiuzulu.

Wanaharakati pamoja na viongozi wa vyama vya siasa wanaamini kuwa kusimamishwa kwa baadhi ya magazeti pamoja na kuzifungia tovuti ni moja ya mipango ya serikali ya kuficha upatikanaji wa taarifa kuhusu kesi hii ya rushwa.

Hata watumiaji wa mitanado ya kijamii wanalengwa na mamlaka za serikali. Blogu za OutSyed The Box, Din Turtle na Minaq Jingo Fotopages zilifungwa mara baada ya kuikosa vikali serikali. Tume ya Mawasiliano na Vyombo vya Habari (MCMC) ilitoa vitisho kwa watumiaji wa mtandao watakaojaribu kuchapisha jumbe za dhihaka dhidi ya Najib. Katika hali ya kustaajabisha, ilikuwa pia tovuti ya Grupa iliyosambaza ujumbe wa kejeli na baadae polisi kumtaadharisha mwanaharakti ambaye ni msanii wa uchoraji kuwa tovuti ya Grupa inachunguzwa kwa kutuma ujumbe wa kejeli wa Najib kupitia mtandao wa Twitter.

Kampeni ya Grupa dhidi ya kudhibitiwa kwa watumiaji wa mtandao wa intaneti inatilia mkazo viungo habari vya #‎freethemedia na‬ ‪#‎bebasmedia (Viachie huru vyombo vya habari)‬.

Yafuatayo ni baadhi ya mabango yaliyopakiwa kwenye ukurasa wa Facebook wa Grupa pamoja na kwenye kurasa za Twitter:

Grupa asserts that the media should not simply broadcast government propaganda, especially those coming from the Prime Minister's Office (PMO). Image from Grupa

Grupa yatanabaisha kuwa vyombo vya habari havipaswi kutangaza propaganda za serikali, hususani propaganda kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu(PMO). Picha kutoka Grupa

Image from Grupa

Picha kutoka Grupa

Image from Grupa

Picha kutoka Grupa

Image from Grupa

Picha kutoka Grupa

Activists are calling for the review of the law passed in 1998 which gives broad powers to the Malaysian Communications And Multimedia Commission (MCMC) to censor and block news portals. Image from Grupa

Wanaharakati wanashinikiza kupitiwa upya kwa sheria iliyopitishwa mwaka 1998 iliyoipa mamlaka makubwa Tume ya Mawasiliano na vyombo vya Habari ya Malasia ya kudhibiti na kufunga vyombo vya habari. Picha kutoka Grupa

Image from Grupa

Picha kutoka Grupa

Image from Grupa

Picha kutoka Grupa

Image from Grupa

Picha kutoka Grupa

Image from Grupa

Picha kutoka Grupa

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.