Wa-Cuba Watafakari Ziara ya Obama Jijini Havana

"Cuba and Obama reestablish relations." Cartoon via Linhas Livres.

“Mahusiano Mapya kati ya Cuba na Obama.” Katuni na Linhas Livres.

“Mustakabali wa Cuba utaamuliwa na wa-Cuba wenyewe.” Akiongea jijini Havana mnamo Machi 21, 2016, Obama aliapa kwamba vikwazo vya kibiashara vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Cuba “vitaondoshwa” na kadhalika alionesha nia ya kuheshimu maamuzi ya wa-Cuba kuhusiana na mustakabali wa nchi yao.

Wakati sauti ya Obama ilionesha kubadilisha mwenendo wa marais wa zamani wa Marekani, uangalifu wake katika kuchagua maneno uliwaacha watumiaji wengi wa mitandao wakijiuliza Obama alimaanisha nini aliposema “wa-Cuba”.

Mwanablogu mtetezi wa misimamo ya serikali Iroel Sanchez alijibu, kwa kuuliza:

#‎ObamaenCuba‬ ha dicho que el destino de ‪#‎Cuba‬ es asunto de los cubanos. El problema es cuáles cubanos ¿la minoría que el quiere “empoderar” haciéndolos dependientes de los negocios con ‪#‎EEUU‬ o todos los cubanos?

Obama anasema kwamba mustakabali wa Cuba ni jukumu la wa-Cuba kuamua. Tatizo ni hili, anawazungumzia wa-Cuba wepi –wachache anaotaka “kuwawezesha” wategemee biashara za ki-Marekani? Au wa-Cuba wote?

Wa-Cuba waishio kwenye kingo za Mfereji wa Florida wanatazama kwa makini juma hili ambapo Rais Barack Obama anakuwa rais wa kwanza aliye madarakani kuitembelea nchi hiyo tangu mwaka 1928. Mamia ya waandishi wa Marekani wanaoripoti ziara hiyo wanaonekana kama vile wanasita sita wanapo-twiti na kuripoti chochote iwe biashara ama malazi ya AirBnB au mashindano ya Mpira wa Mikono ya Industriales – Tampa Rays yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Wakati huo huo, wa-Cuba wanaoishi kwenye kisiwa hicho (angalau wale wenye mtandao wa intaneti) na walio nje ya kisiwa hicho wanafanya uchambuzi wa kina kuwakosoa viongozi hao wawili.

Akiiandikia La Joven Cuba, blogu inayoendeshwa na wanafunzi wa chuo kikuu wenye mazoea ya kuunga mkono serikali ya Castro, Jesús López Martínez alipendekeza kwamba badala ya kumruhusu Obama “kuleta maono ya namna ya kusonga mbele” kwa Cuba, viongozi wa Cuba lazima wamfundishe Obama manufaa ya mfumo wao:

Podemos ofrecerle experiencias en el campo de la salud para que las lleve a su país donde millones de personas no tienen atención médica. Que quiere hablar de derechos humanos, pues enseñémosle como actúa nuestra policía y a lo mejor puede evitar que sus gendarmes maten los negros a mansalva en el país del norte.

Tunaweza kutoa uzoefu wetu katika masuala ya afya ya jamii, uzoefu ambao anaweza kuupeleka kwa nchi yake, ambako mamilioni ya watu hawana uhakika wa huduma za afya. Kama anataka kuzungumzia haki za binadamu, tunaweza kumfundisha namna polisi wetu wanavyofanya kazi zao, ili aondoe mauaji wa watu weusi yanayofanywa na polisi wao wenyewe.

Wakati watumiaji wengi wa mtandao wa Twita waliunga mkono mtazamo huo wa Martínez kuhusu afya ya jamii, idadi kubwa ya polisi kwenye maeneo ya mengi jijini humo na matukio ya kukamatwa kwa wanaharakati wanaoipinga serikali kabla la baada ya ziara [ya Obama] ilififiisha hoja yake ya pili.

Kwa hakika, ziara hiyo imeambatana na matukio ya kukamatwa na kuwekwa kizuizini kwa baadhi ya wakosoaji wakuu wa serikali ya Castro wanaoishi nchini humo. Aidha, vyombo vingi vya habari viliripoti kuhusu matukio ya ukamataji yaliyofanyika Jumapili mchana ambako Damas de Blanco (Wanawake Wavaao Mavazi Meupe), umoja wa wake na mama wa wafungwa wa kiume nchini Cuba ambao huendesha maandamano mara kwa mara –na kujikuta baadhi yao wakikamatwa na vyombo vya dola –katika maeneo ya wazi jijini Havana.

Wakili maarufu wa haki za binadamu Elizardo Sánchez aliwekwa kizuini wakati akiwa njiani kwenda Havana siku ya Jumamosi, alikokuwa amekusudia kukutana na Obama. Sánchez anakadiria kwamba wa-Cuba 180 wamekamatwa kabla na baada ya ziara hiyo mpaka sasa.

‘Nchi ngapi zinaheshimu haki zote za binadamu? Hakuna hata moja.’

Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari viongozi hao wawili –tukio nadra kutokea kwa Castro — suala la haki za binadamu lilijitokeza mara kadhaa. Mwandishi maarufu wa televisheni nchini Marekani Andrea Mitchell aliwauliza viongozi hao wawili namna nchi hizo zinavyoweza kufanya kazi kwa kuangalia tofauti zao kwenye suala hilo. Baada ya majibu ya Obama, Castro alisema:

Nchi gani inaheshimu [haki zote za binadamu]? Unajua ziko ngapi? Mimi ninajua. Hakuna. Hakuna hata moja.Baadhi ya nchi zinaheshimu baadhi ya haki, nyingine zinaheshimu haki nyingine. Na sisi ni miongoni mwa nchi hizo. Kati ya maeneo 61 ya haki za binadamu, Cuba imeheshimu maeneo 47. Zipo nchi zinaweza kuheshimu maeneo mengine zaidi, kadhalika, zipo zinazoheshimu maeneo machache zaidi. Ninadhani masuala ya haki za binadamu yasifanyiwe siasa.

Castro aliendelea, akasifia mifumo ya huduma za afya na elimu na sera inayofanya malipo sawa kwa jinsia zote kuwa suala la lazima.

Baadae kidogo, mwandishi aliuliza kama serikali ya Cuba inakusudia kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa. Raúl Castro alionesha wasiwasi wake kama kweli kuna wafungwa wa kisiasa nchini Cuba, kisha akajibu: “Nipe orodha ya wafungwa wa kisiasa na nitawachilia,” kisha akagoma kuendelea kuzungumzia suala hilo.

Ndipo, wa-Cuba na wa-Cuba Wamarekani kwenye mtandao wa Facebook na Twita wakaanza kusambaza kila namna ya matoleo ya orodha kama hiyo. Mwanateknolojia na mwanablogu Eliécer Avila alibainisha kwamba jibu la Raúl ni ushahidi wa kukosekana kwa mchakato yakinifu ya kisheria nchini Cuba:

Demuestra que aquí no hay ley ni sistema judicial más que su voluntad, por eso afirma confiado que si le pasan una lista de presos políticos “estarían en la calle esta tarde”.

…Inaonesha kwamba hapa hakuna sheria wala mfumo wa kimahakama unaoweza kuwa juu ya matakwa [Castro], ndio maana aliahidi kwa ujasiri kwamba kama angepewa orodha ya wafungwa wa kisiasa, “watarudi mitaani leo leo.”

Taarifa nyingi zimeenea kuonesha kwamba polisi wa nchi hiyo waliongeza udhibiti dhidi ya wakosoaji wa utawala wa nchi hiyo. Mtetezi wa demokrasia na mwanachama wa baraza la Vuguvugu la Kikristo la Ukombozi [CLM] Rosa María Rodriguez alielezea tahadhari zilizotolewa na serikali wakati wa ziara hiyo kama “viashiria vidogo tu.” “Hakuna kinachoendelea bila wao kujua,” alisema.

Taasisi ya Rodriguez, ambayo ipo nchini Cuba, ilianzishwa na Oswaldo Payá, mtetezi wa demokrasia anayefahamika kwa kushinikiza mabadiliko ya kidemokrasia katika katiba ya Cuba mpaka alipofariki kwa ajali ya gari katika mazingira ya kutatanisha mwaka 2012.

‘Obama anaongea lugha ya demokrasia ya karne ya 21′

Wakosoaji wengi, zaidi wakiandika kutoka nje ya Cuba, walizungumzia maana ya taswira na utambulisho wa kisiasa wa Obama katika mazingira ya Cuba. Inamaanisha nini, waliuliza, kwa wa-Cuba kumwona rais kijana, mweusi akichaguliwa kwa mihula miwili nchini Marekani, wakati uongozi wa juu wa serikali ya Cuba bado umetawaliwa na wazee weupe wenye umri wa miaka 70 na 80? Takwimu za Sensa zinaonesha kwamba asilimia 14 ya idadi ya watu Marekani ni weusi au wenye rangi mchanganyiko, wakati ikikadiriwa kwamba asilimia 36 ya idadi ya watu nchini Cuba ni ama weusi au “mestizo” (chotara).

Akiandikia Huffington Post, Mmarekani mtaalam wa sosholojia na masuala ya Cuba Ted Henken alitafakari suala la ubaguzi wa rangi kwenye mataifa hayo ya Marekani na Cuba, akimwelezea Obama kama “alama imara” ya mafanikio ya Marekani katika “Haki na usawa wa makundi ya rangi,” wakati huo huo akikubaliana kwamba Marekani bado ina “safari ndefu.”

Akiandika kwa ajili ya El Pais, mwanahistoria wa Cuba na mwandishi anayeishi Mexico Rafael Rojas aliichambua dhana ya Obama kama alama ya maendeleo sio tu kwenye eneo la ubaguzi wa rangi, lakini kama mtu “anayezungumzia lugha ya demokrasia ya karne ya 21″:

Obama encarna muchas cosas que la ciudadanía joven de la isla valora positivamente después de 56 años de comunismo: el ascenso social y político de los afroamericanos en Estados Unidos, la apuesta por una gestión pública en beneficio de las mayorías, un ejercicio diplomático que prioriza la negociación de conflictos, un demócrata del siglo XXI que habla el lenguaje de las democracias del siglo XXI. Pero Obama es, además, la prueba viviente de algo que la juventud cubana tiene que ver con una mezcla de extrañeza y fascinación: un político que abandona el poder a los 55 años, la edad que tienen los sucesores más jóvenes de los octogenarios gobernantes de la isla…

Obama ni sura ya masuala mengi ambayo wa-Cuba vijana visiwani humu wanayathamini baada ya miaka 56 ya ukomunisti: kuinuka kijamii na kisiasa kwa wa-Afrika Weusi nchini Marekani, hatua mbele kwa sera za nchi zinazoweza kuwanufaisha wananchi wengi…mwanademokrasia wa karne ya 21 anayeongea lugha ya demokrasia ya karne ya 21. Lakini pia Obama ni ushahidi hai wa kile ambacho wa-Cuba wanapaswa kukiona kama mchanganyiko wa matamanio na mshangao: mwanasiasa anayeachia madaraka akiwa na miaka 55, umri ambao ni wa mdogo zaidi miongoni mwa vikongwe wanaotawala visiwa hivyo…

Waumini wa u-Marx walia na tabia ya serikali kudhibiti mazungumzo ya wazi

Observatorio Crítico, msomi wa kikomunisti na mwanablogu alileta tazamo tofauti wenyekukosoanamna mamlaka za Cuba zilivyoshughulikia ziara hiyo, akitumia mtazamo wa ki-Marx:

En situaciones como la visita de Obama a nuestro país se impone evitar manifestaciones de confrontación, pero reivindicamos la necesidad de distinguir entre los protocolos de gobierno y las expresiones del pueblo.

Es indispensable que las organizaciones de masas y otras expresiones de la sociedad civil puedan realizar agitación política ante la visita de mandatarios como Obama y François Hollande, o ante las arbitrariedades cometidas por gobiernos con los que se tienen relaciones económicas prometedoras.

Katika mazingira kama haya ya ziara ya Obama, nchi yetu inatakiwa kukwepa kuonesha migogoro au misuguano, lakini ikihitajika kulinda umuhimu wa kutofautisha protokali za kiserikali na kusema kinachotakiwa kusemwa hadharani.

Taasisi za kijamii na mashirika mengine ya kiraia yanayopaza sauti hazikwepeki katika mchakato wa kusaidia kufikia uelewa mpaka wa masuala ya kisiasa pale ziara za kiserikali zinapofanywa na viongozi kama Obama na François Hollande, ama katika mazingira ya tunayoyaona ambapo hatua za vitisho zinachukuliwa na serikali hizi dhidi ya taasisi zile zile ambazo serikali hizi zinadai kutaka kuimairisha mahusiano ya uchummi nazo.

Observatorio Critico anabainisha suala muhimu hapa: Pamoja na kutokukubaliana katika masuala ya haki za kibinadamu na sera za kijamii, mwisho wa siku, kufufuka kwa mahusiano kati ya Cuba na Marekani kunaweza kuwa kumechochewa na imani inayofanana kwamba mabadiliko ni muhimu yalete maslahi ya kiuchumi pande zote.


Tembelea ukurasa maalumu wa Global Voices kuhusu Mahusiano ya Marekani na Cuba.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.