- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Umesikia? Podikasti ya Global Voices Imerejea

Mada za Habari: Amerika Kusini, Asia Mashariki, Asia ya Kati, Ulaya Mashariki na Kati, China, Macedonia, Mexico, Tajikistan, Urusi, Censorship, Filamu, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Podikasti za Global Voices

Baada ya mapumziko ya miaka mitatu, Podicasti ya Global Voices sasa imerejea. Ujio huu mpya tunauita “Wiki Iliyokuwepo Global Voices”

Kwenye toleo hili, Mhariri wa Habari wa Global Voices, Lauren Finch pamoja na mimi — Mhariri Mtendaji wa Global Voices– tunakupeleka hadi Mexico, China, Tajikistan, Macedonia na Urusi.

Nchini Mexico, tunakupa simulizi kuhusu Arne Aus den Ruthen, mtumishi wa umma, raia wa Mexico, atumiaye Periskopu [1] kuwaumbua wavunja sheria, simulizi inayoletwa kwetu na mwandishi wa Global Voices J.Tadeo.

Pia, tutakupa habari kuhusu simulizi yetu ya wiki ya udhibiti wa mtandao [2] kutoka China, ambapo mhariri wetu wa Asia ya Kaskazini Mashariki, Oiwan Lam alitudokeza. Baadae tutakupeleka hadi Tajikistan, pia Macedonia ambapo tutakuwa na maongezi na mhariri wetu wa RuNet Echo, Kevin Rothrock kuhusu filamu mpya inayobeza Harry Potter na kuonesha hali ya  Wasiwasi wa Uzalendo wa Urusi [3].

Tuna furaha ya kipekee kurudisha tena Podikasti ya Global Voices.  Shukrani nyingi kwa waandishi wetu, watafsiri makala, na wahariri waliotusaidia kufanikisha kutolewa kwa makala haya.

Katika toleo la wiki hii la Global Voices, tumezungumzia muziki uliopewa ithibati ya Creative Commons kutoka kwenye hifadhi ya Muziki wa Bure, ikiwa ni pamoja na Please Listen Carefully na Jahzzar [4]Mexico by Jimmy Pe [5], Air Hockey Saloon na Chris Zabriskie [6],>Rainbow Street na Scott Holmes. [7] Simulizi ya Tamasha la Kirusi na bendi ya The Freak Fandango Orchestra. [8]

Tunatarajia kusikika tena wiki mbili zijazo.