Mwanaharakati wa Haki za Binadamu na Kiongozi wa Jamii za Wazawa Berta Cáceres Auawa nchini Honduras

Photo: Berta Caceres in interview with the media Venas Abiertas. Screenshot taken from the video, available on Youtube.

Berta Caceres katika mahojiano na kituo cha habari cha Venas Abiertas. Picha: Youtube.

Baada ya kufanya uanaharakati wa mazingira na kuzipigania jamii za wazawa, mtetezi nguli wa haki za binadamu Berta Caceres aliuawa nchini Honduras manamo tarehe 3 Machi, kama ilivyotaarifiwa na SOAWatch:

Takribani saa sita za usiku, Mkurugenzi Mkuu wa COPINH, Berta Caceres aliuawa katika mji wa La Esperanza, Intibuca. Watu wanaokadiriwa kufikia wawili walivunja mlango wa nyumba alipokuwa anaishi Berta, ya Residencial La Líbano na kisha kumpiga risasi na kumuua.

Akifahamika ulimwenguni kote kwa uanaharakati wake, mwaka jana Caceres alishinda Tuzo ya Mazingira ya Goldman  kwa kufanikiwa kushinikiza kusitishwa kwa ujenzi wa bwawa kubwa la maji ya mto. Sambamba na mafanikio yake, kulikuwamo pia na vitisho vingi vya kifo, kama inavyowekwa bayana kwenye  mkutano na vyombo vya habari  ulioambatana na tuzo yake:

Kumekuwa na vitisho vya vifo visivyoisha dhidi ya Cáceres. Mauaji yake yasingekuwa ya kushangaza sana miongoni mwa wenzake, ambao walikuwa wakimsifia sana pamoja na kujua hatari zilizokuwa zikimkabili. Hata hivyo, pamoja na hatari zote hizi, alionekana majukwaani akiendelea na majukumu yake. Katika nchi inayoweka rekodi ya kuwa na matukio mengi ya mauaji duniani, Cáceres alitegemea ushindi alioupata Agua Zarca ungeleta matumaini kwa wanaharakati wanaopinga ujenzi holela nchini Honduras na sehemu nyingine yoyote ya Amerika ya Kusini.

Taasisi ya “Witness for Peace” iliainisha magumu ambayo Caceres alikabiliana nayo pale alipokuwa akipinga kujengwa kwa bwawa:

Kufuatia suala la kutekwa kimamlaka kwa serikali ya Hodnuras na Marekani mwaka 2009, umilikishaji wa ardhi ya Hodnuras pamoja na maliasili kwa makampuni ya nje na ya ndani ulishamiri. Kwa mfano, serikali iliyoporwa mamlaka ilimilikisha mitambo 47 ya kufua umeme kwa kutumia sheria moja, bila ya kuzishirikisha jamii ambazo zingepatwa na athari ya moja kwa moja, na hivyo serikali ikawa imevunja makubaliano ya kimataifa ikiwamo sheria namba 169 ya makubaliano ya Shirika la Kazi Duniani (ILo) inayolitaka Taifa la Honduras kutetea ardhi ya wazawa na maliasili ikiwa ni pamoja na matumizi ya nguvu ya kuwahamisha raia.

Siku chache tu zilizopita, taasisi ya Caceres COPINHHONDURAS, ilipaza sauti kukemea ukandamizwaji wa jamii za wazawa na kutoa ushuhuda wa uporwaji mali wa jamii ya Lenca:

Mfulizo wa uporwaji mali: mashamba yanaendelea kuporwa kutoka kwa raia wa Honduras wa jamii ya Lenca

Mfuatiliaji maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za raia wazawa pia ameshataarifu udhalilishaji unaofanywa dhidi ya jamii za wazawa wa Lenca na harakati zao za kudai mazingira rafiki. Katika safari yake ya hivi karibuni nchini Hodnuras, alifafanua :

Kitika kutembelea kwangu na kuchuguza hali halisi ya raia wazawa, nilishudia hali tete iliyokuwa inawakabili hususani kwenye suala la haki ya ardhi yao na mali asili, machafuko, upatikanaji wa amani na rushwa, kokosekana kwa utetezi wa kimahakama, pamoja na kukosekana kwa huduma za msingi za kijamii kama vile elimu na huduma za afya.

Nchi ya Honduras, inayokabiliwa na tatizo sugu la rushwa, ina historia mbaya sana haswa kwenye matukio ya mauaji ya  wanaharakati wa mazingira na wanawake. Mashirika kutoka ulimwenguni kote yanaitaka serikali ya Honduras kuchukua hatua stahiki mapema kuyatafutia suluhisho mambo ambayo Caceres aliyapigania. Wanaharakati pia wanaziomba nchi nyingine kushinikiza viongozi wa serikali ya Honduras, ambao hivi karibuni walizindua Tume ya Honduras ya Kudai Amani .

Kuna matumaini kuwa tume hii inaweza kuwa ni fursa ya serikali kuonesha utayari wake wa kisiasa. Kwa sasa, jambo lililo dhahiri mara baada ya masahibu ya mauaji ya Caceres ni kuona serikali inabuni mbinu za kusaidia kukabiliana na wimbi la machafuko, rushwa na kupatikana kwa amani

3 maoni

Sitisha majibu

jiunge na Mazungumzo -> mussa hassani

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.