- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mchora Katuni Snoggie Achambua Siasa za Uganda kwa Kutumia Ucheshi

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Uganda, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchaguzi, Vichekesho
A compilation of some of Snoggie's work.

Baadhi ya katuni za msanii Snoggie

Uchaguzi wa hivi karibuni nchini Uganda uligubikwa na mihemuko, matukio ya watu kukamatwa, na madai ya udanganyifu [1]. Masuala haya si ya kuchekesha kwa hakika, lakini bado kuna namna yanaweza kukufanya ukacheka. Muulize Snoggie [2], mmoja wa wachoraji maarufu wa katuni za kisiasa nchini humo, ambaye ametoa maoni mara kadhaa katika kipindi cha zoezi la upigaji kura.

Wa-Ganda walipiga kura kumchagua rais, wabunge na madiwani mnamo Februari 18, 2016. Tume ya Uchaguzi ya Uganda ilitangaza [3] siku mbili baadae kwamba Rais aliye madarakani Yoweri Museveni [4] alipata ushindi wa asilimia 60.75 ya kura. Mpinzi wake wa karibu Kizza Besigye, ambaye aliwekwa kizuizini mara kadhaa katika kipindi cha kuelekea kwenye uchaguzi, alijipatia asilimia 35.37, na Waziri Mkuu wa zamani Amama Mbabazi alishika nafasi ya tatu kwa asilimia 1.75.

Snoogie huchapisha kazi zake za sanaa kwenye gazeti la kila siku la Uganda pamoja na kuziweka kwenye ukurasa wake wa Facebook, Ulimwengu wa Snoggies kwa Uganda,  [2] ambao una wafuatiliaji wapatao 30,000. Katuni zake zinachambua mwenendo wa siasa zinazoendelea hivi sasa nchini Uganda. Hapa chini unaweza kuona baadhi ya kazi alizoziweka kwenye ukurasa wake wa Facebook.

snoggie 6

Image by Snoggie. Used with permission.

Mtu anayeonekana kwenye kiti cha dereva hapo juu ni mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Badru Kiggundu. Abiria kwenye viti vya nyuma ni viongozi wakuu wa vyama vya upinzani, Amma Mbabazi wa VuguVugu la “Go Forward” [Tusonge Mbele] na Kizza Besigye, anayetumia kauli mbiu ya “Kwa Mabadiliko Tuyatakayo.” Mwenye ramani ni Rais Yoweri Museveni.

snoggie 5

Image by Snoggie. Used with permission.

Rais Museveni alikataa [5] kushiriki mdahalo wa kwanza wa wagombea Urais kwa kusema alibanwa na majukumu mengi. Hata hivyo, alishiriki mdahalo wa pili wa wagombea Urais. Mirundi alikuwa msaidizi wa habari wa Rais Museveni kwa miaka 13.

snoggie 3

Image by Snoggie. Used with permission.

Akiwasilisha hati ya kumfukuza mtu hapo juu ni Kizza Besigye, kiongozi mkuu wa upinzani. Besigye alivuta umati mkubwa wa watu wakati wa kampeni. Watu wengi walitarajia kwamba Museveni alikuwa anaelekea kushindwa kabla matokeo ya uchaguzi hayajatangazwa.

snoggie 4

Image by Snoggie. Used with permission.

Baada ya uchaguzi, kulikuwa na idadi kubwa ya polisi na vikosi vya majeshi mitaani. Tofauti na ilivyokuwa kwenye chaguzi nyingine, mitaa haikuwa na watu wanaosherehekea ushindi [6].

snoggie 2

Image by Snoggie. Used with permission.

Afande tafsiri yake ni afisa wa polisi , na Dk. Badru Kiggundu ni mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi. Mtu aliyechini ya ulizi wa afisa wa polisi ni Kizza Besigye, aliyekamatwa mara nne kati ya tarehe 15-23 Februari. Aliwekwa chini ya ulinzi nyumbani kwake [7] baada ya matokeo kutangazwa.

Snoggie 1

Image by Snoggie. Used with permission.

Uganda ni nchi pekee kwenye eneo la Afrika Mashariki isiyo na ukomo wa mihula ya urais. Kiufundi, Museveni anaweza kugombea urais kwenye uchaguzi wa 2021.