- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Polisi wa Kidini Thelathini Nchini Saudi Arabia Wahitimu Mafunzo ya Kukabiliana na Uchawi

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Saudi Arabia, Dini, Sheria, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vichekesho
Hogwarts headmaster Professor Dumbledore reacts to the news saying "Bring it on!" Photo source: Hummus for Thought Facebook page [1]

Mkuu wa Hogwarts, Profesa Dumbledore avijibu vyombo vya habari kwa kusema “Uwekeni bayana!” Chanzo cha picha: Ukurasa wa wa Facebook wa Hummus for Thought

Polisi watukutu wa nchini Saudi Arabia wanatarajia kupata utaalam wa masuala ya uchawi kama ule alionao Profesa Albus Dumbledore [2], ambaye ni mkuu wa shule ya Hogwarts. Wajumbe thelathini wa Tume ya Kusimamia Maadili na Kukabiliana na Maovu [3] wamehitimu mafunzo ya siku tano [4] ambayo yanatarajiwa kuwawezesha kukabiliana na uchawi, kuwatambua walozi na hata kuvunja laana zao.

Bila hata kusemwa, kujihusisha na uchawi ni jambo linalopingwa vikali kwenye Falme za Wahafidhina halisi, ambapo yeyote atakayekutwa na hatia ya kujihusisha na uganga na ulozi ananyongwa.
Kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu,UAE, mchambuzi Sultan Al Qassemi anasema:

Wengine waliliangalia jambo hili kwa kufananisha na yale yaliyokwishafanywa na wengine na kujaribu kuwaiga, mfano ukichukuliwa kutoka kwa J K Rowling's [7] mwandishi mashuhuri wa makala za riwaya ya Harry Potter [8].

Nadim Rifai alimtwiti mwandishi wa riwaya moja kwa moja kwa kusema:

Pia, Hassan Cha anasema kuwa kuwapatia mafunzo haya polisi wa kidini ni “toleo la Harry Potter lililosanifiwa”:

Ukiweka pembeni Harry Potter, inaonekana kuwa programu kama hizi zilishaanza kitambo. Mtumiaji mmoja wa Facebook alichapisha makala iliyoandikwa mwaka 2013 [14] iliyokuwa inazungumzia mafunzo yanayofanana na haya. Kiuhaliasia, kupambana na ulozi [15] ni moja ya maeneo muhimu matano ambayo polisi wa kidini wanapaswa kuyashughulikia wawapo kwenye majukumu yao. Mambo mengine manne ni: “kuulinda Uislam, kuzuia kushurutisha mtu kutoa taarifa zake, kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu pamoja na kuhakikisha kuwa hakuna yeyote anayekaidi kuwatii watawala.”