Mfahamu Fish, Mkazi Katika Kambi Kubwa ya Wakimbizi Duniani

Abdullah Hassan, known as Fish, lived at the Dadaab refugee camp in Kenya for 23 years. Credit: Abdullah Hassan/Courtesy

Abdullah Hassan, anayefahamika kama Fish, aliishi katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya kwa miaka 23. Picha kwa hisani ya: Abdullah Hassan/Courtesy

Makala hii iliyoandaliwa na Rachel Gotbaum kwa ajili ya The World kwa mara ya kwanza  ilichapishwa kwenye tovuti ya PRI.org tarehe 18 Februari, 2016, na inarudiwa kuchapishwa hapa kwa makubaliano ya kushirikiana maudhui.

Abdullah Hassan, ambaye jina lake la utani ni Fish alikuwa na umri wa miaka 7 pale baba yake alipouawa na wanamgambo nchini Somalia. Na ndipo aliposafiri kuelekea kwenye kambi ya wakimbizi ya Dadaab.

Wakiwa njiani, kaka wawili na dada yake Hassan walipoteza maisha kwa ugonjwa wa utapia mlo. Yeye na mama yake walipowasili kambini hapo, mazingira ya kambi hayakuwa yakuridhisha.

Kambi hii ilianzishwa mwaka 1992 kwa ajili ya kuwahifadhi wakimbizi 90,000 wa Somalia waliokuwa wakikimbia vita vya kiraia nchini humo.

Hadi sasa, kuna miundo mbinu hafifu sana ya maji au maji yanayotiririka, na pia shirika linaloshughulika na wakimbizi limepunguza sana ugawaji wa vyakula kambini hapo. Wakimbizi wengi wameshafariki kwa sababu ya kukosa chakula. Kumekuwa pia na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwa sababu ya idadi kubwa ya wakimbizi pamoja na mfumo hafifu wa uwekaji safi mazingira.

Mke wa Fish alifariki kwa vidonda vya tumbo kutokana na kukosa matibabu stahiki.

Fish's work with the Danish Refugee Council is considered volunteerism due to his refugee status. Credit: Abdullah Hassan/Courtesy

Fish kufanya kazi na Baraza la Wakimbizi la Kidenishi inachukuliwa kuwa ni kujitolea kutokana na hali ya yeye kuwa ni mkimbizi. Picha kwa hisani ya: Abdullah Hassan/Courtesy

Wakimbizi hawaruhusiwi kufanya kazi na wachache sana huruhusiwa kuondoka kambini. Fish anafanya kazi na Baraza la Wakimbizi la Kidenishi, lakini katika hali ya kawaida, hii siyo kazi haswa ya kumuingizia kipato: Baraza hili linampatia Fish hela ya kujikumu tu na hivyo kuchukuliwa kama mtu anayejitolea.

Hadi sasa, kambi ya Dadaab inawahifadhi wakimbizi 500,000 ikiwa na miundombinu chakavu sana na ukubwa wake unalinganishwa na ukubwa wa jiji la New Orleans.

Hivi karibuni, kikundi cha wanamgambo wa Al Shabaab kilivamia kambi hii.

“Tulipata mateso makali sana, kutekwa, kupigwa risasi, magari mengi yalilipuliwa” Hassan anasimulia. “Baadhi ya wenzangu katika jamii ile waliuawa.”

Fish alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa wanalengwa na ilimlazimu kwenda Nairobi, ambapo anaishi hadi sasa bila ya kuwa na kibali. Mara kwa mara amekuwa akikaguliwa na polisi na amekuwa akiwapa hongo ili asikamatwe.

Baada ya kukaa kwenye kambi ya Dadaab nchini Kenya kwa miaka 23, Fish ana matumaini ya kupata mahali pengine palipo na auheni pa kuishi yeye pamoja na watoto wake wa kike ambao bado wanaishi kambini hapo. Anayo matumaini ya kuanza maisha mapya.

“Ninaamini kuwa ninaweza kuimaha Kenya na kupata utulivu mpya” anafafanua. “Ni kusubiria muda tu, Mungu anajibu juu yangu.”

Maisha ya Fish yanajumuishwa kwenye kitabu kipya “City of Thorns” cha Ben Rawlence. Soma zaidi kuhusu kitabu hiki hapa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.